Maafisa utumishi elimisheni watumishi wa umma kuhudu dressing codes.

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
Ni vyema watumishi wa umma wakaelimishwa ni nguo za namna gani wanapaswa kuzivaa pindi wanapokuwa maofisini.


Sawa kuna wengi wao wanafahamu nguo zipi zinaruhusiwa na zipi haziruhusiwi kwa mujibu wa kanuni zao za kiutumishi.

Lakini kuna watumishi ambao ni wageni maofisini na hawajui ni nguo zipi wanatakiwa kuzivaa wawapo ofisini.


Maafisa utumishi kazi yenu hiyo ya kuhakikisha mtumishi anafahamu vitu hivyo.


Na ni vyema pia wakafahamu nguo kama suti zinatakiwa kuvaliwa wakati gani au msimu gani.


Lakini pia tunaiomba Serikali yetu tukufu chini ya Rais wetu Dk john Joseph Pombe Magufuli kupitia wizara ya utumishi na or tamisemi kuendelea kutoa elimu kwa viongozi wapya ktk utumishi wa umma juu ya kanuni na taratibu za kiutumishi.


Maana sometimes ni aibu kuona kiongozi mkubwa kabisa anasimama kwenye umati na kutoa marufuku zisizokuwa na base.


Viongozi mliopewa dhamna na Rais wetu mjitahidi kuwaelimisha viongozi wapya hizo taratibu. Hazihitaji Rais ndio aelimishe. Rais ana kazi nyingi sana ndio maana aliwaamini kuwa mtamsaidia hizo kazi.


Mungu akulinde Rais wetu uendelee kuipambania nchi yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom