Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi Machi 3, 2017 alimaliza ziara yake ya awamu ya pili katika kata kumi za wilaya hiyo ambapo alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuzungumza na wananchi sambamba na kuamsha hari ya utendaji kazi kwa watumishi wa Manispaa ya Kinondoni. Hii inafanya Hapi kuwa ametembelea wananchi na kukagua maendeleo katika kata zote 20 za wilaya yake ya Kinondoni jambo ambalo baadhi ya wazee wa kata za Kinondoni ikiwemo kata ya Hananasifu wanalitaja kama ni la kihistoria kuwahi kutokea.
Awamu ya kwanza ya ziara ya DC Hapi ilifanyika robo ya mwisho ya mwaka 2016 mwezi septemba hadi Oktoba kabla ya kufanyika kwa ziara ya 'Dar Mpya' iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa nyakati tofauti katika ziara yake awamu ya pili ambayo alianzia kwenye kata ya Mbweni na kumalizia kata ya Makongo Juu, Hapi alitoa magizo mazito kwa viongozi na watendaji kuanzia ngazi ya mtaa hadi kata pamoja na watumishi wa umma yaliyolenga kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi kuanzia sekta ya elimu, afya, miundombinu, pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha ziara hii ya aina yake iliwapa wananchi wa maeneo husika fursa ya kuuliza maswali na kueleza kero zao mbele ya Mkuu wa Wilaya na timu aliyoambatana nayo.
Miongoni mwa maagizo hayo ni pamoja na kupiga marufuku viongozi wa serikali za mitaa kuchangisha wananchi fedha za michango ya maendeleo pasipo kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Aaron Kagurumjuli kutokana kwamba uchangishwaji holela wa fedha kwa wananchi unasababisha upotevu wa fedha na ubadhirifu kitendo kinachokwamisha utekelezaji wa miradi husika na kuibua malalamiko.
Hapi alilitoa agizo hilo kwenye kata ya Kijitonyama na Makongo baada ya kubaini uwepo wa malalamiko ya ubadhirifu wa michango ya fedha za umma unaofanywa na baadhi ya wenyeviti.
Katika ziara yake hiyo, Hapi alikutana na hoja nyingi za migogoro ya ardhi hususan uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii, na kwamba kwa sababu ya uvamizi wa maeneo hayo, kuna baadhi ya kata hazina shule, zahanati na vituo vya polisi kutokana na kutokuwa na maeneo. Kufuatia uvamizi huo aliagiza vyombo vya usalama kufuatilia na hatimaye Kamati ya ulinzi kuunda kamati ya kuchunguza maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi ili kuyarejesha serikalini. Alilitoa agizo hilo alipotembelea kata ya Kinondoni.
Agizo lingine alilolitoa ni kwa wakuu wa shule na walimu kutowachangisha wanafunzi fedha za michango mbalimbali kwani michango hiyo imefutwa, na kwamba kwa wazazi wanaotaka kutoa michango yao kwa hiari kwa shule hawana budi kupata kibali cha Mkuu wa Mkoa. Aidhaa, michango hiyo yapasa kutoipitishia kwa wanafunzi au waalimu moja kwa moja bali wazazi wakiamua kwa hiyari wachangishane fedha na kuzielekeza katika mradi husika uliokusudiwa kutekelezwa au akaunti ya shule.
Katika hatua nyingine, Hapi aliwaagiza watendaji wa serikali za mitaa na kata kutoa taarifa kwa wananchi juu ya mapato na matumizi ya maeneo yao ili wafahamu miradi iliyoko kwao na matumizi ya fedha za serikali na zile zinazotozwa kwa wananchi kama tozo za usafi na ulinzi shirikishi. Agizo hilo lilitolewa alipokuwa katika hitimisho kata ya Makongo Juu baada ya kupata taarifa za upotevu wa fedha zilizochangishwa na wananchi wa kata hiyo zaidi ya milioni 9.
Kwa upande wa sekta ya afya, Hapi aliwaagiza maafisa afya kuanzia ngazi ya kata hadi manispaa kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaochafua mazingira kinyume cha sheria pamoja na wale wanaokaidi agizo la kutoa fedha za ushuru wa taka, kwa kuwa hukwamisha shughuli za uzoaji taka na kusababisha magonjwa ya milipuko hasa wa kipindupindu. Aidha, alimuagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Mohamed Msangi na Afisa MipangoMiji Respicius Mathew kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa dampo la kisasa la manispaa ambapo alishauri eneo la Boko Chama ambalo lilikuwa linachimbwa kokoto kuwa dampo kuwa linaweza kutazamwa kwa shughuli hiyo.
Hali kadhalika, Hapi alipiga marufuku biashara ya uvuvi haramu katika ukanda wa pwani wa wilaya ya Kinondoni sambamba na kuanzisha vita dhidi ya uvuvi haramu ambapo aliteketeza nyavu haramu zenye thamani ya shilingi milioni 60 na alimkabidhi kamishna wa polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni suzan akaganda majina ya wanaotajwa kuhusika na uvuvi haramu yaliyowasilishwa kwake na wananchi kwa uchunguzi na hatua za kisheria.
Agizo lingine alilitoa ni kwa watendaji wa kata, mitaaa na manispaa ambapo aliwataka kutembelea wananchi ili kubaini changamoto za wananchi pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Mh. Hapi aliambatana na timu ya wataalam wa manispaa ya Kinondoni wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo.
Tukutane sehemu ya pili ya makala hii ya ziara ya DC Hapi.