Maafa makubwa kutokea serikali ikijaribu kufanya haya kwenye mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maafa makubwa kutokea serikali ikijaribu kufanya haya kwenye mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by vimon, Mar 8, 2012.

 1. vimon

  vimon Senior Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kutokana Taarifa zilizonifikia punde wakati nikipita katika hospitali zetu za rufaa na Kuongea na baadhi ya Madakatari kuna mpango ambao serikali ikiutekeleza itakuwa kwenye wakati mbaya na inawezekana ikamfanya mkuu wa nchi atishi uchaguzi wa uraisi mapema kabla ya 2015.

  Mambo haya ni yafuatayo:-

  1. Kuwafukuza madaktari wote na kuwaambia wa apply upya
  2. Kuwaleta flying doctors (Naomba tusiulize mambo ya malipo kwao, maana it is only spinal cord working by now)
  3. Residents kufutiwa udhamini
  4. Kuleta madaktari wa kichina au kutoka nje

  Mambo yatakayotokea
  1. Mgomo utasambaa nchi nzima na utawahushisha kada zote mpaka manesi,utajuumuisha dispensary,hospitali za wilaya na hii itakuwa ni kuparalyse mfumo mzima wa afya Tanzania
  2.Hawata apply kazi upya na wameapa kuwa wammoja mpaka mwisho wa mgomo kwa hiyo serikali itakuwa imepoteza na huu wamesema itakuwa ndio ticket ya kuondoka kwa baadhi ya madaktari.
  3. Hii ya kufuta udhamini itawaumiza wananchi na taifa kwani Tanzania ni ya mwisho duniani kwa ratio ya doctor to patient na kufikia malengo ya WHO ya patient to doctor ratio ya 1:7,500
  The doctor : patient ratio in Tanzania is 1 : 26,000, Uganda's rate is 1 : 8,000 and Zambia's is 1: 11,000 Source WHO
  4. Mfumo wa flying doctors ni wa ghali za kuendesha na unaendeshwa na AMREF,unatumia wataalamu kutoka nchi husikana jirani sasa mara nyingi wanasaidia na na wataalamu wa ndani kuandaa vifaa na mambo mengine hapa naona serikali yetu ina maana imepata pesa wapi ya mipango ya dharura.
  5. Iwapo manesi na kada nyingine ambao wanaonekana hawajagoma lakini wanajuwa madaktari wakifanikiw na wao wamefanikiwa hawatakubali kufanya kazi na hao watakaoletwa (HAPA NI HATARI)
  6. Iwapo ikatokea baada ya huu mgomo tukawa tumewapoteza madaktari wetu kwa mfano wengine wkiamua kuachana kazi ya kutibu wakaenda kweny NGOs,hospitali za private,research,siasa,private sector au hata wakaenda nje ya nchi hapa atayeumia si mwananchi wa chini. Gharama ya kumsomesha daktari mmoja si chini ya milioni 42 serikali yetu ipo tayari kupoteza kiasi hichi cha pesa?

  Kama hospitali zetu hazina mashine za kisas nyingi ni mbovu,miaka ya hamsini ya uhuru hospitali ya taifa inaweza kuishiwa hata na gloves lakini hawataki kuambiwa ukweli wao wanasingizia kila kitu ni siasa/udini na mambo ambayo haya msingi.

  Kama kweli madaktari wanalipwa vizuri kila sector iweke mishahara na marupuru yake hadharani tuone kama nchi itatawalika kama migomo haitatawala kila kona tuanze na mishahara TRA, BOT, TANAPA, BUNGE Alafu tulinganishe na ya madaktari, waalimu, wanajeshi, manesi, Engeneers, lawyers etc alafu kama haipo sawa tuweke sawa ili tuache kutafuta mchawi kila mtu aridhike na professional yake na sio kulalamika kila kukicha.

  Nawaunga mkono madaktari naamini mwisho wa siku ukweli utajulikana.

  Mungu ibariki Tanzania!

  Updates za Mgomo kupatika mchana fuatilia hapa..
   
 2. Mbavu mbili

  Mbavu mbili JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 803
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  mmmmh kazi ipo
   
 3. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Kuna wakati nikiona tangazo la ajira TANAPA, walikuwa wanahitaji katibu muhtasi.Mshahara ulikuwa laki 9 na ushee plus other benefit.
   
 4. P

  PakavuNateleza JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 957
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 180
  Serikali inapambana na watu(doctors) ambao hawana cha kupoteza, and that is a very bad war
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Madaktari wangeorodhesha japo kwa kifupi vifo vinavyotakana na ukosefu wa vifaa/dawa. Serikali inaonekana kuzidisha propaganda hivyo nadhani ni vizuri kuonesha ni jinsi gani afya za watanzania zinawekwa hatarini kutokana na uzembe wa serikali.

