Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,316
- 72,742
Ukisoma kwa makini yaliyo elezwa katika Budget kivuli kwa makini bila kuweka ushabiki wa kisiasa na kwa mapenzi mema ya nchi yetu utaona wazi kuwa Budget ya serikali iliyowasilishwa na Dr Mpango na mtiririko wa zile budget za wizara mbalimbali kabla ya hiyo budget mama utagundua kuwa hii ni bajeti hewa.
Kwa mfano uhalisia wa budget inasemwa ni Trilioni 29 wakati ni Trilioni 22 wanamdanganya nani? Njoo kwenye manunuzi ya hizo ndege za ATCL, fedha za kununulia na hali halisi ni mashaka matupu, hewa. Karibu vipengele vingi ni uongo wa wazi kabisa hewa. Kwa nini hawana woga hawa watu? Au ndio ilikuwa sababu ya kuzuia tusilione bunge nasi huku nje kuhoji hii hewa? Au ndio maana wale wabunge wenye uwezo wa kuhoji wanaundiwa zengwe la kufukuzwa bungeni na wengine kuudhiwa ili wagome kushiriki?
Kuna mtu kanihoji kwamba kama Wapinzani walikuwa na sintofahamu na Naibu spika na wamesema akiwapo yeye hawataingia, kwa vile Spika mwenyewe hayupo kwa nini isitumike busara Wenyeviti hao watatu wakaongoza bunge ili muafaka upatikane na shughuli ziendelee smoothly? Lakini huyo anayekataliwa ndio kang'ang'ania kuwepo ili hao wanaohojihoji watoke.
Hewa, hewa, hewa. Sasa nchi hii tunakoelekea kutakuwa na waume hewa, wake hewa na watoto hewa. Serikali hewa na kila kitu hewa.