Maajabu: Daraja la Furahisha Mwanza lajengwa kwa Bil 4.7, kumbuka hostel za UDSM zilijengwa kwa bil 10

Hilo daraja watavushia ng'ombe.
Hata fisi zao zitavuka hapo wakati wa usiku. Kwani hukumsikia rais? Hivyo lazima washeherekee hako kadaraja katakaoepusha wao na mifugo yao kugongwa na magari ya mwendokasi eneo hilo.
 
Yaani huko upinzani hamfudishwi jinsi ya kushusha nondo.. oops nimesahau
Nyie wakurupukaji hata mada zilizoenda shule hamuwezi kuziandika.
Jibu hoja iliyopo mezani, daraja la furahisha ni zaidi ya 4bil, yakijengwa matatu yataishinda gharama Magufuli hostel. Shushan nondo kwanini Yale hela zaidi?
 
Yaani huko upinzani hamfudishwi jinsi ya kushusha nondo.. oops nimesahau
Nyie wakurupukaji hata mada zilizoenda shule hamuwezi kuziandika.
Ana hoja usimpuuze hebu ona huo uwiano hapo uone walakini uliopo
 
Ana hoja usimpuuze hebu ona huo uwiano hapo uone walakini uliopo

Achana na uwiano..jibu langu silibadili

Mtu akileta mada vizuri aiweke kwa kuchambua.. huyo ni upinzani lazima nimpe jotoooi

Mimi nawewe ndio twaweza jenga nyumba aina moja ila kuanzia misingi tukatofautiana kiasi tutakachotumia.
 
Maajabu hayataacha nchi hii salama na uwongo wa kiongozi mkubwa hapa nchini.

Hilo daraja la furahisha mkandarasi ni yuleyule TBA kalijenga kwa bil 4.7 ila zile hostel za uDSM walijenga kwa bil 10.

Tusaidiane na ukweli usemwe wanaompinga zito hawako timamu


View attachment 620702
Hili ndilo Daraja la furahisha lililipo jijini Mwanza.
View attachment 621163
Haya ni majengo 20 yenye ghorofa nne kila jengo na yana uwezo wa kuhudumia wanafunzi 4,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Acha uwongo. Daraja la Furahisha mjenzi/mkandarasi Ni Nyanza Roadworks Limited chini ya usimamizi wa TanRoads
 
Barabara pamoja na daraja bei ni BILLION hizo ulizotaja na sio daraja pekee.....

ila ngoja tukukubalie maana "upotoshaji" ndio silaha pekee mliyobaki nayo

NGOSHA ENDELEA KUYABANA HAYA MANYUMBU
 
Barabara pamoja na daraja bei ni BILLION hizo ulizotaja na sio daraja pekee.....

ila ngoja tukukubalie maana "upotoshaji" ndio silaha pekee mliyobaki nayo

NGOSHA ENDELEA KUYABANA HAYA MANYUMBU
Jinga kabisa

Rais DK. JOHN MAGUFULI leo amefungua daraja la juu la watembea kwa miguu la Furahisha Mjini Mwanza lililojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.747, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

Rais MAGUFULI amefungua daraja hilo muda mfupi baada ya kuwasili Mjini Mwanza ambako leo ameanza ziara ya kikazi ya siku 2.

Daraja hilo ambalo limetajwa kuwa alama ya utambulisho wa Jiji la Mwanza lina urefu wa meta 46, upana wa meta 3.6, kimo cha meta 5.8 na njia za kuingia na kutoka zenye jumla ya meta 700.

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi PATRICK MFUGALE amemueleza Rais kuwa kazi ya usimamizi wa ujenzi wa daraja hilo imefanywa na TANROADS yenyewe, ujenzi umefanywa na kampuni ya Kitanzania ya Nyanza Roads Works Ltd na daraja limekamilika kwa ubora unaotakiwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano PROF. MAKAME MBARAWA MNYAA amesema pamoja na kujengwa kwa Daraja hilo Serikali inaendelea kujenga madaraja mbalimbali nchini ili kuimarisha miundombinu yakiwemo madaraja.

Kwa upande wao wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu PROF. NORMAN SIGALLA KING na ZUBERI MOHAMED KUCHAUKA wamempongeza Rais MAGUFULI kwa juhudi kubwa anazofanya kuharakisha maendeleo nchini ikiwemo kujenga miundombinu na wametoa wito kwa Watanzania wote kumuunga mkono.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Daraja hilo Rais MAGUFULI amesema aliamua kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya Sherehe za Muungano za mwaka 2016 baada ya kuguswa na vifo vilivyosababishwa na ajali za watembea kwa miguu, kugongwa na magari wakati wakivuka barabara katika eneo la Furahisha.

Rais MAGUFULI pia amezungumzia juhudi nyingine za kuendeleza Jiji la Mwanza kuwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa barabara ya njia nne ya kutoka uwanja wa ndege hadi Mwanza Mjini na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ili kuuwezesha uwanja huo kuwa wa kimataifa, utakaokuwa kituo cha kuingia na kutoka Afrika Mashariki kwa kampuni kubwa za ndege kutua.

Rais MAGUFULI anaendelea na ziara yake hapa Mwanza na baadaye leo atafungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona.
 
Back
Top Bottom