Maadili ya kazi na tabia zetu sisi hasa watanzani!

wabuyaga

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,683
1,225
Ndugu wana JF,
Ninaomba niongee machache kutokana ninayoendelea kuyaona katika kufanya biashara pamoja na kazi za kiofisi hapa nchini.

Je ni kweli sisi tunashindwa kuthamini muda wa kazi? Inakuwaje mtu mnapanga kukutana saa nne, eti baadae anatoa excuse kuwa alisahau au ana shughuli nyingine hata bila kukutaarifu kabla ya kuanza safari ya kukutana naye! Hao ni watanzania wenzangu.

Je ni kweli tunashindwa kutimiza ahadi zetu? Haya nitalishughulikia hili jambo ktk siku 5 zijazo nitakupa jibu! Jibu hakuna na hata kutuma email au msg hakuna kabisa. Hao ni watanzania wenzetu

Mfano mwingine wa kusikitisha kabisa:
Mimi na rafiki yangu kutokea Norway, tulikuwa na appointment na baadhi ya jamaa hapa Dar (some were prof and Dr by ac achievement----). Baada ya kufika ofisini kwao hawakuwa wamejiandaa kuhusu maswala tuliyokubaliana kuyazungumza. Aibu kama hii ilinipata kwani mimi kama mtanzania, na colleaque alikuwa ni mgeni! Jamain hata wasomi wetu? Hao ndio watanzania wenzetu!

Hivi jamani ninauliza, kwa mwendo huu tutafika? Au mimi ninakutana na maajabu ya MUSA? Hebu nijuze experience yenu kutokana na HILI!
 

Bonny

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
13,222
2,000
weee unaona hilo kubwa wenzio wameoindua mpaka rasimu ya warioba wameweka ya kwao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom