Maajabu: Kichwa cha treni kilichookotwa bandarini ndio kimepata ajali Kigoma. Hivi kumbe walishanunua kimya kimya?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Maajabu ya serikali hii na maigizo hayaishi. Vile vichwa vya treni tulivyoambiwa vimeokotwa bandarini na havina mwenyewe ni kichwa kimoja wapo kilichopata ajali kigoma na kuanguka.

Kumbe mwenyewe alishapatika na kashanunua kimya kimya na mambo yanaendelea kama kawaida

FB_IMG_1520010308580.jpg
FB_IMG_1520010316637.jpg


Vile vichwa vya treni tulivyopigwa fix kwamba vimeokotwa bandarini na havina mwenyewe, kimoja kimepiga mzinga huko Kigoma.
_
"Uongo hufika haraka kwa sababu hupanda lift. Ukweli huchelewa kwa sababu hupanda ngazi, lakini mwisho ukweli hudhihirika na uongo hupotea kwa aibu" Zitto Kabwe.
_
"Unaweza kuwadanganya watu fulani kwa muda wote, au kuwadanganya watu wote kwa muda fulani, lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda wote" Tundu Lissu.
_
"Ukiwa muongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri" English proverb.
_
"Njia ya mwongo ni fupi" Swahili proverb
_
"Ukijaribu kufanya jambo la kipuuzi/aibu na likashindwa kufanikiwa, futa ushahidi wote unaoonesha kuwa uliwahi kujaribu kufanya jambo hilo" Adolph Hittler.

Bahati mbaya hii principle ya Hittler imemshinda "mzee wa Fix". Alifanya jambo la aibu (kutudanganya kaokota vichwa vya treni) halafu akasahau kufuta ushahidi. Hivi hata hizo namba walishindwa kubadilisha? Ama kweli mwisho wa ubaya ni aibu. Shame!!

Habari zaidi, soma=>TPA na TRC wakanusha juu ya kuondolewa na kutumika kwa vichwa vya treni kimya kimya
 
Kichwa cha treni kilichoanguka Mkoani Kigoma ni kimojawapo kati ya viwili vilivyopokelewa tarehe 21/03/2015 na TRL ambapo inadaiwa waliagiza vichwa 13 kwa bilioni 70.5 na kulipia fedha yote kutoka kampuni ya Electro-Motive Diesel (EMD) ya Marekani na vikatengenezwa na kampuni ya DCD ya Kichwa cha treni kilichoanguka Mkoani Kigoma ni kimojawapo kati ya viwili vilivyopokelewa tarehe 21/03/2015 na TRL ambapo inadaiwa waliagiza vichwa 13 kwa bilioni 70.5 na kulipia fedha yote kutoka kampuni ya Electro-Motive Diesel (EMD) ya Marekani na vikatengenezwa na kampuni ya DCD ya huko Afrika Kusini.

TRL ilikataa kuvipokea kwasababu ni vibovu na havina ubora kama walivyokubaliana kuvitengeneza na Electro-Motive Diesel (EMD) ikavitelekeza bandarini maana pesa walikwishalipwa, kwa hofu ya kupata hasara ya kuvirudisha kuviboresha.

Inadaiwa kuwa vichwa hivyo ni vikuukuu vilivyotoka kwenye karakanya Morogoro kwenda India kutengenezwa na kurudishwa nchini ambapo viwili vilipokelewa na 11 kutelekezwa baada ya kubainika ni vibovu na hatimaye kubainika bandarini kuwa havina mwenyewe.

Serikali sasa imethibitisha kuvinunua tena vichwa hivyo kwa dola milioni 26.4 kutoka kampuni hiyo ya EMD
 
Acha uongo! Hizi habari za kutunga ni kwa manufaa ya nani?
Kichwa hata kitoke mbinguni, kama reli ni mbovu yenye umri zaidi ya miaka mia, kitaanguka tu.
Vichwa ambavyo vinafanyiwa remanufacturing ni vile vikuu kuu vyenye umri wa zaidi ya miaka arobaini wala hata sio hivi vichwa vipya!
 
Kutokujua wewe kama walishanunua haina maana kuwa hawajasema kama walinunua.

Kuna mtu anaweza asijue kuwa kuna Dar es Salaam lakini haina maana kuwa haipo au haitangazwi kama ipo.

Tumia hata common sense katika fikra zako.
Acha upoyoyo ivi ivyo vichwa mwenyekiti wako alisena ni vya nani? Unapokamata kitu cha wizi au ukiokota then unakinunua?
 
Back
Top Bottom