Maafisa wa Nigeria wamekamata mchele wa plastiki

mpuyango

Member
Aug 17, 2016
60
68
Maafisa wa Nigeria wamekamata mchele wa plastiki
1482321067443.jpg

Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.

Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".

Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".

Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.

Source: BBC Swahili
 
_93060903_raaaaaaaa.jpg

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemsha, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya wali wa kawaida

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".

Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".

Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hii ni hatari sana!! Wataalam wetu mipakani chukueni hatua maana kesho yaweza kuwa bongo!!!
 
Plastiki husababisha zaidi ya aina 50 ya saratani duniani. Hongereni sana Nigeria, afya ndo maisha.
 
TFDA na TBS hizi habari sasa chukueni hatua, mkikanusha nitamuomba Mh Rais awatoe kwa kutojali Afya zetu
 
Hatari sana, Naamini hatuko salama, kama mafuta feki ya kula yanaingia
 
Da huu mchele jamaa yangu alinitumia Clip jinsi unavyotengenezwa huko China,nikapuuzia kumbe usikute hata kwetu upo,tunaomba mamlaka husika fuatilieni tafadhali
 
Nilitumiwa video ikionyesha mchele huu unavyo tengenezwa duuuuh hatare sana aiseee tushaanza kufa tuu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom