Maagizo ya machinga na Corona kupuuzwa nini chanzo? Ni kivuli cha Magufuli?

Rais SSH amewajengea hofu viongozi wa mikoa na wilaya baada ya kuwatumbua DC na mkurugenzi wake pale Morogoro mjini. Mama anajipendekeza kwa machinga na bodaboda ili 2025 wampigie debe.

Na kuhusu korona mzimu wa Magufuli juu ya kuhimiza watu watumie njia za kishirikina za kujifukiza bado upo. Na kwa kuwa watanzania wengi ni wajinga na ni washirikina itakuwa ngumu kuchukua tahadhari.

Labda mama atumie mbinu ya Durtete, mtu asiyetaka kuvaa barakoa na chanjo jela.
kama njia za kishirikina zimetufaa hatuna budi kuzitumia maana majirani wametumia njia za kisasa bt matoken yake corona imewaendesha na kila siku wanafunga mashule na madhara ni makubwa kuliko sisi.

ufike wakati tupunguze unafiki hata kama hatumkubali mtu basi tuthamini juhudi yake ilolivusha taifa katika kipindi kigumu zaidi.
 
ndicho kinajadiliwa hapa,tamko lilikuwa waondoke.

kwani unadhani hoja ni wao kuziba biashara au kuuza bila kulipa kodi,na kunyima wateja wenye frem rasmi!!!!
Baada ya Hilo Tamko mama Samia si alikuja Kariakoo ku clarify? Maagizo yake yalikua waondoke ama wa behave?
 
Tatizo hata hao wataalamu wetu wenyewe ni watu wa kukaririshwa tu, kuna siku nilikuwa namsikiliza Doctor wa muhimbili alikuwa anahojiwa yani yeye anaona kabisa kuwa hizi chanjo za corona ina shida mahali kuhusiana na huku kugandisha damu na anaona kuwa ni kitu ambacho inafaa tuelezwe ila ndio hivyo tena wenye jukumu hilo wao wanakomaa kusema chanjo hazina shida.
Siyo kila Daktari anaweza kuongelea chanjo. Hili liongee na mabingwa wa virology and immunology wengine wanajuwa mambo yao tu. Kwa mfano Dr Mollel Naibu Waziri kwenye immunology Ni mbumbumbu kwa vile yeye ni dentist, ukitaka mjuzi hapa ongea na Dr Faistine Ndugulile ambaye kwa sasa ni Waziri wa vifurushi vya mitandao
 
Kwa nini usizifuate Dubai?
Kwenda Dubai hatuendi kwa Super Feo kama kwenda Songea.

Ukweli Mwendazake alipotosha sana na nadharia zake za kipumbavu. tunashukuru Mungu ametukomboa toka mikono ya Afriti Shetani
 
Siyo kila Daktari anaweza kuongelea chanjo. Hili liongee na mabingwa wa virology and immunology wengine wanajuwa mambo yao tu. Kwa mfano Dr Mollel Naibu Waziri kwenye immunology Ni mbumbumbu kwa vile yeye ni dentist, ukitaka mjuzi hapa ongea na Dr Faistine Ndugulile ambaye kwa sasa ni Waziri wa vifurushi vya mitandao
Na point yangu ilikuwa kwamba tunakaririshwa sana vitu, huyo Daktari alikuwa anaeleza kwa maoni yake binafsi tu ila tatizo hawafundishwi kuwa hivyo.
 
Lakini Ndege, Sgr, flyover hazijafutika na utazitumia sana huku nafsi ikikusuta mpaka kufa kwako
Kodi yang inanifanya nizitumie, ctumii bure ingekua alitoa pesa yake mfukoni sawa lkn ni pesa ya watanzania. So hilo sio la kujivunia juu yake bali ni watanzania. Halafu acha kupotosha.. Tanzania bado hatuna flyover tuna madaraja ya juu, tuliotembea tunajua what is flyover
 
Imani kubwa ya waafrika ni maisha baada ya kifo. Waliokufa wanaendelea kuwepo. Huu pia ni ujinga
 
Lakini Ndege, Sgr, flyover hazijafutika na utazitumia sana huku nafsi ikikusuta mpaka kufa kwako
Kuna barabara, reli, madaraja, miji, majengo n.k. yaliyoasisiwa na wakoloni, je tuendelee kuwasujudia hata leo na kesho? Ukiangalia kwa mfano miji na barabara tunazo karabati kwa magorofa mapya, lami na kokoto tunafuata mule mule walimopita wakoloni. Tukubali mabadiliko la sivyo tutakuta watu wakipungua mitaani bila kulazimishwa. Kwenye Biblia kuna habari ya Nuhu watu walimcheka na kumdhihaki, mwisho wa siku waliangamia.
 
Ningeshangaa msaliti kulipwa hela. Kwa kazi ipi aliyofanya? Kwa kuzunguka nchi za ulaya akiitukana Tanzania na watanzania?
Tutashitakiwa MIGA?

UJINGA MTUPU
Noah zetu ziko wapi, mzee? Hatujasahau ahadi. Tunaomba zisichelewe sana maana idadi ya watu inaongezeka kwa kasi kwa kuwa ni ruksa kufyatua bila kikomo!
 
Tulishuhudia mkuu wa mkoa wa Dar Bw. Amos Makala alipoapishwa tu alitoka mbio mbio kwenda kutangaza oparation ya kuondoa machinga na ombaomba wote ili jiji lirudi kwenye hadhi yake ya usafi, lakini mpaka leo agizo hilo halijatekelezwa.

Makala alifanya mpaka kikao na wakuu wa wilaya, madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwapa maagizo ili kuwezesha kuwatoa wamachinga, mpaka magari yalianza kupita mitaani yakitangaza wamachinga wote waondoke lakini mpaka leo kimya shughuli zinaendelea kama kawaida.

Haikupita muda kamati ya Corona iliyoundwa na rais Samia ikaja na mapendekezo ya kuwataka wanachi wote kuvaa barakoa na kufanya social distance, pia walimtaka waziri wa afya atangaze idadi ya wagonjwa wa corona wanaopatikana kila siku ,pia wiki mbili baadae chama cha madaktari Tanzania kikatoa tamko la kuwataka watanzania kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono na kuvaa barakoa muda wote.

Freeman Mbowe na Chadema pia mapema kabisa alitangaza kuwa yeye amechanjwa na kuwataka watanzania kuvaa barakoa na kujiandaa kupokea chanjo, maagizo yote hayo yamepuuzwa na wananchi mpaka sasa.

Pita sabasaba, kwenye mwendokasi, Kariakoo wananchi wanaendelea na maisha yao kama kawaida kana kwamba kamati ya Corona na chama cha madaktari hawajatoa tamko lolote!

Chanzo cha maagizo haya kupuuzwa nini? Je, ni Kauli za Magufuli bado zinaendelea kuishi kwenye ubongo wa watu?

Baadhi ya wananchi wamehojiwa kuhusu maagizo hayo wamesema maagizo hayo hayana tija yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuwatia hofu watu.
Halaf maisha yanaendelea kama kawaida wala hakuna Vifo uzur wake
 
Very sure... Suala na corona kwa mfano,.... Tushazoea maisha yetu tukifurahia uhuru, leo wanakuja na masheria yao kwa ajili ya kufurahisha wazungu... Huku mtaani maisha ni yale yale ya siku zote... Wanapokuja kutaka kuturudisha kwenye hofu ni upuuzi mtupu...

Back
Top Bottom