Maagizo ya Rais Samia kwanini hayafanyiwi kazi kwa wakati?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,900
2,000
Agizo la kufuta kesi zote hewa za watu waliobambikizwa kwanini watu bado wapo mahabusu mfano Mashehe wa uhamsho?

Agizo la kufungua vyombo vya habari mpaka sasa kimya

Agizo la kufungua biashara kati ya Tanzania na Kenya leo usiku kuna wavuvi wa Kenya wamekamatwa kwenye ziwa Victoria.

Report ya CAG mpaka sasa kimya

Suala la bundle mpaka leo voda na airtel bado wamegoma kurudisha bundle za zamani

Suala la kulikemea Bunge kwamba wawe wana discuss issue ambazo zinahusu taifa juzi tu Ndugai katapika tena eti anamkemea Nape kwa kuwasema wabunge wa viti maalumu.

Sasa tutasema tuna Rais hapa Rais ambaye akitoa maelekezo watu hawafanyi?

Nasisitiza nipo na Mama kwenye suala la kufufua uwekezaji nchini lakini sikubaliani yeye kushindwa kusimama kwenye uzembe na uwajibikaji wa watu wote walio chini yake.

Afanye maamuzi magumu sometime asiwe Rais Dhaifu.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Agizo la kufuta kesi zote hewa za watu waliobambikizwa kwanini watu bado wapo mahabusu mfano Mashehe wa uhamsho?
Umejuaje kuwa Masheikh wa Uamsho wamebambikiwa kesi ?

Wengi tunapenda Uamsho watendewe haki. Kama ni dhamana wapewe na kama wana hatia basi wafungwe ifahamike. Na kama hawana hatia waachiwe.

Kitu ambacho hakitakiwi ni kuwaweka watu mahabusu Miaka 10 au zaidi. Huu ni upuuzi kwasababu siku wakikutwa hawana hatia utawalipa fidia ya muda wao?
Agizo la kufungua vyombo vya habari mpaka sasa kimya
Wewe unamiliki chombo cha habari?

Mmiliki gani wa chombo cha habari umesikia analalama kwamba chombo chake kimekataliwa.

Ninavyojua Kubenea mpaka sasa ameshakutana waziri husika na labda wapo kwenye process.

Kuhusu Mbowe na Tanzania Daima sijui.

Maria Sarungi wa Kwanza TV mwenyewe kasema haendi na mpaka sasa kashaanzisha channel mpya Mwanzo TV.
Agizo la kufungua biashara kati ya Tanzania na Kenya leo usiku kuna wavuvi wa Kenya wamekamatwa kwenye ziwa Victoria.

Kufungua biashara tafsiri yake siyo kwamba biashara zifanyike kiholela. Kwamba kwasababu biashara zimefunguliwa ndio wavuvi wa Tanzania wakavue samaki kiholela upande wa Kenya?

Una akili wewe kweli?
Report ya CAG mpaka sasa kimya

Report ya CAG kwa upande wa serikali tayari, kwasasa iko stage ya bunge.

Bunge liko kimya then unamlaumu Rais, kweli?

Sote tulikuwa tunalia hapa uhuru wa bunge leo tena tunataka Rais aburuze bunge !!!
Suala la bundle mpaka leo voda na airtel bado wamegoma kurudisha bundle za zamani

Kwamba Rais aingilie mpaka makampuni binafsi ayalazimishe namna ya kupanga bei ya bidhaa zao, siyo?

Binafsi natumia VodaCom na Halotel. Bundle za Voda hazijawahi kuwa cheap. Na hii ni kutokana na kasi na ubora wa internet yao ukilinganisha na mitandao mingine.

Usilazimishe kupata kitu bora kwa bei kitonga. Ukiona Voda hawajabadili au wamebadili kidogo maana yake wateja wake wengi wanamudu kununua hivyo hivyo. Kuna mitandao 4 nchi hii, hamia penye unafuu. Achana na kampuni za watu.

Mimi mwenyewe bundle natumia Halotel, ikitokea watu wote wakayasusa mabando ya Voda automatically wao wenyewe watarekebisha.
Suala la kulikemea Bunge kwamba wawe wana discuss issue ambazo zinahusu taifa juzi tu Ndugai katapika tena eti anamkemea Nape kwa kuwasema wabunge wa viti maalumu.

