Maafisa ardhi Sumbawanga acheni kusababisha baina ya wamiliki halali na wavamizi

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika katika wizara zilizoshindika ni pamoja na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi bora wizara ikahamia ofisi ya rais labda watendaji wake wataheshimu sheria.

Maafisa ardhi Manispaa ya Sumbawanga wamekuwa wanachochochea migogoro ya ardhi baina ya wamiliki halali wenye hati milki za muda mrefu (title deed) na watu wanadai eti hivyo viwanja vipo kwenye mashamba yao.

Mwaka 2004 manispaa iliyatwaa mashamba hayo na kuwalipa fidia wahusika na ushahidi upo kwenye majedwali ya fidia ofisi ya mkuu wa wilaya. Badala ya maafisa ardhi kujihakiki kupitia majedwali hayo ili kujua kama kweli hao ndio wenye hayo mashamba na hawakulipwa fidia wao wamekuwa wanatoa barua za kuwaruhusu kuviendeleza viwanja kwa hao watu huku wakijua wamiliki wa viwanha hivyo wapo na wana hati za muda mrefu (title deed) zilizoandaliwa na maafisa ardhi hao hao wa manispaa.

Kama hao wanaodai fidia walisahaulika wakati wa ulipaji fidia mwaka 2004 manispaa inapaswa itafute fedha za kuwalipa na sio kuwanyang'anya viwanja wamiliki halali. Sasa hivi wamiliki wapo waliopeleka kesi mahakamani kupinga utaratibu huu wa kuwanyang'anya viwanja vyao.

Tunamwomba waziri mwenye dhamana asitishe utaratibu huu isiyofuata sheria na kuisababishia serikali hasara.
 
Wizara hii ni kati ya wizara zilizoshindikana kabisa
Utapeli mwingi na rushwa iliyokithiri
Na hakuna wa kuwafanya kitu
 
Back
Top Bottom