Maajabu: CHADEMA Ndio Kama Chama Tawala na CCM Ndio Wapinzani Sasa

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
147
Ndugu wa JF,
Nimekuwa nikifatilia kwa makini hali ya kisiasa nchini mwetu;
Kwa kweli kwa hali halisi sasa imekuwa kana kwamba CHADEMA ndio chama tawala na CCM ndio wapinzani. Haya ni maajabu! Wimbo mkuu umekuwa CHADEMA. Nguvu ambayo CCM inatumia kushambulia CDM ni nguvu ambayo ingeweza kuleta mabadiliko makubwa kama ingeelekezwa eneo jingine lenye manufaa kwa wananchi.

USHAURI WANGU KWA CHAMA TAWALA - CCM: Jamani tusipoteze muda mwingi kuzungumzia CDM. Kadri tunavyowashambulia ndivyo ambavyo wananchi wengi wanaendelea kujiuliza, kulikoni?? Kwa mfano; inaleta maswali mengi sana kwa sisi raia kuona viongozi wetu wa CCM wanaonyesha masikitiko makubwa sana kuhusu maamuzi ya CDM ya kuwasimamisha baadhi ya viongozi wao.

Dawa ya CHADEMA ni kwa CCM kujitahidi kutimiza ahadi zake kwa wananchi; sio kuishambulia CHADEMA.

Asanteni.
 
Hata ivyo wao wapinzani tu! Tuliamua kupotezea tu 2010 jk asiaibike kutawala term moja. Tuendelee kuwaadaa kisaikolojia 2015 waachie dola kwahiari yao.
 
CCM hawawezi kufanya maendeleo bila kuwepo na upinzani imara.
 
CHADEMA ni chama cha kilaghai. lazima tukijadili kwa sana kwa vile kuna watanzania wengi wamelaghaiwa
 
Hata ivyo wao wapinzani tu! Tuliamua kupotezea tu 2010 jk asiaibike kutawala term moja. Tuendelee kuwaadaa kisaikolojia 2015 waachie dola kwahiari yao.

CHADEMA mbele ya Kinana hawana chao. yaani kaisambaratisha kwa muda mfupi sana
 
Kuota Chadema itachukua nchi ni sawa na yule jamaa alieota amegeuzwa kuku halafu akaanza kutaga mayai, alipoamka asubuhi akakuta kitanda kimejaa mwaikimbas...
 
Dawa ya CHADEMA ni kwa CCM kujitahidi kutimiza ahadi zake kwa wananchi; sio kuishambulia CHADEMA.

Asanteni.

Habari za Ulaya,siasa za kibongo hizi unazijua....huo ushauri unawapa chama gani maana ukiwa huku huwezi eleweka vyema.
 
Kuota Cahdema itachukua nchi ni sawa na kuota umegeuzwa kuwa kuku halafu unataga mayai, ukiamka usingizini????

Utakuwa umeota ndoto ya namna siku moja! ila changamsha akili yako na uone namna ambavyo ccm wamekuwa wana deal na chadema kuanzia kwenye ugaidi, udini ba ukabila.

haya yote wananchi wameshajua! pole nasikia jana ulibeep kuwa unataka kurudi chadema! attention sikaaziiii
 
Ndugu wa JF,
Nimekuwa nikifatilia kwa makini hali ya kisiasa nchini mwetu;
Kwa kweli kwa hali halisi sasa imekuwa kana kwamba CHADEMA ndio chama tawala na CCM ndio wapinzani. Haya ni maajabu! Wimbo mkuu umekuwa CHADEMA. Nguvu ambayo CCM inatumia kushambulia CDM ni nguvu ambayo ingeweza kuleta mabadiliko makubwa kama ingeelekezwa eneo jingine lenye manufaa kwa wananchi.

USHAURI WANGU KWA CHAMA TAWALA - CCM: Jamani tusipoteze muda mwingi kuzungumzia CDM. Kadri tunavyowashambulia ndivyo ambavyo wananchi wengi wanaendelea kujiuliza, kulikoni?? Kwa mfano; inaleta maswali mengi sana kwa sisi raia kuona viongozi wetu wa CCM wanaonyesha masikitiko makubwa sana kuhusu maamuzi ya CDM ya kuwasimamisha baadhi ya viongozi wao.

Dawa ya CHADEMA ni kwa CCM kujitahidi kutimiza ahadi zake kwa wananchi; sio kuishambulia CHADEMA.

Asanteni.

Acha uongo mkuu wanaokitaja chadema wengi wao ni wanachadema wenyewe wala siyo CCM. Wengi wanaendelea kuzungumzia swala la Zitto na kamati kuu inayoongozwa na akina Slaa, Mbowe, Lissu na wengineo, ukitizama kwa makini kuna pande mbili moja ni Pro- Zitto na lingine ni Pro-Slaa na wenzake hakuna zaidi.. CCM tunawaona wakikata mbuga wakiongea na wananchi mikoa mbalimbali wakati chadema poroja zimekuwa nyingi wakiwa wanabishana kuhusu swala la zitto
 
CHADEMA mbele ya Kinana hawana chao. yaani kaisambaratisha kwa muda mfupi sana

badala msambaratishe umaskini, maradhi na ujinga wa kutupwa wa Watanzania nyie mnawaza kusambaratisha CHADEMA.

kweli CCM=Chama Cha Mafisi.

CHADEMA ni Mpango wa Mungu. hasambaratikiki!
 
Kuota Chadema itachukua nchi ni sawa na yule jamaa alieota amegeuzwa kuku halafu akaanza kutaga mayai, alipoamka asubuhi akakuta kitanda kimejaa mwaikimbas...

We dogo wewe...!!
Pesa za rambi-rambi za Mwangosi umepeleka wapi wewe...??
 
Acha uongo mkuu wanaokitaja chadema wengi wao ni wanachadema wenyewe wala siyo CCM. Wengi wanaendelea kuzungumzia swala la Zitto na kamati kuu inayoongozwa na akina Slaa, Mbowe, Lissu na wengineo, ukitizama kwa makini kuna pande mbili moja ni Pro- Zitto na lingine ni Pro-Slaa na wenzake hakuna zaidi.. CCM tunawaona wakikata mbuga wakiongea na wananchi mikoa mbalimbali wakati chadema poroja zimekuwa nyingi wakiwa wanabishana kuhusu swala la zitto

Zitto...??

jitetetea-kabla-sijakuvua-bukta.jpg
 
Hata mimi uwa najiuliza,hivi CHADEMA imekuwa tishio kiasi hicho?siku hizi uwezi kusikia vyama vingine vyovyote vinatajwa sio cha CUF,NCCR.CHAWEPO na vinginevyo vingi,sasa hivi vyote ni kama vimekuwa extinct,league imebaki kwa CCM na CHADEMA,hii inadhiihrisha jinsi CHADEMA ilivokuwa tishio kwa siku za karibuni,fanya research kwenye mitandao,magazeti na radio utagunduamkuwa vyama vingine siku hizi havitajwi kabisa wala kuandikwa.ni CCM na CHADEMA basi,tusubiri 2015 NGOMA INOGILE.
 
Kuota Chadema itachukua nchi ni sawa na yule jamaa alieota amegeuzwa kuku halafu akaanza kutaga mayai, alipoamka asubuhi akakuta kitanda kimejaa mwaikimbas...

Lukosi, haya majibu huwa unatoa wapi??? Nimecheka hadi basi!! haya ndugu yangu; ila inabidi tukazane na ilani ya chama, not CDM.
 
Back
Top Bottom