kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,888
Maafisa usalama 3 wa Palestina wauawa shahidi na jeshi la Israel na mwanajeshi mmoja wa Israel aangamizwa.
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limevamia mji wa Jenin ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuua shahidi maafisa usalama watatu wa Palestina.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Adham Yasser Eleiwi, 23, na Tayseer Ayasa, 32, ambao walikuwa maafisa wa Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Palestina wameuawa shahidi mapema leo baada ya askari katili wa Israel kushambulia mji wa Jenin.
Tovuti ya Kituo cha Habari cha Palestina imeripoti kuwa, Jamil Mahmoud al-Amouri, mwanachama wa Brigedi za Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihad Islami ameaga dunia pia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kufyatuliwa risasi na wanajeshi wa Israel katika uvamizi huo.
Duru za habari zinaarifu kuwa, mtafaruku ulianza baada ya wanajeshi katili wa Israel kujaribu kuwateka nyara Wapalestina nje ya Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Palestina katika barabara ya Nazareth mjini Jenin.
Askari wa Israel wanavyowateka nyara Wapalestina
Wakazi wa mji wa Jenin wamefanya maandamano ya kulaani shambulio na mauaji hayo ya kikatili yaliyotekelezwa na wanajeshi vamizi wa utawala haramu wa Israel.
Kwa mujibu wa shirika la habari la al-Jazeera, askari mmoja wa Kizayuni ameangamizwa katika makabiliano hayo ya mapema leo Alkhamisi mjini Jenin, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.