Maagizo waliopewa watendaji Ikulu yaanza kufanyiwa kazi uchaguzi Serikali za mitaa, upinzani wafungiwa ofisi, fomu zimekwisha, wagombea kutekwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,873
FB_IMG_1572406150304.jpg
FB_IMG_1572422569209.jpg
 
Vyama vya upinzani naomba msituletee habari za ajabu,ninyi ni vyama vya upinzani na sio vyama vya malalamiko.

Hali hii imeanza tangu 2015 na hamkuchukua hatua zozote ni kulalama tu na kuendelea na biashara kama kawaida,chaguzi zinakaribia mmeanza tena kulalamikia mambo yale yale. Hii sio biashara ya kichaa kweli?

Watu walisusa kujiandikisha kwasababu hizi mkawahamasisha,mnalalamika nini sasa? Si mnaamini hali ipo sawa kiushindani ndio maana mkawahamasisha?
 
@="lukesam,

Hivi wewe hukuwahi hata kusikia Amnesty International na Human Rights watch walivyolalamika kuhusu uminywaji wa demokrasia nchini Tanzania?

Hivi unataka wapinzani wafanye nini, ili hali Jeshi la Polisi nchini, limegeuzwa kama kitengo cha CCM?
 
Wakati wa kuchukua maamuzi magumu ni sasa ili kuleta heshima. Kuishia kulalamika hakuta saidia kitu, hata kumwagia mmoja wapo maji ya moto ili kutoa funzo inashindikana! Kabisa mtu anagoma kutoa fomu ama kufunga kwa makusudi ofisi ya serikali anaachiwa hivi pasipo kudili naye "personally" ili kutoa fundisho. Hata manati hakuna?
 
Kwa saa vyama vya upinzani vingewekeza nguvu nyingi kwenye kudai katiba mpya.

Uchaguzi kwenye utawala wa kidikteta huwa hauna maana. Watawala ili kuwahadaa walimwengu, wataacha maeneo machache sana haki itendeke ili kupata justification kuwa tunafuata mfumo wa vyama vingi lakini kiuhalisia hakuna uchaguzi.
 
Hivi wewe hukuwahi hata kusikia Amnesty International na Human Rights watch walivyolalamika kuhusu uminywaji wa demokrasia nchini Tanzania??

Hivi unataka wapinzani wafanye nini, ili hali Jeshi la Polisi nchini, limegeuzwa kama kitengo cha CCM??

Kama umesoma mchango wangu nadhani utakuwa umeelewa kabisa natambua hali halisi iliyopo.

Unafikiri ni kwanini hao wapinzani waendelee kushiriki chaguzi ambazo wanaona hazipo sawa kiushindani? Je,waendelee kushiriki tu huku wakilalama mwanzo hadi mwisho kila ufikapo uchaguzi?

Kama wameshindwa kuhakikisha usawa katika uchaguzi ni kwanini wanahamasisha watu wakajiandikishe?
 
Wenye kujitambua tulishasema hakuna uchaguzi bali ni uchafuzii.nimemsikia Mkuu wa wilaya ya hai akiwatishia wagombea wa CHADEMA.

Eti yeye Ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.wagombea wote walipaswa kupewa fomu, waachiwe wananchi wenyewe waamue kwenye sanduku la kura.
 
Bangi zinakuharibu kichwa Mbugila wewe

Wewe nilishabaini una matatizo ama ya kimalezi au ya kisaikolojia muda sana tokea kwenye jukwaa la MUFC kule mkuu.

Kama ni tatizo la kisaikolojia ukipona utajishangaa,ila kama ni tatizo la kimalezi basi kupona ni lazima urudi ukalelewe upya,ni ngumu kupona,pole sana.
 
Wewe pia una lalamika nmetegemea utatoa solution kumbe ni lawama tu
Vyama vya upinzani naomba msituletee habari za ajabu,ninyi ni vyama vya upinzani na sio vyama vya malalamiko.

Hali hii imeanza tangu 2015 na hamkuchukua hatua zozote ni kulalama tu na kuendelea na biashara kama kawaida,chaguzi zinakaribia mmeanza tena kulalamikia mambo yale yale. Hii sio biashara ya kichaa kweli?

Watu walisusa kujiandikisha kwasababu hizi mkawahamasisha,mnalalamika nini sasa? Si mnaamini hali ipo sawa kiushindani ndio maana mkawahamasisha?
 
Back
Top Bottom