Maagizo fedha za UVIKO-19 kutumia wakandarasi wazalendo ni ya kupongeza

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Nilimsikia Rais Samia akisema katika ujenzi unaofanyika watumie wataalamu na wakandarasi wazalendo. Haya ni maamuzi ya kizalendo sana na ya kupongeza sana.

Hizo ndizo njia pekee za kutengeneza ajira na kukuza uchumi kwa watu wetu.

Asia na Ulaya walishaanza mbinu hizo muda mrefu kwani wakikopesha fedha wanataka kazi wafanye watu wao ni wakati na sisi fedha zetu wenyewe na tunazokopa ili watu wetu waje kulipa tutizame ni kwa namna gani tunatumia watu wetu.

Pongezi kubwa kwa mama yetu kuwaza hili.
 
Ulaya watu ni waaminifu pia hakuna rushwa, huku miradi inatolewa kwa kujuana na rushwa ndiyo maana kazi zinakwama
 
Ulaya watu ni waaminifu pia hakuna rushwa, huku miradi inatolewa kwa kujuana na rushwa ndiyo maana kazi zinakwama
Uaminifu unajengwa na mifumo ya maisha iliyowekwa katika jamii, kabla ya kufikia hatua hiyo waliyonayo walipitia mazingira kama yetu ila sisi tunayonafasi ya kwenda kwa haraka zaidi ya wao walikopitia.

Tusijenge woga na kujikwamisha bali tufocus mbele na kujifunza kutoka kwao.

Ni sawa na mtu anayekwenda porini mara kwanza huangaika kutengeneza njia na huyu mtengeneza njia huhangaika sana lakini wanaokuja baadae hupitia njia zile zile alizotengeneza huyu wa kwanza na wao hupita kwa haraka
 
uaminifu unajengwa na mifumo ya maisha iliyowekwa katika jamii, kabla ya kufikia hatua hiyo waliyonayo walipitia mazingira kama yetu ila sisi tunayonafasi ya kwenda kwa haraka zaidi ya wao walikopitia.

tusijenge woga na kujikwamisha bali tufocus mbele na kujifunza kutoka kwao.

ni sawa na mtu anayekwenda porini mara kwanza huangaika kutengeneza njia na huyu mtengeneza njia huhangaika sana lakini wanaokuja baadae hupitia njia zile zile alizotengeneza huyu wa kwanza na wao hupita kwa haraka
Fanya utafiti Africa inakila aina ya rasilimali lakini ni masikini wa akili, rushwa na uongozi mbovu.
 
Back
Top Bottom