Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,650
- 218,105
Utaratibu wa miaka yote mgombea mwenyewe au wapambe wake ndio wenye jukumu la kutafuta wadhamini wa Mgombea wao , si viongozi wa Makao Makuu, hii ni kwa sababu viongozi hao hawatakiwi kubagua wanachama , maana wagombea wanaweza kuwa zaidi ya mmoja , ndio maana wagombea wote wa urais wa CCM 2015 akiwemo mkulima kapuku wa Kigoma waliwajibika wenyewe kutafuta wadhamini , lakini Rodrick Mpogolo ambaye ni kiongozi wa Makao Makuu anahangaika kumtafutia wadhamini Mgombea aliyeomba mwenyewe kugombea urais .
Sasa swali ni iwapo kutakuwa na wagombea wengine kama inavyotarajiwa na wanaccm , viongozi wa Makao Makuu watajigawa namna gani , kwanini wasiache wagombea wajitafutie wenyewe wadhamini?
Sasa swali ni iwapo kutakuwa na wagombea wengine kama inavyotarajiwa na wanaccm , viongozi wa Makao Makuu watajigawa namna gani , kwanini wasiache wagombea wajitafutie wenyewe wadhamini?