Maafisa Maliasili wawili wauawa na wafugaji Kasulu

ngonani

JF-Expert Member
Aug 27, 2012
1,366
597
Tukio limetokea jana jioni katika pori la hifadhi Mvugwe wilayani Kasulu,baada ya maafisa hao kwenda kwenye operation ya kukamata wafugaji, jumla walikuwa 9, wawili wameuawa na majeruhi wanne.

Chanzo: Mimi mwenyewe
 
Safi naamini watanzania wanazidi kuchoka na kuwa majasiri.
 
unajua kwa kuanzia uchunguzi ni vyema wewe kuisaidia polisi kwasababu kuuawa watumishi wa serikali katika kutekeleza majukumu yao unaona waliofanya hivyo ni majasili kaa mkao wa kula.kuunga mkono waliofanya makosa hasa ya kuua ina maana na wewe ni muhusika
 
Safi naamini watanzania wanazidi kuchoka na kuwa majasiri.
Wewe ni pumba kabisa,we unaona watu kujichukulia sheria kwa kuua watendaji wanaotimiza majukumu yao ni sahihi?huu utamaduni wa watu kutoheshimu mamlaka ni lazima ukomeshwe mara moja vinginevyo nchi itakwenda pabaya.I hope polisi watachukua hatua stahiki na kuhakikisha wote waliohusika wanasombwa na sheria ichukue mkondo wake.Wanajamvi tuache kushabikia uhuni,supposed ni mwanao ndio kaanza kazi mwaka huu na yanamkumba au nduguyo au mtu wa karibu na wewe ungeshabikia upuuzi huu?
 
Tukio limetokea jana jioni katika pori la hifadhi mvugwe wilayani Kasulu,baada ya maafisa hao kwenda kwenye operation ya kukamata wafugaji,jumla walikuwa 9,wawili wameuwawa na majeruhi wanne.Chanzo mimi mwenyewe

Hebu leta taarifa vizuri haijakaa vizuri, ni wafugaji kutoka wapi? Rwandwa au geita, shy ....?

Kuna jambo serikali haijaritambua kwenye hili swala la mifugo: siku moja nilipata siri kutoka kwa mfugaji mmoja msukuma alinieleza yafuatayo: yeye anamiliki Ng'ombe zaidi ya 8,000 waliogawanywa katika maeneo kadhaa nchini kama ifuatavyo. GEITA zaidi ya Ng'ombe 3000, MVUHA MKOANI MOROGORO zaidi ya ngombe 600, Kilosa Mkoani Morogoro 500 Kigoma 2000, TABORA wilaya ya urambo na kariua 800, Rwanda 400, na wengine kidogo wapo UGANDA-kwa wanyankole.

Lakini alinambia kuwa baada ya serikali kufanya msako maarufu kama operesheni tokomeza, wafugaji wa Rwanda waliondoka na kurudi kwao lkn kwa sababu ya uhaba wa malisho waliamua kurudisha mifugo kwa style nyingine ya kuwapa mifugo watanzania hasa wasukuma na kulipwa ujira wa Ng'ombe 2 kila baada ya miezi 6, mchungaji hukabidhiwa ng'ombe wasiopungua 300, kulingana na sehemu ya malisho.

Hivyo basi serikali inaweza kuwaonea huruma wafugaji kuwa ni watanzania kumbe siyo hibyo bali ni watanzania wanaochunga makundi ya ng'ombe kutoka nje ya Tanzania.
 
Umenifanya nimkumbuke sana Marehemu Christopher Mtikila..mungu amrehemu!
 
Hawa wafugaji wanaolisha mifugo katika hifadhi wanavunja sheria na wanaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa. Tatizo ni approach zinazotumika kuwakabili, na kibaya zaidi uchaguzi uliopita unatengeneza pengo kubwa sana kati ya maneno yanayosemwa na serikali pamoja na matakwa halisi ya wananchi ambao ndio watawaliwa lakini wakati huo huo ndio waajiri wa wanasiasa.
Mfano unadhani kilichotokea kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa madiwani Kilombero au Dar es salaam na meya kineweza kujenga kuaminiana kati ya wapiga kura na viongozi!? Matokeo yake ni watu kuishia kujichukulia sheria mikononi ili waweze kusurvive na ikiendelea hivi matokeo yake ni mabaya sana.
 
Hebu leta taarifa vizuri haijakaa vizuri, ni wafugaji kutoka wapi? Rwandwa au geita, shy ....?

Kuna jambo serikali haijaritambua kwenye hili swala la mifugo: siku moja nilipata siri kutoka kwa mfugaji mmoja msukuma alinieleza yafuatayo: yeye anamiliki Ng'ombe zaidi ya 8,000 waliogawanywa katika maeneo kadhaa nchini kama ifuatavyo. GEITA zaidi ya Ng'ombe 3000, MVUHA MKOANI MOROGORO zaidi ya ngombe 600, Kilosa Mkoani Morogoro 500 Kigoma 2000, TABORA wilaya ya urambo na kariua 800, Rwanda 400, na wengine kidogo wapo UGANDA-kwa wanyankole.

Lakini alinambia kuwa baada ya serikali kufanya msako maarufu kama operesheni tokomeza, wafugaji wa Rwanda waliondoka na kurudi kwao lkn kwa sababu ya uhaba wa malisho waliamua kurudisha mifugo kwa style nyingine ya kuwapa mifugo watanzania hasa wasukuma na kulipwa ujira wa Ng'ombe 2 kila baada ya miezi 6, mchungaji hukabidhiwa ng'ombe wasiopungua 300, kulingana na sehemu ya malisho.

Hivyo basi serikali inaweza kuwaonea huruma wafugaji kuwa ni watanzania kumbe siyo hibyo bali ni watanzania wanaochunga makundi ya ng'ombe kutoka nje ya Tanzania.
Ilo eneo asilimia kubwa kama sio yote ni ng'ombe wa wasukuma na kuna vijiji informal vya wasukuma vimeanza kuchipuka maeneo hayo
 
Hili swala serikali ikilichukulia poa litaleta maafa makubwa sana ktk nchi hii, kwa sababu wafugaji wameharibu uoto wa asili sehemu wanazofuga kwa muda mrefu, matokeo yake ni kwamba maeneo ya marisho hayapo tena, hivyo wafugaji wanasambaa kila kona ya nchi na kuharibu uoto wa asili, hasa wanashuka kutoka kanda ya ziwa kwenda magharibi na kusini mwa mchi. Ukienda Rukwa, Katavi, Mbeya, Morogoro, Lindi tatizo ni hilo hilo. bahati mbaya wanasabaisha vifo na uharibifu wa mazao.
 
kwanini uwa mnapinga tu hata vitu vilivyo obvious?mmoja alifia kwenye tukio na wa pili kafia hospitali.Kama una jamaa yako anafanya mrotuary muulize kama hiyo miili haikuhifadhiwa hapo.
Sio jamaa Mimi nipo hapa mvugwe hakuna kitu kama hicho.
 
Wewe ni pumba kabisa,we unaona watu kujichukulia sheria kwa kuua watendaji wanaotimiza majukumu yao ni sahihi?huu utamaduni wa watu kutoheshimu mamlaka ni lazima ukomeshwe mara moja vinginevyo nchi itakwenda pabaya.I hope polisi watachukua hatua stahiki na kuhakikisha wote waliohusika wanasombwa na sheria ichukue mkondo wake.Wanajamvi tuache kushabikia uhuni,supposed ni mwanao ndio kaanza kazi mwaka huu na yanamkumba au nduguyo au mtu wa karibu na wewe ungeshabikia upuuzi huu?
kwahiyo samaki akila mtu kosa ila mtu akila samaki ni sawa,tabia za maafisa waserikali ni zakinyanyasaji sana hasa huko kwa watu ambao hawajaenda shule,mnataka kujifanya hamuoni maonezi ya polisi kwa raia au kwasababu nyie mnalindwa na system
 
Back
Top Bottom