Maajabu niliyoyaona WODI ya SEWAHAJI Muhimbili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maajabu niliyoyaona WODI ya SEWAHAJI Muhimbili.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Sep 27, 2012.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Ni mchana wa saa saba, kama kawaida nilikwenda kumjulia hali mgonjwa wangu aliyelazwa wodi ya SEWAHAJI NO 18, Ghafla nilisikia mzozo ambao ilikuwa ni kati Daktari na mgonjwa aliyekuwa amelazwa huku akiwa ametundikwa chuma , nafikiri anatatizo la mguu. Daktari huyo wa kike ambaye alikuwa hajavaa Uniform, alikuwa amevaa kitambulisho ambacho alikigeuza ili isiwe rahisi kutambulika jina lake, hiyo ilikuwa tarehe 24/09/2012. Mgonjwa huyo alikuwa analazimishwa aachie kitanda alale chini kwa kile kilichoelezwa kuwa amelala kwenye kitanda hicho zaidi ya wiki mbili hivyo hana budi kupisha mgonjwa mwenzake naye afaidi. Kimsingi wodi ya SEWAHAJI imefurika watu hata kupita ni shida na uangalizi ni 0 kwani hata drip za damu ambazo tumezoea kuziona zimetundikwa kwenye vyuma maalum nilishuhudia zikiwa zimewekwa sakafuni na damu kutapakaa sakafuni. Mgonjwa huyo ambaye aligomea kitendo cha kushushwa alisababisha mzozo hata hivyo namsifu maana alipinga kitendo hicho kwa nguvu zote japo sijui kama baadaye tulipoondoka ilikuwaje.

  MAAJABU: Baada ya Daktari huyo wa kike kushindwa aliungana na wauguzi wengine, kujadili cha kufanya, ndugu wa mgonjwa aliyekuwa anatakiwa apandishwe kitandani walisogelea wauguzi hao ili kuona kama zoezi limeshindikana au vipi " wauguzi waliwatamkia bila aibu wala kificho ndugu wa mgonjwa kuwa wakitoa Laki moja kitanda kitapatikana" haya kwangu ni maajabu makubwa. Hiyo ndiyo Muhimbili, serikali imegoma kuongeza Posho sasa wauguzi wanasanya. Hivyo kama unamgonjwa wako unataka apate kitanda Muhimbili wodi ya SEWAHAJI andaa Laki vinginevyo atalazwa sakafuni. Hii kitu inayoitwa TAKUKURU kazi zao wanazifanyia wapi? mbona jamani rushwa zipo njenje hivi?
   
 2. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Maskini akiwa kwake analala kwenye kitanda, ila akiugua na kwenda Muhimbili ajiandae kulala chini.
  Wodi za Muhimbili hazikidhi mahitaji hivyo kanuni za uchumi, si za kitabibu, zinaamua nani alale kwenye kitanda na nani alale chini.
   
 3. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Maskini akiwa kwake analala kwenye kitanda, ila akiugua na kwenda Muhimbili ajiandae kulala chini.
  Wodi za Muhimbili hazikidhi idadi ya wagonjwa hivyo kanuni za uchumi, si za kitabibu, zinaamua nani alale kwenye kitanda na nani alale chini.
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo tafsiri ya maisha bora aliyoahidi Kikwete. Ajabu ukiwambia kuwa CCM na Kikwete ni janga la kitaifa unaonekana mchochezi na mtu asiyesifia mafanikio yao. Tuna mafanikio gani zaidi ya wizi na ujambazi mtupu tena vikifanywa mchana kweupe?
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Labda ni maajabu(kwa kuwa hujawahi) kukumbwa na haya mkuu Anold, ..ila ni mambo ya kawaida kabisa katika hospitali zetu..sijui katikahoapitali zilizo pembezoni mwa miji!!
   
 6. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Je wakati wa utawala wa MWINYI na MKAPA watu walikuwa hawalali chini?
   
 7. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mkuu unamaanisha kuwa kwa vile feri toka tunapata uhuru watu wanavuka kwa kuogelea hatuna haja ya kujenga daraja? Ile hosp ilejengwa kuhudumia watu wangapi? Je kwa sasa inakidhi mahitaji, na kama sio ni juhudi gani zinafanyika? Watu kulala chini toka enzi hizo hairuhusu waendelee kulala chini. Yaani kwavile babu yako alilalia kitanda cha kamba nawe ulalie hicho hicho! Think big mkuu.
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kama yanayosemwa ni kweli, basi huenda wagonjwa huuawa ili kutoa nafasi ya kitanda cha kuuza kwa laki moja.
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Tatizo si uwepo wa Takukuru!
  Kwani hili hamkliona likiwa linakuja?
  Dawa ya malari ni ''mseto'
  Panadol inapunguza maumivu, ikiisha nguvu homa na kichwa kuuma viko pale pale
   
 10. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mbona ulimboka alilazwa kwenye kitanda kina mavideo na vimulimuli!!
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  madactar walipogomea haya mliwaita wauwaji wa ndugu zenu sasa meona ,
   
 12. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Na bado!
   
 13. Azizi Mussa

  Azizi Mussa Verified User

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,600
  Likes Received: 2,238
  Trophy Points: 280
  mimi naona watanzania tunawalauumu viongozi tu,lakini kizazi hiki kwa ujumla wake kimeoza kwa asilimia kubwa!suala ni mimi na wewe tuanze kuleta mabadiliko(ikiwa sisi ni watu wema)
   
 14. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  na kweli na bado walijitahidi sana hawa watu watu waliwapinga sana mkasema ni maslahi yao wanadai wao wakajinyamazia wakijua watakula cha juu sasa mnalalama hukutulieni kimya kama mnanyolewa vile ,mlisema sana hapa
   
 15. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  ya chama,yanakujaje apa we mjduufujhweqlwr,mkubwa we,kwa iyo unataka kusema ingekua siyo ccm uyo mgonjwa angelalla kwenye kitanda?
   
 16. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Bila shaka angelala kwenye kitanda nawe hilo unajua. Kama CCM na serikali yake wangewajibika haya yangetoka wapi?Hebu funguka macho uone mambo kama yalivyo badala ya ndoto za Alinacha.
   
 17. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Wonders shall never end. Hapa unakana chama tena wakati nchi hii inaendeshwa na sare na laana sorry sera na ilani ya chama tawala?
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuwaongezea posho madaktari Vs uwepo/upatikanaji wa nafasi na vitanda.........duuh!......au ndio mtuambie mnawajaza wagonjwa kwenye wodi moja ili muuze vitanda/nafasi wodi zingine!!.......duuh
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Wewe unataka TAKUKURU waje kufanya nini hapo? Masikini wauguzi hawawezi kujipangia vikao wala safari ili wapate posho, na kwa vile Mlawi atakula kutoka kwenye madhabahu basi na burudani iendelee.
  Juzi ndugu yetu alivunjika mguu akapelekwa Temeke, dakitari akatuambia wazi bila kificho kuwa bila elfu sitini (exclusive gharama za kawaida) mgonjwa wetu hatahudumiwa siku hiyo kwa kuwa foleni ni kubwa, halafu jeraha litaoza then atakatwa mguu.
  Sasa unafanyaje mshua, utaita hao wapuuzi wako unaowataka au utagawana umaskini mtu wako apone?
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
Loading...