  Kwa mfano, waseme wagonjwa wanalala wangapi kwenye kitanda kimoja, hospitali ziko ngapi na ngapi kati yake zina x-ray na vifaa muhimu vya upasuaji, madaktari wanafanya kazi masaa mangapi kwa siku, na wanatumia mbinu gani pale wanapokosa vifaa muhimu. Kuna hospotali hata gloves hakuna! Doctors wanatakiwa sasa wajielekeze kwenye points ili kuzima hizi propaganda.
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  CRAAAAAAAAP. Hakuna kitu hapo ulichoandika zaidi yakuandika makala ndefu na ***** mtupu. Wafukuzwe na washitakiwe. Na wakija huku mtaani waje wapambane na sie magwiji wa Street University,wataomba wao wenyewe kurudi

   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Najua na wewe ni daktari, unasikilizia upepo unaendaje. Mtakoma, mnafikiri tutawaunga mkono kwa kuacha kutoa matibabu, wapuuzi kabisa nyie!
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huu ulioubandika hapa ni ugaidi, na unamtisha nani? wananchi au Serikali? Tunaomba utujulishe wewe ni nani tuje tuongee ana kwa ana, kama kweli una nia njema na nchi na wananchi wa Tanzania.
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tusiende mbali muhimbili wodi ya wazazi kitanda kimoja wazazi wawili pamoja na watoto wao.
  Imagine vitanda vyenyewe sijui ni 6*3.
  Achilia mbali wanaolala chini!
   
 10. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  wewe siyo dume la mbegu, bali unapewa mbegu na midume
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280


  aisee mnapata shida kweli.
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CHADEMA wanataka kutumia maisha ya watanzania kujitafutia umaarufu wa kisiasa! Hili litawagharimu sana baadaye!
   
 13. K

  Karata JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Idadi ya madaktari (MDs) Tanzania 2010/2011 ni 4,649. Idadi ya madaktari bingwa nchini Tanzania 2010/2011 ni 377, zaidi ya 80% ya madaktari bingwa wapo hospitali ya Taifa Muhimbili. Idadi ya wingi wa watu Tanzania ni mill 45. Zaidi ya 90% ya watu wa Tanzania ni maskini. Mahesabu yeyote anayoyafanya Pinda yaanzie hapa.
   
 14. Kiwewe

  Kiwewe Senior Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama Serikali itaweza kufanya upuuzi wa kuwaleta Flying doctors. Kama kweli serikali imefikia hatua hii ili kuonyesha ubabe wake na kuacha kushughulikia matatizo ambayo yapo ndani ya uwezo wake, basi wajiandae kuleta Flying teachers, Flying famers, Flying lawyers, Flying Engeneers nk. Nafikiri hili litasaidia kuboresha hizi sekta na kutuashiria watanzania kwamba kuna kada zisizotakiwa nchini humu. Kama ilikuwa inapesa kiasi hicho, ilishindwaje kuzitumia katika kufanya maboresho kwenye afya, elimu, kilimo, miundombinu nk. SIDHANI KAMA SERIKALI ITAFIKIA KUFANYA UPUUZI HUU.
   
 15. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa taarifa tu kada nyingine za afya hasa mawilwyani na mikoani mpaka vijijini ndio zinazo piga mzigo wa kutibu Watanzania walio wengi kada hizo ni kama AMO,CO,MAFUNDI SANIFU,WAUGUZI WA AINA ZOTE hawa mishahara ya Madaktari ikipanda na wao wamepata sasa tusiombe na wao wagome itakuwa balaa wakuu haijawahi tokea nchi hii kitanuka sasa serikali iwe sikivu isije kukuza mambo yakawa makubwa itatue tatizo hili mapema.
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dume la Mbegu na Jabulani

  1. Mnajaribu kuzuia mafuriko yasitafute njia

  2. Ndiyo maana mpo "Street University" ambako mtindio wa ubongo mllio nao mnatibu kwa madawa ya kulevya kama siyo tunguli.

  3. Msisahau kila zama na mambo yake. Hili la migomo ikiwepo ya madaktari mnalo na hamna jinsi
   
 17. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  mbaazi akikoswa maua husingizia jua
   
 18. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CDM wanatoka wapi tena? Au ni yale yale kama walivyoleta mafuriko Dar?
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wajalibu kuwafukuza waone....na kwa taarifa zilizopo huo ndio mpango wa pinda na mjinga mwenzie jk
   
 20. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo viongozi wetu wapo kwa maslahi yao binafsi, ndiyo maana hawana wanachofikiri chochote cha kuwahusu wananchi. Nawaunga mkono madaktari
   
Loading...