Maafisa wa TAKUKURU waitangaza kampeni ya kupinga rushwa za barabarani bungeni

The Sheriff

Senior Member
Joined
Oct 10, 2019
Messages
143
Points
250

The Sheriff

Senior Member
Joined Oct 10, 2019
143 250
index.jpg

Pichani ni maafisa hao walioongozwa na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma - TAKUKURU, Joseph Mwaiswelo, wakiwa na Waziri Mkuchika pamoja na naibu waziri wake Dkt Mary Mwanjelwa.

Maafisa 53 wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU wameshiriki kikao cha bunge lengo likiwa ni kuitangaza kampeni ya ‘UTATU’ inayoshirikisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi pamoja na wadau katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa barabarani.

Maafisa hao walioongozwa na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TAKUKURU, Joseph Mwaiswelo, wakiwa na Waziri Mkuchika pamoja na Naibu Waziri wake Dkt Mary Mwanjelwa.

Kampeni hiyo ya ‘UTATU’ ni muunganiko wa pande Kuu tatu: TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau ambapo lengo lake kuu ni kuzuia rushwa za barabarani ambayo imebainika ni kisababishi kimojawapo cha ajali zinazotokea barabarani.

Kampeni hiyo imejiwekea mambo malengo mahususi manne, ikiwa kila lengo linatakiwa kutekelezwa na kila mdau kwa nafasi yake:
  • Kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa wasimamizi wa sheria za barabarani
  • Kuandaa mkakati wa kuzuia vitendo vya rushwa barabarani
  • Kushirikisha Umma kuzuia vitendo vya rushwa barabarani
  • Matumizi ya TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani
Pia soma:
 

Forum statistics

Threads 1,389,939
Members 528,059
Posts 34,039,264
Top