Maajabu hayaishi Tanzania. Kijana amemaliza chuo hana ajira lakini anaishabikia CCM

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,646
35,979
Kuna classmates wangu kadhaa nawaona mitandaoni hasa Facebook wakiwa ndani ya nguo za CCM. Kwakuwa Mimi ni Mwajiriwa wa Serikali hii basi wanajua mimi ni mwana CCM pia. Nikiwahoji wanafanya kazi gani wanabaki kulia njaa tu na kunipiga mizinga au connection.

Serikali si lazima ikuajiri lakini inapaswa kutengeneza mazingira ya vijana kuajiriwa tena si kama vibarua bali ajira rasmi. Ajira ni haki ya kijana yeyote ndio maana watoto wa viongozi karibu wote ni waajiriwa.

Sasa vijana hawa jobless sijui wamerogwa na nani, hawana kazi guarantee lakini wanakisifia chama kilichoua ndoto zao. Biashara au kilimo vinafana ukiwa na kazi au mtaji mnono.
 
Ajira ni tatizo la dunia nzima wala usijidanganye kuwa CHADEMA wakibahatika kuchukua nchi watamaliza tatizo la ajira Tanzania.

Pia wapinzani mmekua mkilia kuwa katiba inakandamizwa wakati huo huo unasahau kuwa katiba imetoa uhuru kwa mwananchi yeyote kuchagua kuwa mwanachama wa chama chochote kadri itakavyompendeza.
 
Kuna classmates wangu kadhaa nawaona mitandaoni hasa Facebook wakiwa ndani ya nguo za CCM. Kwakuwa Mimi ni mwajiriwa wa serikali hii basi wanajua mimi ni mwana CCM pia...

Watakuwa wanachekechea teuzi au fursa (lose balls) fulani fulani zinazoweza kupatikana.

Wenyewe huita mvumilivu hula mbivu.

Ndiyo kina shilinde, hapi, makondakta, katambi na wa namna hiyo.

Hawana ujasiri wa kupigana zaidi ya kusubiria kubebwa.
 
Mkuu wewe hushangai chama kinachojiita kikuu cha upinzani pamoja na kupokea ruzuku kila mwezi bado ni wapangaji kwa miaka 20 na wanataka kuongoza nchi.

Sasa kama chenyewe hakijiwezi kwa kujenga hata banda la mbao, ndio kitamletea maendeleo nani, no wonder wanakataa maendeleo anayofanya Rais.
 
Unawashangaa vijana wa Tz Nenda Zimbabwe raia wa nchi ile sijui ZANUPF imewapa Nini ni zaidi ya mapoyoyo wana njaa bado wanashabikia ZANUPF
 
Itafika time tutaanza kuambiwa kuwapenda wake zetu ni upoyoyo,
Time will tell.
 
Hizo nchi za dunia ya Kwanza yenyewe wamelishindwa tatzo la ajira,sembuse TZ.

Nigeria inaongoza chama pinzani lakini hakuna lililobadilika.
Nyinyi viongozi mnaowataka wanatoka dunia mpya?

Si bure ndo mana watu wanawapinga na kuwaona wasanii tu.
 
Ajira ni tatizo la dunia nzima wala usijidanganye kuwa Chadema wakibahatika kuchukua nchi watamaliza tatizo la ajira Tanzania.

Pia wapinzani mmekua mkilia kuwa katiba inakandamizwa wakati huo huo unasahau kuwa katiba imetoa uhuru kwa mwananchi yeyote kuchagua kuwa mwanachama wa chama chochote kadri itakavyompendeza.
Ni kweli ajira ni tatizo la dunia mzima lakini ni taifa la kipumbavu peke yake ndiyo litaacha waalimu na madaktari mtaani wakati shule na hospitali hazina wanataaluma husika lakini hapo hapo taifa linapoteza millions of dollars kuwekeza kwenye crazy projects kama ndege huku likijigamba linanunua ndege kwa cash!

Kwa miaka nenda rudi nchi ina uhaba mkubwa wa Walimu wa Sayansi! Baada ya kila njia kushindikana, ikawa introduced 3 years Special Diploma (Science & Maths) ili kukabiliana na uhaba huo!

Magu kaingia, kaifuta ile special diploma; watu tukawa tunasubiria alternative plan, miaka 5 inakata sasa no plan!!!

Hakuna taifa duniani linaweza kufanya ujinga kama huo unless liwe na leadership kama ya Magufuli na ndio maana hadi kesho hawajaona umuhimu wa ku-cover hizo kada muhimu kwa ustawi wa jamii!
 
Ni kweli ajira ni tatizo la dunia mzima lakini ni taifa la kipumbavu peke yake ndiyo litaacha waalimu na madaktari mtaani wakati shule na hospitali hazina wanataaluma husika lakini hapo hapo taifa linapoteza millions of dollars kuwekeza kwenye crazy projects kama ndege huku likijigamba linanunua ndege kwa cash...
Kuhusu kada ya madaktari na walimu nenda kafanye research ya kutosha ndo uje tujadiliane. Nakuahidi saa sita mchana nitakuja na data za kutosha.

Najiandaa kwenda kwenye ujenzi wa taifa siwezi kuweka kila kitu kwa muda huu.
 
Back
Top Bottom