Maafisa wapya wa JWTZ wanaapishwa Ikulu Dar es Salaam leo na siyo Monduli

Warrior

JF-Expert Member
Oct 2, 2015
612
1,000
Sasa hizo commisionned ranks za second lieutenant si zina watu wa nchi jirani? sasa kuwapeleka nyumba kuu kiholela holela aaah mimi nimenuna aisee twitwitwitwiiiiii

Uwe unafuatilia habari husika kabla ya kupost , aliyekuwambia kuna watu wa nje kwenye kupewa kamisheni ni nani ????
 

Panapet

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
748
500
Leo asubuhi nilitaka kupita njia ya Ikulu ya huku baharini nikakuta imefungwa, kumbe kuna Maafisa wa JWTZ (Officer Cadets) wanakula kiapo leo na kuwa Maluteni usu. Hii shughuli ndo kwa mara ya kwanza inafanyikia Ikulu, nasikia huwa miaka yote ya nyuma hufanyika Monduli Arusha.

Hivyo mnaotaka kutumia njia hiyo imefungwa kwa sasa.

============

Kipindi Mubashara TBC1 ni hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa 194 wa JWTZ. Kwa kuwa mafunzo ya kamisheni yamefanyika Monduli na kuhitimishwa kwa hafla fupi ya kukamilisha utoaji wa kamisheni kwa Maafisa hao wa JWTZ katika viwanja vya Ikulu Magogoni.

Je, utaratibu huu wa kutoa kamisheni kwa maafisa wa JWTZ kufanyika Ikulu ni utaratibu mpya badala ya Rais kwenda Monduli kulikofanyika mafunzo au ni kubana matumizi kwa safari ambayo angeenda Monduli?
86b554ecb7b4d2b8f1fb26a34a442ad4.jpg

40b79aee278d96a75131784582cf2e95.jpg


Pongezi kwa mh rais hakuna haja za safari za monduli .
 

Hansss

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,370
2,000
Mi hata sielewi naona mambo hobelahobela tu km niko kijiji cha ukimbizini yaan
 

Olecranon

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,383
2,000
Unaonaje ukianzisha uzi wako mkuu useme unachotaka kusema!mimi lengo langu ni kuwajulisha wadau wanaotumia njia hyo wasisumbuke kupita huko na kuwahabarisha nini kinaendelea leo katika viwanja vya ikulu,kwani ni mara ya kwanza hyo barabara inafungwa kwa shughuli za kiserikali acha hii ya leo?!think positive!!
Umeweka thread yako hapa na umeelezea kuwa maafisa wa jeshi wanaapishwa ikulu hivyo barabara imefungwa. Sasa GT wanajadili toka lini hili likafanyika ikulu? Tangu enzi za Nyerere mahafali haya hufanyika monduli na hili ndio watu wanajadili. Wanajiuliza, je ni kubana matumizi? Binafsi sidhani kwani kuleta watu 200 Dar uwagharamie usafiri, malazi na chakula hiyo itakuwa pesa nyingi sana. You brought it here to JF for one reason, which is to be discussed. Hivyo kaa chini fuatilia mjadala.
 

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
9,268
2,000
Utaratibu huu,sio kawaida na haijawahi kufanyika siku za nyuma.
Monduli wanahudhuria maofisa kutoka nchi zingine za afrika mfano namibia,Zimbabwe,Rwanda n.k.
Mazingira ya makazi ya mkuu wa nchi yanaanikwa kwa maofisa wanaohitimu kama wapo wanaotoka nchi za jirani.
Au kwa vile mji wa Arusha haujatilia(maana pale mwanasiasa wa upinzani aliona ndoto,ambayo imemfanya awekwe maabusu mpaka leo!)
Suala la kufanya shughuli hii sidhani kama imekuwa na majadiliano ya kutosha!
Keshokutwa mama anawapa kamisheni hapo Monduli, tunarudi kwenye utaratibu sasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom