Maajabu: Aonekana baada ya kufa na kuzikwa miezi mitatu iliyopita

kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
6,299
6,321
Salam wadau humu,

Daaa jumamosi iliyopita nilistaajabu sana huku. Yaani kuna Dada alifariki mwezi Wa saba tukahudhuria msiba,nikaaga ule mwili kwa kuuona kwa macho yangu halafu juzi akaonekana huku akiwa hai ila aliyevurugika Akili. Yaani kijiji kizima watu walikuwa kama wapo msibani mana kila kona habari zilikuwa ni huyo Dada na hadi sasa huku habari ni hizohizo na watu wanaendelea kumiminika nyumbani kwao na huyo Dada ili kumuona utadhani ni kipindi kile kule Loliondo. Niliwaza sana.

Kabla ya kifo chake huyo Dada alikuwa na magunia ya mpunga kama 80 hivi, na ng'ombe kadhaa, kajumba kake na kiwanja pamoja na cherehani vitu ambavyo vyote viliuzwa na ndugu Mara tu baada ya kifo chake. Na aliporudi hyo juzi vitu pekee alivyoweza kuwauliza watu wakamuelewa ni hayo magunia yake ya mpunga, ng'ombe na cherehani yake.

Sura ya huyo Dada tangu arudi imekuwa ikibadilika badilika, Mara awe mweusi Mara awe maji ya kunde. Na haongei tena kiluga anaongea kiswahili kilichonyooka. Polisi walikuja wakamcheki wakawauliza ndugu waliodai huyo kiumbe ndiye ndugu yao alozikwa mwezi Wa saba. Ndugu hao walidai sura ya ndugu yao imebadilika kwa kiasi Fulani ila alama zote za mwilini zilifanya waamini yule ni ndugu yao. Baada ya hapo polisi walimuhojihoji huyo Dada japo hawakupata ushirikiano vema mana dishi lilionekana kuyumba kisha wakaondoka na kuwaachia ndugu huyo ndugu yao

Wataalamu Wa haya mambo kama wapo humu watufafanulie vizuri mazingira ya namna hii huwa ni nini hasa na inawezekanaje?

Jambo hili limetokea Wilaya ya Kwimba ktk kijiji cha Sanga.
 
Maisha magumu ni kweli hatukatai, ila acha kutafuta hela kwa njia za mkato. Kama marehemu alifariki na kuzikwa full stop. Nothing new.
 
Hapo tu ndiyo tunawazidi watu weupe,.Big up kwa Wanga wote na wachawi,.Sema sasa hao ndugu mbona wamefanya fasta kuuza mali za marehemu?
Asee zingine zilianza kutumika siku ya msiba wake. Na Kiwanja chake kikauzwa fasta na mtu keshajenga. Sasa sijui Akili zitamrudia!!?
 
Alivyorudi siku nyumbani alikuwa amevaa nguo alizozikwa nazo au alikuwa ameulambia nguo zingine?
Alivaa zingine. Anadai hata msibani alikuwepo kwa kipindi kifupi na alikuwa anawaona watu wanavyolia yeye alikaa pembeni kabla hajaondoka. Inaonyesha ana kama majini hivi kichwani kwake mana kuna wakati anaongea vitu straight na kuna kipindi haeleweki
 
Back
Top Bottom