Maajabu: Kichwa cha treni kilichookotwa bandarini ndio kimepata ajali Kigoma. Hivi kumbe walishanunua kimya kimya?

Kwani washamalizana na mnunuzi mpaka wakaanza kutumia,? Maana taarifa yao ya mwisho nakumbuka ni kuongee na mwenyemali.....
 
Kivipo mkuu? Labda sijakuelewa!

HABARI,
"Safari_ni_Safari,
Mada si inazungumzia kichwa cha treni kati ya vile vilivyokuwa havijulikani mmiliki,Sasa kile kichwa Number 9001 Cha bandarini hakifanani na kile kilichopata ajali angalia kwa kina utaona tofauti kubwa na pia kile kilichopata ajali ile Number 9001 sasa hapo hatujui ukweli ni upi.

LUMUMBA
 
Picha ya ajali ni kwa nyuma na ile ya bandarini ni kwa mbele. Obvious hazitafanana. Ni sawa na gari yako tu kwa mbele na nyuma inafanana japo namba ya registration ni ileile?
 
Nani alikudanganya kuwa kila tenda lazima ishindanishwe?

Ni wapi sheria ya manunuzi inasema KILA tenda lazima ishindanishwe?

Haya ndio matatizo ya kukalili maneno!
Unajua sheria ya manunuzi kwenye kununua vitu kama mashine au ndege?
 
Kutokujua wewe kama walishanunua haina maana kuwa hawajasema kama walinunua.

Kwa mfano, kuna mtu anaweza asijue kuwa kuna Dar es Salaam hapa duniani lakini haina maana kuwa haipo au haitangazwi kama ipo.

Tumia hata common sense katika fikra zako.

Pitia hii thread kuhusu tamko la serikali mwezi Oktoba 2017;

LINK>>>Vichwa 15 vya Treni Kununuliwa na Serikali
Ukificha moto mfukono basi moshi itakuumbuwa
 
Kutokujua wewe kama walishanunua haina maana kuwa hawajasema kama walinunua.

Kwa mfano, kuna mtu anaweza asijue kuwa kuna Dar es Salaam hapa duniani lakini haina maana kuwa haipo au haitangazwi kama ipo.

Tumia hata common sense katika fikra zako.

Pitia hii thread kuhusu tamko la serikali mwezi Oktoba 2017;

LINK>>>Vichwa 15 vya Treni Kununuliwa na Serikali
Acha uzuzu, mtu mzima unapodondosha nguo mbele za watu huna budi kuchutama sasa hapa serikali imedondosha nguo dawa siyo kutetea dawa ni kukaa kimya
 
Utaratibu wa manunuzi ni upi?

Weka hapa huo utaratibu ili tuone jinsi ambavyo umekiukwa kwa sababu kuna uwezekano umekalili tu neno ''utaratibu wa manunuzi''.
1.Kutangazwa kwa tenda
2.Kushindanisha walioomba kandarasi
3.Kufanya assessment ya aliyeshinda.
4.Kusainia mkataba na aloshinda
5.Kuweka oda kulingana na specifications
6.Kufanya malipo ya awali.
7.Kupokea mzigo/bidhaa
8.Kuhakiki bidhaa kulingana na specifications
9.Kupokea bidhaa husika.
Lakini pia Procurement Act ya 2009 ina miongozo mizur sana japo JPM anasema ina udhaifu.
 
Back
Top Bottom