Maadui wa nchi yangu


Forgo

Forgo

Member
Joined
Apr 7, 2016
Messages
27
Likes
60
Points
15
Forgo

Forgo

Member
Joined Apr 7, 2016
27 60 15
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitufundisha kuwa maadui wakubwa watatu ni umasikini, ujinga na maradhi.

Mwalimu hakuishia hapo, bali alikuwa na ulimi wa kushawishi wananchi wake wafanye kazi kwa nguvu, hiari na furaha. Wakati fulani mwaka 1967 akiwatembelea wananchi wa Handeni waliojenga shule kwa gharama zao wenyewe, kiasi cha Tsh. 200/= aliwaambia;
"Msipojitaabisha kwa faida yenu wenyewe, basi mtataabishwa kwa faida za wengine".

Ni kauli hamasishi, ndio sifa ya kiongozi.

Miongo mitano baadae, maadui ni wale wale; Umasikini, Ujinga na Maradhi. Lakini sasa watawala wanajiongezea maadui wengine; wananchi wao wenyewe.
Ndio, huwezi kumnyina Uhuru mwananchi wako halafu ukamuita rafiki, tayari ni adui. Kwa kuwa Uhuru wa kuongea ni tunu ya asili kutoka kwa Mungu mwenyewe. Kuwaziba watu midomo ni kujipa uungu. Na kwa hiyo unakuwa mungu mtu. mungu mtu hawezi kuwa mtu! Na hawezi kuonwa kuwa ni miongoni mwa watu. Anakuwa kiumbe kingine cha kuogofya. Unapokutana na Mungu mtu, utu wako unanyauka kama nyasi wakati wa jua kali, na uhai/afya yako itategemea namna utakavyomtazama/ utakavyomu'handle'.

Kwa sababu hiyo, ingawa maadui wetu sisi wananchi ni walewale, umasikini, ujinga na maradhi, lakini watawala wetu wamejiongezea adui wa nne. Ukiwauliza watasema ni vyama vya siasa lakini kwa uhalisia wake, ni wananchi, au kwa usahihi zaidi, 'wenye nchi'. wanaweza kuwa wachache au wengi.
Ni aibu kutumia mabavu kuzima sauti za wananchi 'waliokuchagua wenyewe'. Ni tabia za watawala wa kale, 'uncivilized'. 'Primitive'. 'Barbarism'. Miaka 10000+ iliyopita.

Wakati tukiwapa dhamana ya kutuongoza kupigana na maadui hawa watatu, wao wanajiongezea adui wa nne! Na adui huyo ni sisi wenyewe. Hatutavuka.
Kuna kitu cha kuongeza hapa! Mtu mmoja (a superficial observer of events) anaweza kuwaza kuhusu makundi kinzani, kwamba pengine andiko hili ni kutoka kundi kinzani, na kwa hiyo lina lengo kinzani!
Ndio, ni kundi kinzani! Lakini kuna zaidi hili;

Adolf Hitler, Joseph Stalin, Gorbachev nk. Nao walikuwa na wafuasi vilevile. Tena walisheherekewa kweli, kwa vitendo vyao vya kinyama.
Hapa ndipo kanuni ya siasa inapojidhihirisha, kwamba; Watawala huwagawa wananchi katika makundi makubwa mawili; Maadui wao na Vijakazi wao! Nimesema watawala sio viongozi.
Bado natathmini ile ziara ya kwanza, Ilikuwa Rwanda.

Anawakilisha Dr.
 

Forum statistics

Threads 1,235,066
Members 474,351
Posts 29,211,286