Maajabu! Jiji la Mombasa halina stand ya bus

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450
Habari zenu wana Jf

kwa siku kadhaa nimekuwa nikisoma uzi kadhaa kuhusu miji ya Afrika mashariki hapa JF.

mji wa Mombasa ni mmoja wa miji yenye kusifiwa sana kwa mambo mazuri,
nilibahatika kufika pale wiki kadhaa nyuma lakini ajabu niliyoona mji ule hauna hata Stand ya Bus.

yaani kila kampuni inapakilia abiria ofisini kwake.

nikamuuliza mwenyeji wangu kulikoni? kaniambia mabepari walishauza kila kitu hata viwanja vya wazi hakuna,nikashangaa kuona hata daladala (Matatu) zao hazina stand zinapakia kokote tu.

ukweli mpangilio wa mji ule uko hovyo kabisa kwa mjini pale labda pembeni ambako sijatembelea.

Kitu kimoja tu nilipenda mji ule pale kivuko cha LIKONI pale wana ferry kama 3 au 4 zinapishana na watu wanapanda bure tu ila magari na vyombo vingine ndio wanalipa.Kwa hilo hongereni sisi hapa tuliambiwa kama hatuna pesa tupige mbizi tu.

Kingine barabara ya kutoka horohoro kwenda MSA ni mbovu hovyo kabisa na nyembamba mno.

Na nilichoona kingine Kenya maendeleo yao mengi ni ya mkoloni tu lakini toka wapate uhuru sidhani kama kuna la maana wamefanya.

Kingine maisha ni magumu sana sana nchi ile jamaa wana dhiki vibaya sana,najiuliza wao kuwa vinara wa Afrika Mashariki kwa uchumi imara lakini uchumi wao hauna faida wala msaada kwa raia wa kawaida, ni hayo tu kwa leo.
 
Habari zenu wana Jf

kwa siku kadhaa nimekuwa nikisoma uzi kadhaa kuhusu miji ya Afrika mashariki hapa JF
mji wa Mombasa ni mmoja wa miji yenye kusifiwa sana kwa mambo mazuri,
nilibahatika kufika pale wiki kadhaa nyuma lakini ajabu niliyoona mji ule hauna hata Stand ya Bus ,
yaani kila kampuni inapakilia abiria ofisini kwake,
nikamuuliza mwenyeji wangu kulikoni? kaniambia mabepari walishauza kila kitu hata viwanja vya wazi hakuna,nikashangaa kuona hata daladala (Matatu) zao hazina stand zinapakia kokote tu,
ukweli mpangilio wa mji ule uko hovyo kabisa kwa mjini pale labda pembeni ambako sijatembelea,

kitu kimoja tu nilipenda mji ule pale kivuko cha LIKONI pale wana ferry kama 3 au 4 zinapishana na watu wanapanda bure tu ila magari na vyombo vingine ndio wanalipa
kwa hilo hongereni sisi hapa tuliambiwa kama hatuna pesa tupige mbizi tu

Kingine barabara ya kutoka horohoro kwenda MSA ni mbovu hovyo kabisa na nyembamba mno,
na nilichoona kingine Kenya maendeleo yao mengi ni ya mkoloni tu lakini toka wapate uhuru sidhani kama kuna la maana wamefanya,
kingine maisha ni magumu sana sana nchi ile jamaa wana dhiki vibaya san,najiuliza wao kuwa vinara wa afrika mashariki kwa uchumi imara lakini uchumi wao hauna faida wala msaada kwa raia wa kawaida, ni hayo tu kwa leo


Siyo Mombasa tu hata Nairobi hakuna stendi kuu ya mabasi kila basi lina stendi yake hivyo ni juu yako kuzunguka mji mzima kutafuta!
 
Siyo Mombasa tu hata Nairobi hakuna stendi kuu ya mabasi kila basi lina stendi yake hivyo ni juu yako kuzunguka mji mzima kutafuta!
Ni kweli kabisa. Inashangaza sana Jiji kama Nairobi linakosa stendi ya mabasi.
 
Hii ni kweli kabisa, bus stand kwa mombasa na nairobi ni kero tupu...

Matatu na gari kubwa zinajiegesha tu sehemu fulani but siyo kusema stand kama zilizopo huku kwetu.
 
Hii ni kweli kanisa, bus stand kwa mombasa na nairobi ni kero tupu...

Matatu na gari kubwa zinajiegesha tu sehemu fulani but siyo kusema stand kama zilizopo huku kwetu.
Wenye vituo vya mafuta ndio wanapata tabu sana maana sehem zao Ndio matatu zinapakilia abiria, pembezoni hapo wafanyabiashara wamejaa yaani ikitokea ajali yyte mfano ya moto madhara makubwa sana
 
Siyo Mombasa tu hata Nairobi hakuna stendi kuu ya mabasi kila basi lina stendi yake hivyo ni juu yako kuzunguka mji mzima kutafuta!
Unafahamu mahali kwa jina country bus station? fahamu kampuni nyingi za mabasi zimekuwa na stendi Zao purely for customer convenience. Mfano enzi za kituo cha Abood bus hapo msimbazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom