Maafa ya mafuriko Tanga yaliyoacha maumivu yenye makovu ya milele

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
138,438
2,000
Kama unafikiri unapitia mitihani migumu na mapito magumu sana hapa duniani basi vaa viatu vya mtoto huyu umshukuru Mungu kwa hapo ulipo na usonge mbele.

Jumamosi iliyopita ilikuwa graduation yake ya form 4 na wazazi wake baba, mama, dada zake wawili na mdogo wao mchanga walikuwa kwenye gari yao kuelekea kwenye graduation ya mtoto wao.

Walipofika Tanga daraja lilisombwa na mafuriko na wote wakafa palepale hadi sasa mtoto mchanga hajapatikana, aliwasubiri sana hadi graduation inaisha lakini hawakutokea.

Mtoto huyu wa kidato cha nne wazazi wake na ndugu zake watazikwa wote na yeye hatoambiwa ili aweze kufanya mitihani yake week ijayo na atakapomaliza mitihani yake ya form four atarudi nyumbani kukabiliana na mtihani huu mkubwa kwani atakuta nyumba haina mtu zaidi sana atakutana na kaburi la baba, mama, dada zake na mdogo wake na atakuwa amebaki yeye na Mungu wake. Mungu amsaidie sana kwani mzigo huu ni mzito.

Maisha ni safari na mwisho wa safari ni popote pale tuache kuumizana au kuchukiana kwa ajili ya vitu vya duniani tuombeane tukijua kila kitu kina mwanzo na mwisho na yote tutayaacha duniani hapa hakuna tutakachoenda nacho.

Mungu awapokee

Post hii ni kwa niaba ya mtandao wa WhatsApp. Mwandishi hajaweka jina lake. Nimeiweka hapa tujifunze na kuona maumivu ya wengine.

IMG-20191030-WA0088.jpeg
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
2,904
2,000
Mkuu hii ndo ile ajali ya noah iliyoua watu 8(ambaao wakubwa) na watoto 2?
 
Top Bottom