Maagizo ya ubomoaji nyumba toka kwa mh. Lukuvi yamepindishwa.

Rich Forever

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
467
469
Hilo agizo limepindishwa namsikiliza lukuvi muda huu kupitia magic fm kasema nyumba zinazobolewa ni zile zinazojengwa sasa ktk maeneo yasiyoruhusiwa na ambao wanakesi za uporaji wa viwanja waliojenga kibabe katolea mfano wa mbezi beach na tegeta kuna wanyonge wana hati zao lakini wenye fedha wamewapora wanyonge hao na kujenga nyumb atalala nao mbele waporaji ili wanyonge wapate haki yao sio kubomoa nyumba za zaman.

Pia kasema nyumba zaman zilizojengwa kiholela basi serikali itajitahid kuwatambua na kuwahurumia kwa kuwapa hati ili waweze kulipa kodi ya jengo katoa angalizo kwamba hatoi ruksa au kuhalalisha waanze kujenga sasa ili wapate huruma hiyo upendeleo wamepewa wenye nyumba za zamani.

Pia katoa agizo kwa wakurugenzi wa miji kuziwekea alama ya x nyumba mpya zinazojengwa ktk maeneo ya wazi na yasiyoruhusiwa au yenye utata wa umiliki na yasiyopimwa hizo zitabomolewa.
 
Hivi kweli mtu anafuatilia kibali cha kujenga nyumba anazungushwa bara sijui baraza la madiwani sijui imekuwaje panda shuka na mtu ameshachukua mkopo anazungushwa tu

Akaamua kujenga mjengo wake tuseme ametumia kama m50+ umekamilika leo hii uje kuubomoa eti hana kibali?????


Malparida putas, mnataka watu wawanywe supu sio?
 
Back
Top Bottom