Maajabu 20 ya tunda la stafeli katika tiba

saidi bunduki

Member
Mar 10, 2018
24
23
Kwa jina jingine hujulikana kama (Tope tope) Nadhani ni kwa sababu ya umbile lake hasa likiwa limeiva huwa laini mfano wa tope.

Huenda sura yake ikawa mbaya kwa muonekano, lakini ni tunda lenye faida nyingi sana ikiwemo uponyaji wa magonjwa mbali mbali.



Tunda lenyewe ni hili (stafeli)


NAMNA YA KUTUMIA STAFELI
Stafeli linaweza kuliwa katika aina tofauti. Kama unataka kupata faida zake zote, unaweza kulila lililoiva kama lilivyo au unaweza kutengeneza juisi yake. Unywaji wa maji yatokanayo na majani, mizizi au magamba yake, unaweza kunywa kama chai au kinywaji kingine cha kawaida.


FAIDA ZA TUNDA LA STAFELI (TOPE TOPE)
Stafeli lina virutubisho vingi, baadhi yake ni AMINO ACID, ACETOGENINC, VITAMIN C, IRON, PHOSPHORUS, CALCIUM, NIACIN, RIBOFLAVIN na vingine vingi.

1. HUSAIDIA KUTIBU SARATANI
Ingawa sio tiba ya moja kwa moja kwa saratani, lakini hakuna shaka kabisa kuwa lina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana au kupunguza makali ya saratani.

Ukweli uliogundulika hivi karibuni, umewapa wagonjwa wa saratani njia nyingine mbadala ambayo haikuwepo hapo awali. Kwani hivi sasa wanaweza kulitumia stafeli kama dawa ya kupunguza makali au kuwapa kinga dhidi ya saratani na wanaweza pia kuitumia pamoja na matibabu wanayopewa ya mionzi na kupata ahueni kubwa.

UCHUNGUZI WA WATAALAM

Zaidi ya majaribio 15 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli, yamebaini haya yafuatayo:

  • Stafeli huua chembechembe za saratani (cancerous cells) aina 12, ikiwemo saratani ya matiti, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo n.k.
  • Stafeli lina mchanganyiko wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mara 10,000 zaidi ya dawa ya ‘Adriamycin’ ambayo ndiyo hutumika kutibu aina mbalimbali ya saratani.
  • Mchanganyiko wa virutubisho vya ‘Annonaceous’ ‘Acetogenins’ vilivyomo kwenye stafeli huuwa seli zilizoathirika tu na saratani, tofauti na dawa za kisasa ambazo zenyewe huua seli zilizoathirika na hata zisizoathirika.
  • Stafeli hudhibiti ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo kwa dawa za kisasa, ambazo wakati mgonjwa anapozitumia, iwe zile za njia ya mionzi, sindano au vidonge, huwa zina athari mbaya kwa mtumiaji na wakati mwingine huweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.
2. HUSAIDIA MAUMIVU YA KIPANDA USO
Miongoni mwa virutubisho vilivyomo katika tunda hili ni pamoja na 'Riboflavin' husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda uso.

3. HUZUIA ANEMIA (Ugonjwa wa kukauka damu)
Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini.

4. HUTIBU MAGONJWA YA INI
Ukiachana na ladha tamu ya juisi ya stafeli lakini pia inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.


authentic-jamaican-soursop-juice-recipe-21827735.jpg
Juis ya Stafeli


5. KUIMARISHA MIFUPA
Stafeli ni chanzo kizuri pia cha madini ya kopa (copper) na kalshiamu (calcium), virutubisho ambavyo huwa muhimu kwa ukuaji wa mifupa mwilini.

Matatizo mengine yanayoweza kudhibitiwa na stafeli ni pamoja na kuumwa miguu, maumivu kwenye ‘joints’, mwili kukosa nguvu na matatizo mengine ya viungo.

FAIDA NYINGINE ZA STAFELI (Kwa ufupi)
• Hutumika kutibu maumivu ya nyuma ya mgongo ( low back pain )

• Mstafeli hutumika kutibu maumivu ya jongo/gout

• Hurekebisha usawa wa kiasi cha damu na sukari mwilini.

• Huongeza kinga ya mwilini

• Hudhibiti ukuaji wa bacteria, virusi, vijidudu nyemelezi na uvimbe.

• Huongeza stamina ya mwili na kurahisisha kupona haraka unapokuwa mgonjwa.

• Hutibu jipu na uvimbe.

• Hukimbiza chawa.

MAJANI, MIZIZI, MAGAMBA NAYO NI DAWA
Mbali ya tunda lenyewe kuwa na faida lukuki kama zilivyoanishwa hapo juu, vilivyomo vingine kwenye mti huo kama vile mizizi, majani, mbegu na magamba yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali:
  • Unywaji wa maji yaliyotengenezwa kutokana na majani ya mstafeli hutibu magonjwa ya ngozi, chunusi na uvimbe wa mwili.
  • Maji ya majani ya mstafeli pia hutibu ugonjwa wa kuhara, kukohoa, kuvimba miguu, mapunye kichwani. Aidha, maji ya majani ya mstafeli yamethibitika kushusha kiwango cha sukari mwilini.
  • Mbegu zake hutengenezwa dawa ya kula na kufukuza wadudu waharibifu.
  • Majani ya mti wa mstafeli hutumika kutibu maumivu ya mishipa. Saga majani yake mpaka yalainike kabisa, kasha paka taratibu eneo la mishipa lililo na maumivu mara mbili kwa siku.
  • Ni tiba ya asili ya maumivu ya mishipa, yasage majani yake mpaka yalainike kabisa kisha paka taratibu eneo la mshipa lililo na maumivu mara mbili kwa siku
  • Huongeza kinga ya mwili
  • Hutibu jipu na uvimbe

TAHADHARI
Inaelezwa kwamba stafeli linaweza kuwa siyo salama kwa wajawazito, wagonjwa wa presha ya kupanda au kushuka (hypotension or hypertension). Hivyo wanashauriwa kabla ya kula, wapate ushauri wa daktari kwanza.

Lakini pia stafeli kwa asili yake lina kiasi kingi cha virutubisho vinavyoua bakteria, hivyo ulaji wa muda mrefu wa tunda hili kunaweza kuua bakteria wote tumboni hata wale wazuri, hivyo iwapo utalila tunda hili kwa zaidi siku 30 mfululizo, unashauriwa pia kuongezea na dawa za kulainisha njia ya chakula.

Imeandaliwa na SAIDI BUNDUKI
 
Asante Mkuu. Kitu ingine nzuri kwa afya ni Almonds na Juice ya Limao
Juice ya limao inasemekana huathiri nguvu za kiume hasa inaponywewa kwa wingi.

Nilipitia documentary moja ilikuwa inaelezea juu ya matatizo ya nguvu za kiume.
 
mwenyewe nayapenda sana ila sina utalam wa wap yanaweza kustaw vzur mi nipo chato
Hiyo kanda yanastawi vizuri sana sema kupata miche yake na kulikuza ndiyo mtihani.

Nyumbani lilikuwepo mti mkubwa na jingine changa hilo changa lilikaa miaka mingi sana bila kukomaa.

Halafu hata kuyaotesha ni ngumu sana mbegu zake huchukua muda mrefu kuoza na kuota.
 
ila sasa kulipata ni gumu sana jaman na yanastawi sijuw upande gani mwa nchi

We upo wapi mbona yamejaa sana hata kwetu kuna mti kwa mama yangu tena miwili ikianza kuzaa mpaka kero na ni hapa hapa Dar
 
Mkuu saidi bunduki asante kwa ku-share nasi tiba hii. Ila nina swali naomba unisaidie.

Ni herbs gani nyingine ni nzuri kwa kutibu saratani?

Nimeuliza hivyo kwasababu kuna ndugu yangu ana saratani ya titi, na mwaka jana nilimwelekeza atumie majani hayo ya mstaferi, na kweli bwana, yalimsaidia sana sana (maumivu na uvimbe kwenye titi lake yalipungua kwa kasi kubwa).

Kikwazo kikaja hapa:ana pressure ya kushuka na kila alipotumia majani hayo hali yake kwenye mapigo ya moyo ikawa mushkeli. Sasa atumie herbs gani zisizo na side-effects kwa kwa hali yake ya cancer + pressure?
 
Habari za muda wadau,naomba mwenye ufahamu wa matumizi na maadalizi ya majani ya Mstafeli kwa ajili ya tiba na kinga dhidi ya maradhi mbalimbali ya binadamu. Nimesikia juu juu kuhusu tiba hii, na kwamba majani haya yana faida nyingi kwa matumizi ya binadamu KIAFYA.

Kwa kuwa JF ni kisiwa cha maarifa naamini nitapata taarifa nyingi na sahihi kwa matumizi yangu na watu wengine wenye uhitaji na shida za kiafya zinazohitaji matibabu ya tiba lishe na tiba mbadala.

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom