Maagizo ya Rais Samia kwa Waziri Bashungwa kuhusu kujenga Academy ya michezo kila mkoa nchini ni mazuri

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu wakati akiwa Mwanza nilimsikia Rais Samia akizungumzia suala la uanzishwaji wa academics kwa kila mkoa ili kukuza sekta ya mchezo wenyewe.

Ni jambo jema sana ila mimi nina mawazo tofauti na ushauri pia kwamba academy hutayarishwa na timu zote zinazoshiriki kwenye ligi, kuanzia timu kubwa hadi ndogo.

Timu zinapangwa kwa umri na wanakuwa na ligi zao kila mwaka na pia wale ambao wanafaulu mafunzo wanachaguliwa katika timu za wilaya, mikoa hadi taifa kuanzia miaka 15, hapo ndio tunapata timu za taifa under 15, 17, 19, 21 na Taifa Stars.

Lakini wakisema kuanzisha shule za michezo tano au sita ni kupoteza wakati tu.

Maana wenzetu ughaibuni kila timu iliyosajiliwa na inayoshiriki ligi katika madaraja yote huwa na academies ambazo zina umri kuanzia miaka 6 hadi 18.
 
Wewe Acha kukariri.

Tunatakiwa tuwe na viwanja vya michezo yote kila kata.

Sasa timu za mpira zitafanya hivyo?

Kila kata inatakiwa kuwa na viwanja vya michezo.

Michezo yote sio Tu football.

Agizo hili limechelewa sana
warudishe kwanza viwanja vyaa michezo vilivyoporwa, kulikuwa na viwanja vingi vya michezo ambavyo vimegeuzwa matumizi yake , pia shule nyingi zinazoanzishwa hazina viwanja vya michezo.
 
warudishe kwanza viwanja vyaa michezo vilivyoporwa, kulikuwa na viwanja vingi vya michezo ambavyo vimegeuzwa matumizi yake , pia shule nyingi zinazoanzishwa hazina viwanja vya michezo.
.......wamepora hadi ofisi za serikali wanamiliki kama za kwao wakati hawajawahi kujenga hata ofisi moja ktk nchi hii huku wakivikejeli vyama vingine kwamba havina ofisi...!!!
 
Kulitakiwa kuwe na kiwanja kila kaya 25/30.

Sehemu nyingi za Dsm unakuta kaya 1000+ na hakuna kiwanja halafu tunashangaa kwanini taifa la watu 60 mil haliwezi kuzalisha wachezaji hata 10 wenye uwezo wa kucheza ligi 5 bora za ulaya.

Viti vingine vinakera basi tu yaani
 
Wewe Acha kukariri.

Tunatakiwa tuwe na viwanja vya michezo yote kila kata.

Sasa timu za mpira zitafanya hivyo?

Kila kata inatakiwa kuwa na viwanja vya michezo.

Michezo yote sio Tu football.

Agizo hili limechelewa sana
Mkuu Sio Kwamba Nina kariri Ila Hoja yangu Ni Kuwa, Inabidi kujipanga sio kujifanyia kiholela kwasababu tu tunataka tuwe na accademy. Maana ya football academy ni kuwainua vijana wawe na ujuzi na uwezo wa kishindana katika kiwango cha juu, na kukuza hivyo viwango vijana wanatakiwa kuwa na mashindano mengi ili kuimprove competitive skills zao, wanahitaji ligi za mwaka mzima na sio mechi mbili tatu.
.....
Ndio maana ikawekwa mfumo huo wa kila umri kuanzia miaka 6 wawe na ligi yao mwaka mzima na ndio maana wamefanya timu zote zilizosajiliwa ziwe na timu za vijana hao ili wawe na mashindano ya kutosha.
....
Hapo ndipo utaona wachezaji wastaafu au wale waliopata majeruhi sugu hawakosi kazi za ukocha kwani timu zitakuwa nyingi na ajira nyingi za ukocha zitapatikana.
 
Na naomba waweke hili jambo vizuri,Sports Academy msije kutujengea wiwanja vya mpira wa miguu tuu hapana bali iwe Sports Academy Complex zikiwa na viwanja vya michezo mbalimbali kama kuogelea,tenisi,golf,rugby nk nk.

Chondechonde naomba vijengwe kila mkoa na viwe na eneo la kutosha.Kwa muktadha huu ni pesa ya kutosha inatakiwa kutumika, na nashauri Serikali iwe inawapeleka vijana wenye vipaji tuu ili kusudi baada ya miaka kadhaa tuanze kuuza wachezaji na watu amabao watawataka hao vijana lazima watoe pesa.
 
Kulitakiwa kuwe na kiwanja kila kaya 25/30.

Sehemu nyingi za Dsm unakuta kaya 1000+ na hakuna kiwanja halafu tunashangaa kwanini taifa la watu 60 mil haliwezi kuzalisha wachezaji hata 10 wenye uwezo wa kucheza ligi 5 bora za ulaya.

Viti vingine vinakera basi tu yaani
Sio lazima iwe ulaya inaweza kuwa kwa level ya africa
 
warudishe kwanza viwanja vyaa michezo vilivyoporwa, kulikuwa na viwanja vingi vya michezo ambavyo vimegeuzwa matumizi yake , pia shule nyingi zinazoanzishwa hazina viwanja vya michezo.
Shule nyingi za msingi zina viwanja tatizo ikifika jioni wakubwa wanawafukuza wanafunzi uwanjani ili yenyewe yafanye mazoezi badala ya kwenda kulima huko. Shida ya msingi ipo hapa kwahiyo hata ukiweka kiwanja kila shule hakitumiki kwa walengwa
 
Wakuu wakati akiwa Mwanza nilimsikia Rais Samia akizungumzia suala la uanzishwaji wa academics kwa kila mkoa ili kukuza sekta ya mchezo wenyewe.

Ni jambo jema sana ila mimi nina mawazo tofauti na ushauri pia kwamba academy hutayarishwa na timu zote zinazoshiriki kwenye ligi, kuanzia timu kubwa hadi ndogo.

Timu zinapangwa kwa umri na wanakuwa na ligi zao kila mwaka na pia wale ambao wanafaulu mafunzo wanachaguliwa katika timu za wilaya, mikoa hadi taifa kuanzia miaka 15, hapo ndio tunapata timu za taifa under 15, 17, 19, 21 na Taifa Stars.

Lakini wakisema kuanzisha shule za michezo tano au sita ni kupoteza wakati tu.

Maana wenzetu ughaibuni kila timu iliyosajiliwa na inayoshiriki ligi katika madaraja yote huwa na academies ambazo zina umri kuanzia miaka 6 hadi 18.
Yaani Nchi Ina viwanja viwili vyenye hadhi, na kimoja ndio chenye kiwango cha kimataifa.
 
Back
Top Bottom