Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi): Tarehe 1/5/2022

Kupandisha mshahara ni jambo moja, lakini kupanda bei kwa vitu vingine sokoni ni kitu kingine chenye athari pacha.

Ili kutimiza tu wajibu serikali inaweza kutoa ongezeko kiduchu la mishahara "as response to inflationary effect". Lakini ongezeko hili halitaweza kuwa na maana yoyote ile ikiwa kama kila kitu sokoni kitapanda bei.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Wafanyakazi leo mpagigwa na kitu kizito kichwani au chenye ncha kali kama cha Morrison.

Kodi kuongezeka. Nchi inahitaji hela. Wananchi lazima mkamuliwe kama dekio la mochwari.
 
Kupandisha mshahara ni jambo moja, lakini kupanda bei kwa vitu vingine sokoni ni kitu kingine chenye athari pacha.

Ili kutimiza tu wajibu serikali inaweza kutoa ongezeko kiduchu la mishahara "as response to inflationary effect". Lakini ongezeko hili halitaweza kuwa na maana yoyote ile ikiwa kama kila kitu sokoni kitapanda bei.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Hivi vitu vilivyopanda bei Kwa sasa ni sababu ya ongezeko la mshahara au?
Hivi unajua mara ya mwisho mshahara umeongezwa mwaka 2015, hapo bei ya sukari tu ilikuwa TSH 1800 Kwa kilo, jiulize sasa hivi sukari bei gani na mshahara haujawahi kupanda.

Hakuna haja ya kuremba maneno, marehemu alikuwa na roho mbaya....mama asiige Ile roho, ajue Mungu hachapi kwa fimbo
 
Wahenga walisema usiku wa deni haukawii kukucha. Leo wafanyakazi wa Tanzania wanaungana na wafanyakazi kutoka pembe zote za dunia kuadhimisha siku ya wafanyakazi, maarufu kama Mei Mosi. Mtakumbuka mwaka jana Rais wa Tanzania Hon Samia Suluhu Hassan aliaahidi kuwaongezea mishahara wafanyakazi siku ya leo tarehe 1/5/2022 kama alivyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Leo ndio leo, asemaye kesho ni muwongo! Leo lazima mbivu na mbichi zijulikane. Lakini pamoja na ahadi hiyo ambayo Rais aliitoa kwa uhakika, wafanyakazi wajiandae kwa jibu lolote la kukera litakalotolewa siku ya leo kwani mvumilivu hula mbivu. Waendelee tu kuvumilia huku wakila mtori kwa kuwa nyama ziko chini. Unapokula mtori hupaswi kuwa na wasiwasi kwani baada ya kumaliza mtori utazikuta nyama tele chini ya bakuli.

Hata hivyo, habari zinazojipenyeza ni kuwa huenda vita ya Ukraine na Urusi ikachangia mama Samia kutokuwaongezea wafanyakazi mishahara kwa sababu vita hii imeangusha uchumi wa nchi zote duniani, ikiwemo Tanzania kama anavyotupenyezea taarifa mdau huyu hapa chini

Uhakika: Jinsi Vita ya Urusi na Ukraine Itakavyokwamisha Upandishaji wa Mishahara ya Wafanyakazi

Tuendelee kufuatilia nini kitakachotokea siku hii ya leo kwani ni siku mbayo ama wafanyakazi watalia au watatoka na kicheko. Stay tuned!​
Jinga wewe rudi darasani
 
Waziri wenu alishafafanua kuhusu mishahara
IMG-20220430-WA0026.jpg
 
Nakumbuka 2018 Makonda alisema anaomba ruhusa awachape viboko wanaoomba kuongezewa mishahara!!! Miaka 6 ya Magufuli nchi imenajisiwa sana na wahuni
 
kuna baadhi ya watumishi wa umma wanapokea mamilioni na marupurupu kibao!!
sasa hao waongezewe mshahara wa kazi gani?!
nadhani wanao stahili ni wale wa kima cha kawaida/chini
 
Back
Top Bottom