Maajabu: Baba wa watoto 151 na wake 16 aapa kuendelea kuoa hadi kifo

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
1,655
2,000
Misheck Nyandoro, muumini wa Kanisa la Johanne Marange Apostolic ambaye ni baba wa watoto 151 kutoka kwa wake 16 amesema hatakoma kuzaa.

Marange.jpg

Nyandoro kutoka Mbire, eneo la Kati mwa Mashonaland nchini Zimbabwe, alisema ana mpango wa kuoa mke wa 17 ili amzalie watoto wengine zaidi, Gazeti la The Herald limeripoti.

Kulingana na mzee huyo, ndoa ya mitala ni mradi ambao aliuanzisha mwaka 1983 na ataendela nao hadi kifo.

"Yangu ni mradi. Huu mradi wa ndoa ya mitala niliuanzisha tangu mwaka 1983 na nitaumaliza na kifo changu. Wakati nitafariki ndio nitakoma kuoa na kuzaa watoto.

“Ninapanga kuoa mke wangu wa 17 msimu huu wa baridi na tayari mipango inashughulikiwa,"alisema Nyandoro.

Kulingana na mzee huyo mwenye umri wa miaka 66, mradi huo unazaa matunda kwani hupokea pesa na zawadi kochokocho kutoka kwa watoto wake na wakwe.

“Kutokea kwa watoto wangu wanaofanya kazi na kuzawadiwa pesa kupitia EcoCash, karibu kila siku, watoto wangu 11 wameniweka kwenye sera ya mazishi. Ninapata zawadi kutoka kwa wakaza wanangu."

“Sijakoma kuzaa wala kuoa. Mungu akiniruhusu, nitaoa hadi wake 100 na huenda kuzaa watoto 1000. Ulaya una mpango wa kupunguza idadi ya watu Afrika na ninapinga.Mimi ni mpiganaji wa kitambo na serikali inashuhulikia katro ya watoto wangu. Hkauna shida,"aliongeza.

Nyandoro alifichua kuwa kazi yake ni kuketi kwenye kivuli na kusubiri chakula kutoka kwa wake zake 16 ambapo kila mke hupika na yeye huchagua tu chakula kitamu na kutupa kilichopikwa vibaya akidai ni sheria katika boma hilo.

Mzee huyo alijigamba namna ana uwezo wa kuwaridhisha wake zake chumbani ambapo ana ratiba ya kumtembelea kila mke kuwapa haki zao za ndoa.

Alidai kuwa hatumii dawa zozote za kusisimua mapenzi akisisitiza kwamba ana nguvu sawa na kijana wa miaka 18.

Nyandoro pia alisema alioa wake zake kulingana na sheria za kanisa lake na hajawahi kumuoa mwanamke ambaye aliwahi kuolewa ama mwenye umri mdogo.Yeye ndiye huwatongoza warembo ambao anataka kuwaoa bila kuchaguliwa.
 

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,376
2,000
Cha muhimu awe na uchumi imara tu
Hapo ndio vijana mnafeli na mnachelewa kuzaa mapema
Sasa kuzaa na uchumi imara ni vitu viwiri
Ipo hivi kila mja amejariwa uwezo muenekona na tabia yaje
Hvyo ili kupata ndoa bora yenye kutotoa watoto wengi
Hata km una uchumi mbovu wewe
Tafuta mwenzako wa kufanana na wewe tabia na umzidi muonekano na uchumi hakika utaenjoy hata kama unauza genge tafuta wa level zako utafurahia sana ndoa na utaenjoy maisha
Ukisubiri mpk upate pesa nyingi upate warembo utapata watoto uzeeni
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
10,594
2,000
Hapo ndio vijana mnafeli na mnachelewa kuzaa mapema
Sasa kuzaa na uchumi imara ni vitu viwiri
Ipo hivi kila mja amejariwa uwezo muenekona na tabia yaje
Hvyo ili kupata ndoa bora yenye kutotoa watoto wengi
Hata km una uchumi mbovu wewe
Tafuta mwenzako wa kufanana na wewe tabia na umzidi muonekano na uchumi hakika utaenjoy hata kama unauza genge tafuta wa level zako utafurahia sana ndoa na utaenjoy maisha
Ukisubiri mpk upate pesa nyingi upate warembo utapata watoto uzeeni
Unahitaji pole nyingi sana kama ndio mawazo yako haya!

Kuleta watoto duniani kuende sambamba na uchumi wa kutosha kuwapa mahitaji yao yote.
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
16,434
2,000
Alidai kuwa hatumii dawa zozote za kusisimua mapenzi akisisitiza kwamba ana nguvu sawa na kijana wa miaka 18.
Anatakiwa kuwa specific, kijana wa miaka 18 wa nchi gani? Wapo vijana wa age hiyo katika baadhi ya majiji wanakula chips mayai, je atalingana nao?
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
22,677
2,000
Hayo mengine siyo makanisa ni kama kijiwe cha kahawa chenye msimamizi
 

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,376
2,000
Unahitaji pole nyingi sana kama ndio mawazo yako haya!

Kuleta watoto duniani kuende sambamba na uchumi wa kutosha kuwapa mahitaji yao yote.
Wewe hujui raha ya kuizungurukia mibunye minne tofauti tofauti kwa kwa siku
Mmoja raha vile sasa mibunye 16 hiyo mwanawane ebu fikilia siku 1 unasema sufanyi kazi naizungurukia mibunye tuu
Sisi tumeruhusiwa mibunye minne

Sasa mibunye 16 hiyo siyo masihara jamaa anapataa raha aisee

Wewe kaa na uzungu wako wakati sisi tunawekeza mtaji wa watoto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom