Maafisa Magereza wadaiwa kumtorosha mahabusu ...............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,712
2,000
Maafisa Magereza wadaiwa kumtorosha mahabusu
Saturday, 04 December 2010 22:44

Na Frederick Katulanda, Mwanza

JESHI la magereza wilayani Magu mkoani Mwanza limeingia katika kashfa baada ya maofisa wake kudaiwa kuhusika katika mpango wa kumtorosha mahabusu mmoja ambaye aliyakuwa akituhumiwa kwa kesi ya mauaji.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mpango wa kumtorosha mtuhumiwa huyo ulibuniwa na maofisa wa ngazi za juu wa gereza hilo la wilaya baada ya kupokea fedha nyingi kutoka kwa ndugu wa mtuhumiwa huyo na kuandaa mpango huo ambao hatmaye ulifanikiwa na mtuhumiwa huyo(jina tunalo) alitoroka Julai 15, mwaka huu.

Kutokana na kutoroka kwa mtuhumiwa huyo Jeshi la Magereza liliwatimua kazi askari wake sita ngazi za chini wakidaiwa kuhusika na mpango huo baada ya maelezo yao waliyotoa kwa timu ya uchunguzi wa mkoa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Askari ambao wamefukuzwa kazi ni B 4186 WDR Felisian aliyekuwa mlinzi wa malango, B. 3147 WDR Hamis Hassan, B. 6001 WDR Raymond waliokuwa walinzi wa kibanda cha zamu na WDR. Zephania, CPL Busoga aliyekuwa NCO wa zamu siku hiyo.
Mkuu wa Gereza Mkoa wa Mwanza, (RPO)Elisha Molleli alipoulizwa kwa njia ya simu alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa katika hatua ya awali jeshi hilo liliwafukuza kazi askari wote waliokuwa zamu suku kwa vile walihusika na uzembe.

“Tuliwafukuza askari wote sita waliokuwa zamu usiku huo, tumemfukuza hadi aliyekuwa mlangoni, askari waliitwa na mahabusu lakini hawakuweza kufika kutokana na kuwa wamelala. Tumeongea nao na tumeongea na mahabusu na tumefanya ukaguzi katika gereza hilo,” alieleza Mkuu huyo wa Gereza.

Aidha alikanusha kuwepo kwa madai ya kutokuwa na ulinzi upande wan je ya gome ambako Selo ambayo mahabusu huyo alitorekea na kusema katika rosta ya zamu za ulinzi walinzi hao walikuwepo lakini walikuwa wamelala bila kufafanua waliuwa upande gani.

“Siyo kweli kuwa kuna maelezo ya askari yamepotea, lakini nieleze tu kuwa kulikuwa na ulinzi na mkuu wa gereza alitimiza wajibu wake na kupanga walinzi katika zamu, wamefanya uzembe ni wao na tumewatimua kazi,” alisisitiza Mollel bila ya kufafanua zaidi.

Mkuu wa Mereza wa Wilaya Magu, SSP Chipanso alipotakiwa kutoa maelezo kuhusina na tukio hilo alisema masuala yoteya gereza yanapaswa kutolewa maelezo Mkuu wa Gereza wa Mkoa.


Inadaiwa kuwa baada ya vigogo hao wa magereza kusuka mpango huo waliandaa mkakati wao kuhakikisha mtuhumiwa huyo atoroke katika gereza hilo kupitia juu ya bati ambako hakuna misumari.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo siku ya kutoroka kupitia kwenye sehemu hiyo ambayo paa isyo na misumari ambayo inaelezwa kuwa iliondolewa katika kufanikisha mpango huo.

Tukio hilo lilitokea saa 6:15 usiku baada ya mtuhumiwa huyo kuingia ndani ya choo ya selo namba namba moja na kupanda darini na kisha kutoweka kusikojulikana.

Habari zaidi zinaeleza kuwa kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa huyo, baadhi ya mahabusu ambao walikuwa ndani ya selo hiyo walipiga kelele na kugonga kwa nguvu, ambazo zilimfikia mlinzi wa zamu wa mlango mkuu (Ob-keeper) ambaye alifika katika selo hiyo na baada ya kueleza kuwa kulikuwa na mahabusu aliyepanda juu ya paa na kutoroka kwa nje ya ngome, alipiga filimbi kutoa tarifa kwa walinzi wenzake.

Kufuatia tukio hilo asubuhi ya siku iliyofuata timu ya maofisa wa Gereza la Mkoa ACP, Elisha Molleli na ASP Mayunga ambaye ni afisa upelelezi mkuu wa magereza mkoa, walifika kutembela eneo la tukio na gereza pamoja na kufanya mahojiano na askari waliokuwa zamu za ulinzi wakati wa tukio hilo.

Baada ya ukaguzi huo timu hiyo ya mkoa ilitoa taarifa ambayo ilieleza kasoro za ndani na zile za uongozi zilizosababisha kutoroka kwa mahabusu huyo.

Udhaifu wa kwanza ni kutofanyiwa kwa ukarabati wa selo zote nne za gereza hilo ambapo mkuu wa magereza na wasaidizi wake walishuhudia eneo ambalo mtuhumiwa alipitia kutorokea lilikuwa halina misumari sehemu mabati yalipounganishwa.

Pili ni kutopangwa ama kutokuwapo kwa mlinzi eneo la upande ambako mtuhumiwa alitorokea, tatu ni kuwa ndani ya selo hiyo ambako mtuhumiwa aliingia na kisha kupanda ndani ya paa hakukuwa na taa kwa muda mrefu.

Kasoro nyingine ambayo iligunduliwa na timu hiyo ni askari wanaokuwa katika kibanda kupangwa katika lindo hilo usiku bila ya kuwa na silaha, jambo ambalo limesababisha walinzi hao kumwona mtuhumiwa akikimbia wakashindwa kudhibiti.

Kutokana na sababu hizo zilitodaiwa kutokana na uzembe wa maofisa wa juu wa gereza, ambazo zilizobainishwa na timu hiyo ya Magereza mkoa, mkuu wa magereza mkoa aliagiza kufanyika kwa mabadiliko ya ulinzi haraka na kwamba askari wa usiku walianza kulinda na silaha, kulijengwa kibanda cha ulinzi upande wa eneo ambako mahabusu alitoroka.

Vile vile, selo zote zilifanyiwa ukarabati pamoja na kuweka taa ndani ya choo alichopia kutorokea matuhumiwa na zingine zilizokuwa giza.

Imeelezwa kuwa kutokana na taarifa hiyo hali ilikuwa mbaya kwa maafisa wa gereza hilo kutokana na askari wa zamu kumwaga taarifa za kina kuhusu udhaifu wa uongozi ambayo yalitumwa mkoani na kisha kutumwa makao makuu ya gereza.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa taarifa hiyo mpaka sasa imeshindwa kufanyiwa kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom