Maafisa usalama 3 wa Palestina na 1 wa Israel wauawa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,634
2,000
Maafisa usalama 3 wa Palestina wauawa shahidi na jeshi la Israel na mwanajeshi mmoja wa Israel aangamizwa.

Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limevamia mji wa Jenin ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuua shahidi maafisa usalama watatu wa Palestina.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Adham Yasser Eleiwi, 23, na Tayseer Ayasa, 32, ambao walikuwa maafisa wa Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Palestina wameuawa shahidi mapema leo baada ya askari katili wa Israel kushambulia mji wa Jenin.

Tovuti ya Kituo cha Habari cha Palestina imeripoti kuwa, Jamil Mahmoud al-Amouri, mwanachama wa Brigedi za Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihad Islami ameaga dunia pia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kufyatuliwa risasi na wanajeshi wa Israel katika uvamizi huo.

Duru za habari zinaarifu kuwa, mtafaruku ulianza baada ya wanajeshi katili wa Israel kujaribu kuwateka nyara Wapalestina nje ya Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Palestina katika barabara ya Nazareth mjini Jenin.

Askari wa Israel wanavyowateka nyara Wapalestina

Wakazi wa mji wa Jenin wamefanya maandamano ya kulaani shambulio na mauaji hayo ya kikatili yaliyotekelezwa na wanajeshi vamizi wa utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la al-Jazeera, askari mmoja wa Kizayuni ameangamizwa katika makabiliano hayo ya mapema leo Alkhamisi mjini Jenin, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

4by2d95a941d7f1vyb2_800C450.jpeg
 
Morogoro kaskazini

JF-Expert Member
Jul 5, 2020
443
1,000
Daah hawa waliuwa vibaya wamestukizwa sasa baada ya kufa ndipo mpalestina mmoja akaamua kuzichapa risasi na wanajesha wa israel ndipo mwanajeshi mmoja akafa wengine watatu walitelekeza silaha na kukimbia
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,955
2,000
Hii vita ya wapalestina na waisrael watu hawaielewi chanzo na sababu. Vitabu vitakatifu vimeandika kwamba vita hii haitakua na mwisho wala mshindi mpaka siku Yesu Kristo (Issa Bin Maryam) atakaposhuka.

Israel ni nchi iliozaliwa 14th May 1948, na ndio ikatambulika kuwa nchi, baada ya mwaka huo ndio ikaanza figisu za kutaka kuongeza ukubwa wa ardhi yao (Ardhi waliokua nayo ilikua ndogo) kwa kuwaondoa wapalestina katika ardhi yao. Israel ni nchi ambayo ina makundi mawili (Zionist na Jewish), Wazayuni (Zionist) ndio walioshika serikali ya Israel kuanzia 14th May 1948 mpaka sasa hivi na ndio wanaowaua wapalestina ili wachukue ardhi yao.

Muanzilishi wa itikadi, siasa na kitaifa (Ideology, Political Movement and Natiology) za kizayuni alikua Theodor Herlz, mnamo karne ya 19 (Tarehe 17/01/1896). Alikua mzaliwa wa Australia.

Kwa upande wa Majews (Jewish) hawana nguvu ndani ya serikali ya Israel, na hawawakubali wazayuni sambamba na kuamini kwamba wazayuni ni watu waliopotea njia na waliolaaniwa na mungu. Majews (Jews) wala hawaungi mkono hilo swala la mauwaji ya wapalestina na kudhulumu ardhi yao. Wao ni strictly Orthodox Jews Believers.

Cha kushangaza,

Bongo na africa watu wanafata mkumbo bila kujua uhalisia wa mambo, utasikia mpaka makanisani wahubiri (Wengine wanajiita Manabii na Mitume) wakiwaambia waumini wao wawaombee na wafunge kwaajili ya waisrael ili mungu awasaidie, huku wakiweka mpaka bendera za Israel kwenye magari na majumba yao. Hawajui kwamba wanajiingiza kwenye kundi la wazayuni (Zionist) - Wanawatetea Wazayuni.

Mwalimu Nyerere alikua mkristo kindaki ndaki, ila hakua miongoni mwa watu waliokua wakiwaunga mkono Israel kwasababu alikua anajua Israel inaendeshwa na Wazayuni sio wayahudi asilia. Na alikua anajua wazayuni ni watu wa aina gani. Na alipiga marufuku Israel kufungua hata ubalozi wao nchini Tanzania. Mwalimu hakua mjinga au mpumbavu kwasababu alikua akifuatilia kwa undani maswala ya nchi za wenzetu na migogoro yao.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,048
2,000
Hii vita ya wapalestina na waisrael watu hawaielewi chanzo na sababu. Vitabu vitakatifu vimeandika kwamba vita hii haitakua na mwisho wala mshindi mpaka siku Yesu Kristo (Issa Bin Maryam) atakaposhuka....
Mkuu Not Palestines Hiyo Ardhi waliishi wayahudi kutokana na Tawala eneo hilo Mtawala wa Mwisho ndio aliita Palestines Land na sio ya hao waarabu from Misri huko Gaza na Arabs huko West bank from Jordan na Syria... Eneo hilo lilivamiwa na waarabu wengi tu ndio hata Ottoman alilichukua kirahisi tu akalitawala hadi walipolichukua Waingereza na kuja kuwaachia watu wa asili yao Wayahudi na Wasamalia.

Raia wa Gaza hawana hata mfanano na Wafilist Filistines so usipotezwe na hayo maarabu from Misri ati ardhi yao kwanza hakukuwa na Taifa wanadai maeneo yao yanakaliwa wakati ardhi hiyo eneo kubwa lilikuwa ni Jangwa tu Waisrael ndio walibadilisha Gaza na Maeneo karibu yote ya jangwa na kuwa ardhi yenye rutuba na misitu yote Israel ni imetengenezwa kwa kampeni kubwa hayo Majinga hayana cha kudai chochote.

Kama Wakimbizi hawana nafasi sababu sio kwao na kama wajue walikataa ofa za UN na Ofa Za Israel kuishi pamoja side by side hadi leo hii hawataki Walileta vita ili kuwaua Waisrael wakashindwa na uwepo wao ni huruma tu za Israel kuacha adui aishi... Wayahudi katika nchi za arabuni walifukuzwa waende kuishi Israel na hilo lipo wazi..

So Mi naona wanaoshabikia Arabs za Gaza na West bank ni mazuzu wasiojua kitu... Ukifuatilia wafilisti mabaki yao ya DNA hayaendani hata na muarabu mmoja wa Nchini Israel Gaza na Westbank..

Kelele za Binadamu zikizidi waarabu watafukuzwa na mwapokee
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,694
2,000
Hii vita ya wapalestina na waisrael watu hawaielewi chanzo na sababu. Vitabu vitakatifu vimeandika kwamba vita hii haitakua na mwisho wala mshindi mpaka siku Yesu Kristo (Issa Bin Maryam) atakaposhuka...
Kwamba imeandikwa kwenye vitabu vya mungu vita yao haitasiha hadi Issa bin Maryam atakapo kuja halafu wewe huyo huyo tena unasema Israel imeanzishwa mwaka 1948? Vitabu vya dini vimeandikwa mwaka gani??? Unanichanganya bhana
 
NORTHERNIST

Senior Member
Feb 10, 2021
173
250
Mkuu Not Palestines Hiyo Ardhi waliishi wayahudi kutokana na Tawala eneo hilo Mtawala wa Mwisho ndio aliita Palestines Land na sio ya hao waarabu from Misri huko Gaza na Arabs huko West bank from Jordan na Syria... Eneo hilo lilivamiwa na waarabu wengi tu ndio hata Ottoman alilichukua kirahisi tu akalitawala hadi walipolichukua Waingereza na kuja kuwaachia watu wa asili yao Wayahudi na Wasamalia... Raia wa Gaza hawana hata mfanano na Wafilist Filistines so usipotezwe na hayo maarabu from Misri ati ardhi yao kwanza hakukuwa na Taifa wanadai maeneo yao yanakaliwa wakati ardhi hiyo eneo kubwa lilikuwa ni Jangwa tu Waisrael ndio walibadilisha Gaza na Maeneo karibu yote ya jangwa na kuwa ardhi yenye rutuba na misitu yote Israel ni imetengenezwa kwa kampeni kubwa hayo Majinga hayana cha kudai chochote...

Kama Wakimbizi hawana nafasi sababu sio kwao na kama wajue walikataa ofa za UN na Ofa Za Israel kuishi pamoja side by side hadi leo hii hawataki Walileta vita ili kuwaua Waisrael wakashindwa na uwepo wao ni huruma tu za Israel kuacha adui aishi... Wayahudi katika nchi za arabuni walifukuzwa waende kuishi Israel na hilo lipo wazi..

So Mi naona wanaoshabikia Arabs za Gaza na West bank ni mazuzu wasiojua kitu... Ukifuatilia wafilisti mabaki yao ya DNA hayaendani hata na muarabu mmoja wa Nchini Israel Gaza na Westbank..

Kelele za Binadamu zikizidi waarabu watafukuzwa na mwapokee
Umeelezea vyema
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,955
2,000
KWamba imeandikwa kwenye vitabu vya mungu vita yao haitasiha hadi ISaa bi Maryam atakapo kuja halafu wewe huyo huyo tena unasema Israel imeanzishwa mwaka 1948? Vitabu vya dini vimeandikwa mwaka gani??? Unanichanganya bhana
Unajua maana ya "NCHI"??? Kabla ya hapo kulikua hakuna nchi kama nchi iliokua ikitambulika kama Israel. Mfano, hakuna nchi inaitwa Zanzibar, japo kuna watu wanaitwa wazanzibari, zanzibar ni visiwa ndani ya nchi ya Tanzania, kwasababu bado haijatambulika kama nchi.
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,694
2,000
Unajua maana ya "NCHI"??? Kabla ya hapo kulikua hakuna nchi kama nchi iliokua ikitambulika kama Israel. Mfano, hakuna nchi inaitwa Zanzibar, japo kuna watu wanaitwa wazanzibari, zanzibar ni visiwa ndani ya nchi ya Tanzania, kwasababu bado haijatambulika kama nchi.
Hili suala la Israel linatuchanganya sana wengi, hata nyie mnao onesha kama mnalifahamu bado hua hamjibu maswali ya wachangiajie wengi kama ulivyo jichanganya mwanzoni. Kuna mtu aliwahi kuuliza hivi, "kama Israel imeanza kua taifa/nchi mwaka 1948 then tajeni walau wafalme wa Palestina 5 kabla ya huo mwaka; can you do it brother!?
 
MZEE CHAKA

Member
May 27, 2021
16
45
AHSANTE KWA MAANDIKO YAKO. HATA NAMI HAPO SIKUWEZA KUWATOFAUTISHA KWA UKAMILIFU HAWA WAZAYUNI NA MAYAHUDI. LEO NIMENG'AMUA KITU. AHZENTE
 
inspectorbenja

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
225
250
Hii vita ya wapalestina na waisrael watu hawaielewi chanzo na sababu. Vitabu vitakatifu vimeandika kwamba vita hii haitakua na mwisho wala mshindi mpaka siku Yesu Kristo (Issa Bin Maryam) atakaposhuka.

Israel ni nchi iliozaliwa 14th May 1948, na ndio ikatambulika kuwa nchi, baada ya mwaka huo ndio ikaanza figisu za kutaka kuongeza ukubwa wa ardhi yao (Ardhi waliokua nayo ilikua ndogo) kwa kuwaondoa wapalestina katika ardhi yao. Israel ni nchi ambayo ina makundi mawili (Zionist na Jewish), Wazayuni (Zionist) ndio walioshika serikali ya Israel kuanzia 14th May 1948 mpaka sasa hivi na ndio wanaowaua wapalestina ili wachukue ardhi yao.

Muanzilishi wa itikadi, siasa na kitaifa (Ideology, Political Movement and Natiology) za kizayuni alikua Theodor Herlz, mnamo karne ya 19 (Tarehe 17/01/1896). Alikua mzaliwa wa Australia.

Kwa upande wa Majews (Jewish) hawana nguvu ndani ya serikali ya Israel, na hawawakubali wazayuni sambamba na kuamini kwamba wazayuni ni watu waliopotea njia na waliolaaniwa na mungu. Majews (Jews) wala hawaungi mkono hilo swala la mauwaji ya wapalestina na kudhulumu ardhi yao. Wao ni strictly Orthodox Jews Believers.

Cha kushangaza,

Bongo na africa watu wanafata mkumbo bila kujua uhalisia wa mambo, utasikia mpaka makanisani wahubiri (Wengine wanajiita Manabii na Mitume) wakiwaambia waumini wao wawaombee na wafunge kwaajili ya waisrael ili mungu awasaidie, huku wakiweka mpaka bendera za Israel kwenye magari na majumba yao. Hawajui kwamba wanajiingiza kwenye kundi la wazayuni (Zionist) - Wanawatetea Wazayuni.

Mwalimu Nyerere alikua mkristo kindaki ndaki, ila hakua miongoni mwa watu waliokua wakiwaunga mkono Israel kwasababu alikua anajua Israel inaendeshwa na Wazayuni sio wayahudi asilia. Na alikua anajua wazayuni ni watu wa aina gani. Na alipiga marufuku Israel kufungua hata ubalozi wao nchini Tanzania. Mwalimu hakua mjinga au mpumbavu kwasababu alikua akifuatilia kwa undani maswala ya nchi za wenzetu na migogoro yao.
Unadhani unajua sana kuhusu mgogoro wa mashariki ya kati kumbe unafahamu kwa juu juu tu.Alaf unadhani Makanisa na wahubiri wanaoiunga mkono Israel ni kama mambumbumbu tu,ukifika apo unajiona wewe nfo unajua sana.Kumbe ndo kwanza upo chekechea kwenye mgogoro wa mashariki ya kati
Mgogoro huu una pande tatu kisiasa,kidini(kiimani) na kichumi.
1.Jambo la kwanza kabisa ambalo halizungumziwi sana kwenye medani za kisiasa ni suala la dini.
Itandelea.........
 
Randy orton

JF-Expert Member
Apr 29, 2019
369
1,000
Hii vita ya wapalestina na waisrael watu hawaielewi chanzo na sababu. Vitabu vitakatifu vimeandika kwamba vita hii haitakua na mwisho wala mshindi mpaka siku Yesu Kristo (Issa Bin Maryam) atakaposhuka.

Israel ni nchi iliozaliwa 14th May 1948, na ndio ikatambulika kuwa nchi, baada ya mwaka huo ndio ikaanza figisu za kutaka kuongeza ukubwa wa ardhi yao (Ardhi waliokua nayo ilikua ndogo) kwa kuwaondoa wapalestina katika ardhi yao. Israel ni nchi ambayo ina makundi mawili (Zionist na Jewish), Wazayuni (Zionist) ndio walioshika serikali ya Israel kuanzia 14th May 1948 mpaka sasa hivi na ndio wanaowaua wapalestina ili wachukue ardhi yao.

Muanzilishi wa itikadi, siasa na kitaifa (Ideology, Political Movement and Natiology) za kizayuni alikua Theodor Herlz, mnamo karne ya 19 (Tarehe 17/01/1896). Alikua mzaliwa wa Australia.

Kwa upande wa Majews (Jewish) hawana nguvu ndani ya serikali ya Israel, na hawawakubali wazayuni sambamba na kuamini kwamba wazayuni ni watu waliopotea njia na waliolaaniwa na mungu. Majews (Jews) wala hawaungi mkono hilo swala la mauwaji ya wapalestina na kudhulumu ardhi yao. Wao ni strictly Orthodox Jews Believers.

Cha kushangaza,

Bongo na africa watu wanafata mkumbo bila kujua uhalisia wa mambo, utasikia mpaka makanisani wahubiri (Wengine wanajiita Manabii na Mitume) wakiwaambia waumini wao wawaombee na wafunge kwaajili ya waisrael ili mungu awasaidie, huku wakiweka mpaka bendera za Israel kwenye magari na majumba yao. Hawajui kwamba wanajiingiza kwenye kundi la wazayuni (Zionist) - Wanawatetea Wazayuni.

Mwalimu Nyerere alikua mkristo kindaki ndaki, ila hakua miongoni mwa watu waliokua wakiwaunga mkono Israel kwasababu alikua anajua Israel inaendeshwa na Wazayuni sio wayahudi asilia. Na alikua anajua wazayuni ni watu wa aina gani. Na alipiga marufuku Israel kufungua hata ubalozi wao nchini Tanzania. Mwalimu hakua mjinga au mpumbavu kwasababu alikua akifuatilia kwa undani maswala ya nchi za wenzetu na migogoro yao.
Yesu sio Issa...

Huyo Issa hajasulubiwa wala hajazaliwa kwenye hori la ng'ombe.
 
cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
19,344
2,000
Kila siku nasema wanaume handsome wasiwe wanajeshi, kama hapo wakaka wazuri wanekatishwa uhai wao, aaaah.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom