Posho City
JF-Expert Member
- Mar 15, 2012
- 646
- 415
Kwanza nitoe warning kwamba hii tarehe mlonipa leo nikija mkanipa nyingine jua kabisa siku hiyo hatutaelewana maana hamna sababu za msingi zaidi ya uzembe....Meneja wa NSSF Ilala Boma sijui kama unajua na umekubaliana na hao maafisa wako wanaoandaa cheki za watu tunaojitoa...(fao la kujitoa)..
Mimi nilifungua madai tarehe 16.6.2016 wakanambia nije kuchukua cheki tarehe 30.6.2016...Bila kukosa tarehe hiyo nikaja lakini nikaambiwa cheki bado....Wenzangu waliochukua cheki siku hyo nilowauliza kama wanne wakanambia wao wamechukua baada ya kupigwa tarehe mara moja na wengine mara mbili...
Mimi siku hyo pia nilipigwa tarehe hadi 14.7.2016 na nilipouliza sababu nikaambiwa zipo nyingi lakini sikutajiwa hata moja....Leo nimerudi pale nikijua cheki tayari lakini nikaambiwa nirudi 22.7.2016 kisa cheki bado....Lakini nimeambiwa fomu nilijaza vizuri na michango yangu yote ipo....
Wakati naingia pale nimekutana na kaka mmoja yeye anasema anataka kumuona meneja maana kachoka na kupigwa tarehe...Pale mahali pa kusubiria cheki dada mmoja akaniambia yeye alikuja jana walipompiga tarehe hakukubaliana nao na alienda kwa meneja na cheki yake ikaandaliwa na leo kaichukua....
Pia huyu mama chumba namba 13 ana majibu ya ajabu....ukitaka kwenda kwa meneja anasema usiende kwa meneja na badala yake anakutuma kwa mdada anaitwa SIBAO ambao inaonekana washapanga maana hata huyu majibu yake ni ya ajabu...
Meneja wa tawi hili hebu kuwa mkali kidogo maana sisi wateja hii tabia inakera sana....vihela vyenyewe vidogo then vitupigishe jua kiasi hicho...
Ahsante leo mmeniweza ila tarehe 22.6.2016 hatutaelewana aisee.