Magu alikuwa anadhibiti bunge tunalalamika. Leo tena tunataka Rais adhibiti bunge,!!

Rais atakachofanya ni kutoa ushauri lakini kutaka kulazimisha Rais aingie kwenye midomo na akili za wabunge na kuwalazimisha namna ya kuongea. Huu ni upumbavu.

Sote tunajua akili za wabunge waliomo mle ndani.
Sasa tutasema tuna Rais hapa Rais ambaye akitoa maelekezo watu hawafanyi?

Nasisitiza nipo na Mama kwenye suala la kufufua uwekezaji nchini lakini sikubaliani yeye kushindwa kusimama kwenye uzembe na uwajibikaji wa watu wote walio chini yake.

Afanye maamuzi magumu sometime asiwe Rais Dhaifu.
Huna akili.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,422
2,000
Kuna challenges anazokutana nazo huyu mama lazima zimtoe jasho, japo nyingine naona ziko ndani ya uwezo wake kabisa.

Mfano hilo la masheikh wa uamsho hata wenzake liliwatoa jasho, japo naamini serikali ndio haijaamua kuwa serious kusikiliza hiyo kesi, video za mahubiri ya yale jamaa zikitumika na kauli zao makosa yao yapo wazi.

Kuhusu vifurushi vya simu hili ndio linafanya nimuone Rais yuko "soft" sijui ni kitu gani haswa kinachomshinda, kitendo cha kutoa agizo halafu lisitekelezwe ni dharau, hawa jamaa wa makampuni ya simu sijui wanajiamini nini, au labda ni ule "udhamini" wanaowapa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi.
 
mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
567
1,000
Moja ya sifa ya kuwa kiongozi ni aidha kuogopwa au kusikilizwa vikikosekana hvyo jua kuna tatizo sehemu, bahati mbaya sana matarumbeta ni mengi kuliko kufanya kazi mama ameamua kutengeneza Brand (2025) baada ya kusimamia mission na vision yake
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,798
2,000
Abadilishe watu
Kuna challenges anazokutana nazo huyu mama lazima zimtoe jasho, japo nyingine naona ziko ndani ya uwezo wake kabisa.

Mfano hilo la masheikh wa uamsho hata wenzake liliwatoa jasho, japo naamini serikali ndio haijaamua kuwa serious kusikiliza hiyo kesi, video za mahubiri ya yale jamaa zikitumika na kauli zao makosa yao yapo wazi.

Kuhusu vifurushi vya simu hili ndio linafanya nimuone Rais yuko "soft" sijui ni kitu gani haswa kinachomshinda, kitendo cha kutoa agizo halafu lisitekelezwe ni dharau, hawa jamaa wa makampuni ya simu sijui wanajiamini nini, au labda ni ule "udhamini" wanaowapa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi.
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,944
2,000
Vitu vya kisheria vinaisha kisheria hata Mzee waliposhika ndege kuwaachia watu ilikua mpaka DPP aende na makabrasha yake makubwa watu wakubaliane wasaini hata Rugemalila alikataa kukubaliana na Mzee wakaamua kukaa wamalize kesi yao kisheria na si kukubaliana kutoa fedha kwa Mzee nakumbuka aliwahi sema hadharani kuwa mawakili wanawashauri vibaya wakina Rugemalila na baadae kesi ikaanza kupewa tarehe ndefu ndefu hata yule mkwe wa Lowassa kutolewa ilikua kwa sababu Lowassa kaunga juhudi tuu...usijifanye kutafuta makosa kila ukilala na kuamka.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,136
2,000
Mambo ya kesi yanahitaji muda...kumbuka lazima wapande mahakamani ndio mahakama iwaachie ....sio vinginevyo
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,871
2,000
Mambo ya kesi yanahitaji muda...kumbuka lazima wapande mahakamani ndio mahakama iwaachie ....sio vinginevyo
Bavicha wanajua basi wao wamezoea kuweka akili mfukoni au kushikiwa kabisa.
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,921
2,000
Vitu vingine vipo kisheria zaidi na yale mambo eti ya “Rais akiongea kitu inakuwa ni amri” hatuyataki tena kwani huo ndio mwanya wa kuibaka Katiba mchana kweupe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom