Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Sasa sijui wangapi mliwahi kusikia juu ya maadili ya matangazo ya biashara kwenye vyombo vya habari nchini. Lakini kwa muda sasa kumekuwa na mashauriano ya wadau wa eneo hili nyeti na sasa zimebakia saa kama 24 hivi kabla ya muda wa majadiliano kupita. Kutokana na umuhimu wa JF na jinsi watu wanavyotoa maoni yao nimepenyezewa kama vile mtu anavyopenyeza uzi kwenye tundu la sindano nyaraka hii ili itolewe maoni ili hatimaye yawasilishwe pamoja na ya wengine hapo kesho (msiniulize kwanini wasifanye mwisho uwe Ijumaa).
Nimeweka matoleo mawili.
a. Toleo la Kwanza ni makala jinsi ilivyo sasa na maadili yanayopendekezwa na ambayo yanastahili kutolewa maoni. File linaitwa "CODE OF ETHICS IN ADVERTISING"
B. Toleo la Pili ni lile ambalo mimi nimelitolewa maoni (nimetumia rangi tofauti kuweka maoni yangu. Na ninawapa pia kama sehemu ya kuanzia. Linaitwa "code of ethics in ads comments"
Hivyo unaweza kusoma makala ya kwanza kuelewa nini kinapendekezwa katika maadili ya kutoa matangazo ya biashara (yanahusisha mambo ya siasa, dini, elimu n.k ) halafu unaweza kutoa maoni yako.
Napendekeza na wewe ufanya vile vile. Tunza original document kama ilivyo, halafu fungua nyingine na uifanyie commentary halafu isevu kwa jina jingine.
Endapo utamaliza unaweza kutuma moja kwa moja kwenye email iliyomo au unaweza kunitumia mimi nikazikusanya na kutuma zote kama zip file kama mchango wa wana JF kuhusu maadili ya matangazo ya biashara (ethics in advertising)
Kwa vile sisi siyo walalamikaji na wakosoaji tu, wakati umefika tutoe mawazo ya nini kinafaa au kifanyike. Hii ni mojawapo ya nafasi za kufanya hivyo.