Maafa ya mafuriko Tanga yaliyoacha maumivu yenye makovu ya milele

Wahaya huwa wana utamaduni flani japo sijuhi kama bado wnaufuta : watu wa familia moja kama ndugu, nk huwa hawavuki kwa kutumia mtumbwi mmoja hata kama una uwezo wa kuwabeba wote, inabidi wavushwe kwa awamu! Hili la familia moja kusafiri kwa chombo kimoja cha usafiri mimi sitakaa nilifanye...
 
Mkuu alipangalo MUNGU hamna binadamu awezaye kuliepusha! Yalio tokea ndio ulikuwa mpango wake MUNGU na kwake halina makosa
tunashauriwaga mkiwa ndugu kusafiri wote kwenye usafiri mmoja sio vyema ni basi tu kuna vitu tunavionaga vidogo lakini si vidogo, maana hakuna ajuaye kesho.
 
Kama unafikiri umepatwa na mitihani mikubwa mfikirie huyu mwanafunzi wangu...

Ni msichana wa kidato cha nne ambaye wiki ijayo anaanza mitihani ya kumaliza kidato cha nne ila sio mitihani hiyo ninayotaka kuwaeleza...

Juzi jumamosi ilikuwa graduation yao.Hivyo alitarajia wazazi wake wanakuja.Na alipigiwa simu kwamba safari imeanza tunakuja.

Lahaula.Graduation imeanza mpaka imeisha haoni wazazi waliosema wanakuja.Anaomba simu kuwapigia hawapatikani.Giza linaingia bado hawapatikani wala hawafiki.ANALIA.

Baadhi ya waalimu,wanafunzi wenzake na wageni waliokuja kwenye graduation wanambembeleza.Wanamuambia "nyamaza usilie kuna dharura kwenye maisha ni kawaida."Sherehe inaisha watu wanatawanyika.

Kesho yake anataka tena wazazi wapigiwe simu waulizwe kulikoni?Simu zote hazipatikani.

Jioni tena inafika.Simu inapigwa kutoka Dar.Waliopiga wanaulizia kama wazazi wa mwanafunzi (huyu tunayemzungumzia)walifika jana maana na wao wanawapigia hawapatikani na hawajarudi!!??

Ndipo ufuatiliaji kutoka pande zote unafanyika.Ukweli unafahamika.Ni ukweli mchungu.Lakini ndio ukweli.Wazazi wa mwanafunzi wetu huyu wakiwa na familia nzima ndani ya gari maeneo ya Tanga daraja lilipoharibiwa na mafuriko walizama kwenye maji na gari yao.Wamefariki wote watano.Baba mama dada wawili na mdogo wake wa miezi kadhaa.

Mpaka sasa mwili wa mtoto mdogo bado haujapatikana.Miili ya wengine imepatikana ikiwa imeharibika vibaya.

Usiku huu wanazikwa Dar es salaam.Wameharibika sana hawatangoja kesho.

Mwanafunzi wetu hatumuambii.Afanye mitihani ya form four kwanza.akimaliza anarudi nyumbani kukutana na mitihani migumu zaidi baadhi ya walimu wanataka aambiwe wengine ndio tunasema hapana aachwe amalize mitihani....
IMG-20191030-WA0066.jpeg
 
Najaribu kuvaa uhusika wa huyo mtoto aliyefiwa na wazazi/ndugu zake/familia hakika nashindwa kwa kweli maana si kwa maumivu hayo.

WAPUMUZIKE KWA AMANI WAPENDWA WETU
 
Back
Top Bottom