Maafa Makubwa yanasubiriwa Ubungo Bus Terminal

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,233
8,431
Nimekuwa nikijiuliza kila mara niingiapo UBT (Ubungo Bus Terminal) alfajiri hadi saa 1 hivi asubuhi na kukuta msongamano mkubwa wa Mabasi yaendayo mikoani, magari madogo ya wasindikizaji, Taxi, abiria na wasindikizaji wao bila kuwasahau Madereva, Makonda, wapiga debe na hata wafanyakazi mbalimbali wa UBT na mabasi. Swali ninalojiuliza ni hili, " Je siku moto ukiwaka hapa stendi kuanzia majira ya saa 11:30 hadi 12 hivi asubuhi nini kitatokea?" Hakika ni maafa makubwa.

Ni maafa makubwa kwa nini? Hii stendi ina Milango 3 ya kuingilia na kutokea kwa mabasi na magari. Milango ya abiria ndio hivyo tena inakuruhusu kuingia tu lakini wakati wa kutoka unatumia kimlango kimoja. Katika Mazingira haya unategemea utawezaje kuokoa watu pamoja na mabasi/magari kwa uharaka kwa kutumia hii milango iliyopo?

Nashawishika kuamini kwamba hawa wasimamizi wetu (Serikali), kama ilivyowahi kutokea huko Mwanza na Bukoba (MV-Bukoba) na sasa Zanzibar (MV - Spice), ni wazembe.

Ukifika Ubungo pale, ile asubuhi, ni lazima utaogopa. Hivi kweli hii serikali yetu inawatu wanaotafiti (identify), kutathmini (assessment) na kutafuta namna ya kudhibiti (Manage) majanga/hatari hizi (Risks) kabla hazijatokea? Haingii akili kuona unasubiri kwanza maisha na mali za watu ziteketee ndio uuende tume. Kwa nini msifanye tafiti mapema hasa katika maeneo yanayogusa maisha ya watu kama vile maeneo ya usafiri, mikusanyiko ya watu na mkachukua hatua mapema, basi kama sio kuzuia majanga basi iwe kupunguza athari zitokanazo na majanga haya.

Ubungo Bus Terminal ni janga lingine linalosubiriwa kutokea (Mungu apishe mbali) na hatari kubwa ni kwamba mabasi na baadhi ya abiria hasa wazee na watoto, walemavu na wagonjwa hawataweza kujiokoa.

Tusisubiri kila kitu kukielekeza kwa Mungu tikidai ni mitihani yake wakati ni Uzembe wetu tena tena uliowazi. Chukueni hatua......
 
Mkuu inawezekana ikawa kweli kwa mtizamo wa haraka haraka kulingana na idadi ya watu wakati ulioutaja hapo juu! Lakini moto huo kwa eneo lile (open space) lazima iwe ni moto wa mlipuko mkubwa kama bomu au kitu kingine chochote.

Ukitaja mlipuko wa moto wa aina hiyo basi si kwa UBT pekee, fikiria na huku katikati ya jiji kwenye mlundikano wa majengo na miundo mbinu hafifu na uwingi wa wafanyakazi, sijui, labda, Mwenyezi Mungu atuepushie na maafa ya maji bahari ya Hindi.
 
tutapewa siku tatu za maombolezo na kuombwa "eti tuwe na subira"
 
Umewahai jiuliza mitambo ya umeme wa gesi iliyoko hapo Ubungo na maelfu ya wananchi wanaofanya biashara zao pale na wale wanaokua foleni ktk magari kukitokea ajali ya moto itakuaje?
 
Serikali makini ingeshaliona hilo na kuchukua hatua we subiri tu... Its a matter of time!
 
Umewahai jiuliza mitambo ya umeme wa gesi iliyoko hapo Ubungo na maelfu ya wananchi wanaofanya biashara zao pale na wale wanaokua foleni ktk magari kukitokea ajali ya moto itakuaje?


Hapa ndo kwenye potential mlipuko, high impact kuliko maelezo maana watu ni wengi and its likelhood is higher above the alarming threshold(ilishawahi kujaribu kidogo tu ikathibitiwa) , lakini hakuna tahadhari yoyote.
 
Mkuu hii ndiyo kuwa proactive hasa. Ni kweli inabidi sasa watanzania tuwe tuna identify risks mbalimbali na kuishauri serikali la kufanya isipofanya na janga likatokea tuiwajibishe tu hata kwa kupiga mayowe na kuizomea. Sasa tuanze na hili potential janga la UBT.
 
Kusema kweli kwa wazo lako ni muhimu sana wazili muhusika afikishie huo ujumbe naye aufanyie kazi mana litakuwa ni janga la kitaifa.mungu atuepushie mbali
 
hata uswazi pako hovyo kabisa kiasi kwamba ajali ikitokea
ni hataki kama kule kenya,kifupi no mipango miji at all
 
Juzi wametabiri maafa ya bweni la udsm, jana wametabiri maafa ya treni, leo UBT.. Kesho?
 
Mi naona muda umefika sasa na sisi watanzania kila mmoja wetu achangie kwenye maendeleo ya taifa lake baadala ya kuitegemea serikali kwa kila jambo. Kuna watu wanamijumba ya thamani kubwa hadi biliona lakini hajawahi hata kujitolea hata cent 1 kuchangia maendeleo yoyote. Kwa mfano float jackets mtu unaweza kutoa kama msaada, panda hata miti kwenye mtaa wako, . Upunguze ubinafsi na utegemezi , serikali pekee haiwezi kukuletea maendeleo.
 
serikari inasubiri matukio makubwa watakachofanya ni kuunda tume na kukalia report ya tume... then siku za maombolezo kutangazwa na viongozi wote wa serikali kutembelea wahanga na kujifanya wana uchungu sana
 
Very well said , maana wasomi na wataalam wetu hujulikana wakati wa kujadili baada ya matukio na maafa lakini huwa hawaangalii madhara kabla ya maafa maana si sehemu ya utaalam na usomi wao .
 
Hakuna kitisho cha moto UBT, vitisho pale ni vibaka, wapiga debe wanaoongeza cha juu hadi 100% ya nauli, kulazimishwa kulipa ada ya kuingia hata unasafiri, kukosa sehemu ya kukaa hasa jioni lile banda kuu linapofurika abiria, madereva kuuziwa pombe usiku kocha na asubuhi kupakia abiria, magari kuchelewa kuondoka kinyume na ratiba zao kisha mbele ya safari yanakimbizwa spidi 120 kufidia muda, taxi kutoza gharama za kizungu hata kwa wadengereko, kumpoteza mgeni wako anayefika kwa mara ya kwanza kituoni kwa sababu anapewa maelekezo ambayo hayajui, nk........

hili la moto umejaribu kutahadharisha tu lakini silo hilo...........
 
safari hii tutatafuta mchawi toka kampuni ingine sijui itakuwa TIGO, AIRTEL n.k

Nimeipenda sana hii. mi nilidhani imebinafsishwa kumbe wameuza kabisa

avatar41784_2.gif
 
Nimeipenda sana hii. mi nilidhani imebinafsishwa kumbe wameuza kabisa<br />
<br />
<img src="https://www.jamiiforums.com/customavatars/avatar41784_2.gif" border="0" alt="" />
duh, kama vipi nipewe changu niondoke...
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom