Bonson
Senior Member
- Apr 20, 2013
- 183
- 147
Ndugu wa JF,
Nimekuwa nikifatilia kwa makini hali ya kisiasa nchini mwetu;
Kwa kweli kwa hali halisi sasa imekuwa kana kwamba CHADEMA ndio chama tawala na CCM ndio wapinzani. Haya ni maajabu! Wimbo mkuu umekuwa CHADEMA. Nguvu ambayo CCM inatumia kushambulia CDM ni nguvu ambayo ingeweza kuleta mabadiliko makubwa kama ingeelekezwa eneo jingine lenye manufaa kwa wananchi.
USHAURI WANGU KWA CHAMA TAWALA - CCM: Jamani tusipoteze muda mwingi kuzungumzia CDM. Kadri tunavyowashambulia ndivyo ambavyo wananchi wengi wanaendelea kujiuliza, kulikoni?? Kwa mfano; inaleta maswali mengi sana kwa sisi raia kuona viongozi wetu wa CCM wanaonyesha masikitiko makubwa sana kuhusu maamuzi ya CDM ya kuwasimamisha baadhi ya viongozi wao.
Dawa ya CHADEMA ni kwa CCM kujitahidi kutimiza ahadi zake kwa wananchi; sio kuishambulia CHADEMA.
Asanteni.