Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi): Tarehe 1/5/2022

Mshahara unatosha. Akipandisha vitu vitspanda
Kweli kabisa mkuu. Mishahara ikipanda tu bidhaa na huduma zitapanda bei maisha yatakuwa magumu sana kwa wapigakura. Chondechonde Rais Samia usipandishe mishahara hata kwa senti moja mama yetu mpendwa.
 
Hiyo fedha iliyofujwa na wahuni wachache kwanini haiwanufaishi watumishi?
Wanaofuja fedha nao ni wazalendo kwa kuwa fedha wanazofuja zinaongeza mzunguko wa fedha mtaani hivyo kuwanufaisha wapigakura. Wafujaji wanapaswa kupongezwa kwa kitendo hiki cha uzalendo.
 
Kwa huu wimbo wa mrisho mpoto ni ishara ya moshi mweupe kwa wafanyakazi.

Imeisha hiyo.

Mama wameshampunguzia jambo hapo. Kazi ni kwake tu kutoa namba zitakazo wafanya wafanyakazi wa furahie.
 
Wahenga walisema usiku wa deni haukawii kukucha. Leo wafanyakazi wa Tanzania wanaungana na wafanyakazi kutoka pembe zote za dunia kuadhimisha siku ya wafanyakazi, maarufu kama Mei Mosi. Mtakumbuka mwaka jana Rais wa Tanzania Hon Samia Suluhu Hassan aliaahidi kuwaongezea mishahara wafanyakazi siku ya leo tarehe 1/5/2022 kama alivyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Leo ndio leo, asemaye kesho ni muwongo! Leo lazima mbivu na mbichi zijulikane. Lakini pamoja na ahadi hiyo ambayo Rais aliitoa kwa uhakika, wafanyakazi wajiandae kwa jibu lolote la kukera litakalotolewa siku ya leo kwani mvumilivu hula mbivu. Waendelee tu kuvumilia huku wakila mtori kwa kuwa nyama ziko chini. Unapokula mtori hupaswi kuwa na wasiwasi kwani baada ya kumaliza mtori utazikuta nyama tele chini ya bakuli.

Hata hivyo, habari zinazojipenyeza ni kuwa huenda vita ya Ukraine na Urusi ikachangia mama Samia kutokuwaongezea wafanyakazi mishahara kwa sababu vita hii imeangusha uchumi wa nchi zote duniani, ikiwemo Tanzania kama anavyotupenyezea taarifa mdau huyu hapa chini

Uhakika: Jinsi Vita ya Urusi na Ukraine Itakavyokwamisha Upandishaji wa Mishahara ya Wafanyakazi

Tuendelee kufuatilia nini kitakachotokea siku hii ya leo kwani ni siku mbayo ama wafanyakazi watalia au watatoka na kicheko. Stay tuned!​
Ni kufurahi kwa kwenda mbele.
Wenye roho mbaya mfyuuuuu zenu
Jambo letu na mama limepita
 
Vitu vimepanda maradufu,je ni miaka mingapi mishahara haijaongezwa?
Nashauri hizi nyongeza za mishahara zitungiwe sheria na kanuni isiwe hisani ya wanasiasa hasa Rais.
Ndio maana niliwapa tahadhari mapema kuhusu hili jambo lakini wengine wakaishia kunibagaza na kuniona bazazi. kiko wapi sasa?
 
Mbona hakupandisha lakini tayari bidhaa zilishapanda mapema sana, tena hata kabla ya vita vya Ukraine na Russia

Hivi huwa mnafikiri kabla ya kuongea au ilimradi tu nanyi mmeonekana hapa JF

Heri aghairi kabisa au kupunguza bajeti ya gharama yoyote ile kati ya vipaumbele mojawapo kiuwekezaji 2022/23, kuliko kuvunja rekodi ya UNAFKI kwa kuahidi watu kupandisha mishahara kisha kutopandisha.

Ni mwaka wa 7 sasa mishahara haijapandishwa huku hali mitaani kiuchumi ikiwa tete kabisa.

Natumai Mama ataupiga mwingi, ili CHAWA tuje tuzagae hapa JF kusifia hata visivyostahili kusifiwa, sababu ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi siyo hisani bali ni haki yao kisheria, duniani kote
Tetete kwa hiyo kaupiga mwingi?
 
Back
Top Bottom