Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,665
- 15,061
Wadau amani iwe nanyi
Leo nimekaa na kutafakari msitakabali wa nchi yetu nimekuja na ugunduzi wa mambo kadha wa kadha.
Kwenye siasa za nchi yetu kuna kundi la watu ambalo kazi yao ni kuwaaminisha Wananchi kwamba kiongozi fulani hafai hivyo wasifuate maagizo yake lakini wananchi ndiyo kwanza wanazidi kumfuata na kumsikiliza huyo kiongozi!
Chadema wamekuwa wakimwandama sana RC Makonda na kujaribu kumfubaza mbele ya Wananchi tangu kipindi kile amtaje Mbowe kwenye genge la wauza madawa ya kulevya nchini na kupelekea madawa kuisha kabisa mitaani na mateja kupungua mno nchini kote, tangu hapo kila atakachoagiza Makonda Chadema lazima wapinge.
Mfano tarehe 20/April Makonda alitaka kila mwana Dar es salaam kuanza kuvaa barakoa ili kujikinga na na hivi virus vya Corona lakini Chadema walipinga agizo hilo kwa nguvu zote!
Chadema walipinga agizo hilo kwa kisingizio kwamba anayetakiwa kutoa agizo la kuvaa barakoa ni waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Lakini cha kushangaza pamoja na Chadema kuwataka wananchi wasivae barakoa lakini wananchi wameitikia kweli kweli wito wa Makonda kila kona ya jiji wananchi wameva barakoa, hii ina maana gani kwa Chadema
Je, ina maanisha chadema haisikilizwi tena na wananchi? Mvuto wa chadema umekwisha?
Nini kimetokea chadema iliyokuwa inaagiza watu watoke nje kuandamana na wanatoka kweli licha ya mabomu leo imekuwaje hawafuati maagizo ya chadema? Ni laana ya Dk Slaa? Kwa hali hii Chadema itashinda uchaguzi wowote?
Yetu macho.