Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,666
Habari za saa hizi waungwana
Maadili ni misingi ambayo jamii imejijenga na kujiwekea ya kwamba yanakubalika kwenye jumuiya ya wengi,ni yale matendo yaliyosahihi na yanayowapendezea weng.Wengi wanaambatanisha haya na misingi ya dini na hofu ya mungu lakini kwa mtazamo wangu ni fikra ambazo watu wamejiwekea mfano kuwa na mavazi yenye heshima,kuwa mkarimu na mwenye hekima,kuwa mcha mungu.Kwangu mimi imani ya mtu ni chaguo la mtu binafsi.
Lakini je tushawahi kufikiria kwamba maadili hayohayo yanatunyima uhuru wa kufanya yale ambayo yapo kwenye fikra zetu?ambayo ukiyafanya unakiuka maadili na jamii inakutazama kwa jicho la tatu?Je tumekuwa watumwa wa maadili ambayo tumejijengea kwenye jamii inayotuzunguka. Wengi wanatenda yale ambayo wanaona ni sawa kutokana na maadili na misingi walolelewa nayo lakini kuna wale ambao wanaogopa kufanya yanayowapendezea kwa kuhofia jamii au ndugu wanaowazunguka watawachukuliaje na kuwaelewaje!!Kwanini watu wanajali zaidi kufanya yale yanayowapendezea wengine na yaliyo ya fahari kwenye macho ya wengi kuliko kufanya yale yanayowaridhia?Je nitakosea nikisema tunazidhulumu nafsi zetu?Kama maisha ni yako,ishi unavyopenda ndio utafurahia maisha!Tambua yale yalo na umuhimu kwako na uyatendee haki.Umekuja peke yako kwenye dunia hii na utaondoka peke yako,"Be free" percieve your goals and dreams,"A true spirit will give you peace of heart and mind"
Karibuni wapendwa!