Maafa mvua DSM, Nani alaumiwe Serikali au wakazi wa mabondeni??

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Poleni sana ndugu zangu wa DSM kwa athari zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. Nimekuwa nikifwatilia wasemaji mbalimbali ktk vyombo vya habari na kubaini kuwa wengi wa wazungumzaji hasa viongozi wa serikali, wameendelea kutupia lawama wakaazi wa mabondeni. Nionavyo mimi kwa mvua hizi hata wakazi wa vichuguuni nao wamepata madhara makubwa kama yaliyowapata wale wa mabondeni. Hivyo kitendo cha serikali kutupia lawama wakazi wa mabondeni badala ya kuangalia tatizo hili kwa upana wake mimi naona si sawa hata kidogo.
  • Nionavyo mimi kituo cha mamlaka ya hali ya hewa hakikuwaandaa watu vya kutosha kuhusu expected impacts za mvua hizi. Hii inatokana na kufanya kazi kwa mazoea, tushazoea kusikia "ukanda wa pwani maeneo ya mkoa wa DSM na Pwani kutakuwa na mvua kiasi na ngurumo za hapa na pale".Anayebisha akaangalie taarifa za mamlaka ya hali ya hewa siku moja kabla mvua kubwa ya juz haijaanza kunyesha. Rais naye alishawahi kulisema hili wkt wa ujio wa kwanza wa Bush, I dont know how far He went in rectifying the situation.
  • Miundombinu yetu hasa drainage structures haipo sawa na haifanyiwi maintainance ya kutosha, hili linaenda sambamba na wenye fedha kujenga majumba yao kwenye mitaro/mapito ya maji au kufunga kabisa mitaa na njia za maji. Matokeo yake maji yanakosa pa kupita na hivyo kuvamia majumba ya watu. Hili linajionyesha pale Mbezi Beach Samaki wabichi, kwenye daraja. Kwa ujenzi wa aina hii nani wa kulaumiwa???for sure ni Serikali
  • Serikali imekuwa nyepesi mno kutoa maagizo kwa wakazi wa mabondeni kuwa wahame bila kuonyesha nia ya dhati ya kutekeleza maagizo inayoyatoa, serikali legelege!. Sheria zipo wazi. Ni serikali tu imezembea kuzienforce, sielewi ni wapi serikali inapata nguvu ya kunyooshea kidole wakazi wa mabondeni. Hii ni sawa serikali ipige marufuku ujambazi kwa kutoa maagizo/maneno, then ujambaz ukiendelea serikali ilaumu majambazi kwann hawataki kuacha ujambazi bila serikali kuchukua hatua yoyote kwa majambazi. Hapa Serikali inafanya siasa tu.
  • Kitengo cha mipango miji ni kama hakipo, mara nyingi tumesikia serikali ikiwataka wakazi wamabondeni wahame. Serikali ipo kimya katika kuwaeleza wananchi hao wakishahama mabondeni waelekee wapi ambapo pameshaandaliwa kitaalam na wana mipangomiji kwa kuwahost hao wakazi wa mabondeni. Viwanja vyote vinavyopimwa na halmashaur za wilaya haviuziki kwa watu wa kipato cha chini. Upatikanaji wa viwanja hivi ni mpaka uwe na mtu unayemfahamu na anayehusika ktk mchakato wa kuuza viwanja hivyo au upenyeze rupia ili kuondoa udhia. je hapo tutamtupia nani lawama watu wakijibanza mabondeni???
  • Kitengo cha maafa na uokoaji nacho bado kipo usingizini. Mkuu wa mkoa anasema kuwa helikopta za polisi hazijatengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuokoa watu kwenye maafa,na kwamba helikopta hizo zinazunguka ili kutoa taarifa tu, then what????Huu ni utani kbs! Je ni helikopta gan zilizotengenezwa maalum/mahsusi kwa ajili ya kazi hiyo ya uokoaji??kama zipo helikopta mahsusi kwa ajili ya uokoaji kwann nchi haina hata moja????mbona hatujaziona zikisaidia wananchi????
Kwa sababu tajwa hapo juu na nyingine nyingi, si busara kwa serikali kunyooshea kidole wakazi wa mabondeni/vichuguuni. Na pia si busara kwa serikali kuanza kugombeza/kulaumu(kama alivyofanya mkuu wa Mkoa wa DSM) kwa wakaazi wa mabondeni/vichuguuni muda huu wa maafa ambapo watu wapo katika majonzi makubwa ya kufiwa na kupoteza mali zao. Kama serikali ingekuwa makin wananchi siku nyingi wangekuwa wameshahama mabondeni. Serikali inapaswa ichukue hatua za makusudi za kuwasaidia waliopata maafa kwa kuwapa misaada stahiki ya kibinaadam. then hali ikishatengamaa, moja kwa moja serikali ichukue hatua madhubuti ili kuhakikisha suala hili halijirudii tena na linakuwa historia.
 
Kila mmoja hajawajibika ipasavyo,vinginevyo hali isingekuwa kama ilivyo.
 
Serikali sababu inajua fika Sehemu za jiji la Dar ziko chini ya usawa wa Bahari; umeona nyumba zilizojengwa wakati wa Ukoloni? hakuna hata moja iliyochini ya maji angalau wakoloni walijali uhai wetu sio wazalendo wanajali matumbo yao - uhuru bwana
 
Kabla ya kuuliza swali hili jiulize nio wapi duniani umewahi kuona mafuriko yakitoka nchi kavu kwenye eneo ambalo ni mita 100 kufika baharini? Mara zote miji au maeneo ya karibu na bahari huwa yanaathiriwa na maji yanayotoka baharini kuelekea nchi kavu kutokana na sababu mbalimbali kama vimbunga,Tsunami n.k sasa hii ni ajabu jipya la dunia ...
 
Sio muda wa lawama huu, ni muda wa kuwajibika na kuwajibishana bila kuangalia makunyanzi, awe aliyejenga, aliyeruhusu kujenga, aliyepeleka huduma za jamii, anayewakilisha kiutendaji nk.
 
Na bado inawezekana maji ya kutoka Maneromango na Kisarawe hayajatiririka yote down the Msimbazi.

I pray not.
 
Back
Top Bottom