Maafa yatokea Mgodi wa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu Sekenke/Mgongo, Iramba - Singida

S2dak_Jr

Senior Member
Jul 15, 2012
198
45
Wanajamvi;

Kama mtakumbuka, hapo nyuma nilikuwa nawaletea mabandiko yanayohusu mgogoro wa eneo la uchimbaji mdogo wa dhahabu.

Mgogoro huu mpaka sasa upo mahakamani na maamuzi bado hayajatolewa ila Wachimbaji wadogo walishafukuzwa chini ya Polisi Mkoa na Wilaya. Na mpaka sasa upande wa pili katika kesi hiyo wameshakabidhiwa eneo hilo na kuweka uzio na kuanza kazi za uchimbaji bila ya kesi ya msingi kuamuliwa na mahakama.

Eneo hilo sasa lina ulinzi mkali wa askari wasiopungua kumi. Sasa sijajua kama wawekezaji wa kampuni ya JOKA Mines ambao ni John Bina na ndugu Kabua wana makubaliano gani na Polisi hao.

Nirudi kwenye mada ya msingi:

Ilipofikia asubuhi ya leo kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa kuna watu wamefariki ndani ya mashimo yaliyomo ndani uzio wa eneo linalochimbwa na wawekezaji hao, ila tukio hili linafanywa ni siri ya kampuni.

Baada ya watu kudadisi sana, taarifa zilizidi kutoka kuwa mtu mmoja amefariki na mwili wake upo Hospitali ya Wilaya ya Iramba - Kiomboi.

Taarifa zilizotolewa ni kuwa kifo hicho kimesababishwa na ukosefu wa hewa kwenye mashimo hayo. Pia kuna taarifa kuwa kifo hicho kimesababishwa na kupondwa na mawe yaliyoporomoka ndani ya shimo hilo.

Pia kutokana na usiri mkubwa wa utoaji wa taarifa kutoka ndani ya eneo hilo, wapo wanaotoka na kusema waliofariki ni wawili na wengine wakisema ni saba. Kila mtu anatoka na taarifa yake.

Katika hatua nyingine, wapo pia wanaolihusisha tukio hili na mambo ya kishirikina. Hii inatokana na hasira za wale waliofukuzwa eneo hilo kuzunguuka na kujigamba kuwa hiyo ni kazi ya WAGANGA wao. Mimi siamini katika nadharia hii, sijui ninyi wenzangu.

Nawasilisha.
 
Wanajamvi; Kama mtakumbuka, hapo nyuma nilikuwa nawaletea mabandiko yanayohusu mgogoro wa eneo la uchimbaji mdogo wa dhahabu. Mgogoro huu mpaka sasa upo mahakamani na maamuzi bado hayajatolewa ila Wachimbaji wadogo walishafukuzwa chini ya Polisi Mkoa na Wilaya. Na mpaka sasa upande wa pili katika kesi hiyo wameshakabidhiwa eneo hilo na kuweka uzio na kuanza kazi za uchimbaji bila ya kesi ya msingi kuamuliwa na mahakama. Eneo hilo sasa lina ulinzi mkali wa askari wasiopungua kumi. Sasa sijajua kama wawekezaji wa kampuni ya JOKA Mines ambao ni John Bina na ndugu Kabua wana makubaliano gani na Polisi hao. Nirudi kwenye mada ya msingi: Ilipofikia asubuhi ya leo kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa kuna watu wamefariki ndani ya mashimo yaliyomo ndani uzio wa eneo linalochimbwa na wawekezaji hao, ila tukio hili linafanywa ni siri ya kampuni. Baada ya watu kudadisi sana, taarifa zilizidi kutoka kuwa mtu mmoja amefariki na mwili wake upo Hospitali ya Wilaya ya Iramba - Kiombo.sijaelewa.
 
We si umesikia kauli iliyotolewa juu ya ishu ya mtwara na uchimbaji wa Uranium. Binafsi sina cha kuhoji
 
Back
Top Bottom