Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Nape Nnauye: Inauma kuona tunateswa na rasilimali zetu wenyewe. Wanahabri tusaidie

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKINOLOJIA YA HABARI MHE. NAPE NNAUYE (MB) AKIFUNGUA MAONYESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI NAYOFANYIKA JIJINI ARUSHA TAREHE 2 MEI, 2022

Mhe Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Arusha na mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Mheshimiwa Balozi Manfredo fanti, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania;

Zlatan Millisic, Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa (UN),
Prof. Hubert Gijzen, Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki,
Musabayana Wynne Zvinaiye, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tume ya Muungano WA Umoja wa Afrika,

Mabalozi wote mliopo hapa
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha na Mikoa jirani mliopo hapa;
Ndg. Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali;

Wakuu wa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi mliopo hapa;

Ndg. Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho haya ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani;
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, Churchill Otieno;
Washirika wa Maendeleo;

Wageni Waalikwa;
Waandishi wa Habari;
Mabibi na Mabwana.
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Awali ya yote naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru sana waandaaji kwa kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonyesho ya Sherehe za Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani kwa Mwaka 2022.

Napenda vile vile kutumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru wote mlioko hapa kwa kukubali kuacha shughuli zenu na kuja kushiriki nasi katika shughuli hii muhimu.
Ndugu Washiriki,

Kama tunavyojua, maonyesho ninayoyazindua leo ni sehemu ya shughuli za utangulizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika kesho tarehe 3 Mei, 2022 hapa hapa Jijini Arusha.
Maadhimisho ya Mwaka huu yana Kauli Mbiu inayosema Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti. Katika mazingira ya sasa ya kasi kubwa ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, si ajabu kuona waandaji wa maadhimisho haya wameona ni muhimu kuangalia changamoto za kidigiti kwenye uandishi wa habari.
Ndugu Washiriki,

Najua kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari na Taasisi zake, UNESCO, Vyombo vya Habari na Wadau wa Habari mnashiriki kwenye Maonyesho ya shughuli mbalimbali za wanahabari.
Lakini pia kuna Kliniki ya Kisheria kwa waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vyombo vya habari pamoja na kazi za taasisi zingine zinazosaidia utekelezaji wa majukumu ya vyombo vya habari.

Naomba niwapongeze kwa jitihada na ubunifu huu kwani wanahabari watapata kujifunza mengi kupitia maonesho haya.

Pamoja na mambo mengine wanahabari watapata uelewa juu ya Sheria mbalimbali zinazogusa Sekta ya Habari nchini. Mjadala na uelewa wa sheria mbalimbali zinazogusa tasnia ya habari hasa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2017 na ile Sheria ya Haki ya kupata taarifa ya 2016 pamoja na Kanuni zake, ni muhimu sana wakati huu ambapo tupo katika mchakato wa kufanya mapitio ya sheria na Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
Ni matumaini yangu kuwa uelewa na uzoefu tutakaoupata kwenye ushiriki wetu hapa utasaidia sana kwenye mchakato wa mapitio hayo ya sheria husika.

Ndugu Washiriki,
Nimeelezwa pia kuwa mtakuwa na mijadala na mawasilisho mbalimbali yenye lengo la kuangalia changamoto na fursa katika sekta ya habari Barani Afrika.

Lakini pia ni matumaini yangu kuwa mtatumia fursa hii kujadili na kutafuta njia bora za kushughulikia na kukabiliana na changamoto mtakazozianisha. Naamini mtaainisha pia fursa zilizopo katika kuendeleza sekta ya habari Barani Afrika.
Nimeeelezwa kuwa miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti, Matumizi ya Teknolojia katika kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari, Ubunifu na Tafiti, Majukwaa ya Kidijiti kama Chachu kwa Maendeleo ya Vyombo vya Habari na Kujenga Mshikamano wa Waandishi wa Habari Barani Afrika.

Ndugu Washiriki,
Mada zote nilizozitaja na zingine ambazo sijazitaja ni muhimu katika kuleta afya na maendeleo katika sekta ya habari Barani Afrika.
Ninaamini zitasaidia katika kuongeza wigo wa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza na kupata taarifa. Niwaombe mjadili kwa kina na kuja na majibu ambayo yataleta suluhisho ya changamoto zinazovikabili vyombo vya habari barani Afrika.

Aidha, wakati mkiendelea na mjadala, ni muhimu kuona jinsi vyombo vya habari vitakavyoweza kulinda na kuendeleza uhuru, rasilimali na utamaduni wa mataifa ya Afrika na maslahi mapana ya nchi na Bara la Afrika kwa ujumla wake.

Ndugu washiriki,
Mwisho napenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana UNESCO kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa habari na usalama wa waandishi wa habari.
Natambua nafasi yake kipekee na msaada wake kwa Serikali ya Tanzania. Pia niwashukuru washiriki wote kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Kwa maneno hayo machache napenda sasa kutamka kuwa Maonyesho haya yamefunguliwa rasmi.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
20220502_130859.jpg

View attachment 2208494
View attachment 2208495
Naiunga mkono hoja hotuba hii
P
 
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Ahsante sana Waziri Nape Nnauye.
Hapo hata kura ya kulamba na mkono(kama ipo) 2035?nipo tayari kupiga.
Good speech, Godspeed.
 
HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKINOLOJIA YA HABARI MHE. NAPE NNAUYE (MB) AKIFUNGUA MAONYESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI NAYOFANYIKA JIJINI ARUSHA TAREHE 2 MEI, 2022

Mhe Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Arusha na mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Mheshimiwa Balozi Manfredo fanti, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania;

Zlatan Millisic, Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa (UN),
Prof. Hubert Gijzen, Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki,
Musabayana Wynne Zvinaiye, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tume ya Muungano WA Umoja wa Afrika,

Mabalozi wote mliopo hapa
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha na Mikoa jirani mliopo hapa;
Ndg. Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali;

Wakuu wa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi mliopo hapa;

Ndg. Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho haya ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani;
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, Churchill Otieno;
Washirika wa Maendeleo;

Wageni Waalikwa;
Waandishi wa Habari;
Mabibi na Mabwana.
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Awali ya yote naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru sana waandaaji kwa kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonyesho ya Sherehe za Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani kwa Mwaka 2022.

Napenda vile vile kutumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru wote mlioko hapa kwa kukubali kuacha shughuli zenu na kuja kushiriki nasi katika shughuli hii muhimu.
Ndugu Washiriki,

Kama tunavyojua, maonyesho ninayoyazindua leo ni sehemu ya shughuli za utangulizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika kesho tarehe 3 Mei, 2022 hapa hapa Jijini Arusha.
Maadhimisho ya Mwaka huu yana Kauli Mbiu inayosema Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti. Katika mazingira ya sasa ya kasi kubwa ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, si ajabu kuona waandaji wa maadhimisho haya wameona ni muhimu kuangalia changamoto za kidigiti kwenye uandishi wa habari.
Ndugu Washiriki,

Najua kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari na Taasisi zake, UNESCO, Vyombo vya Habari na Wadau wa Habari mnashiriki kwenye Maonyesho ya shughuli mbalimbali za wanahabari.
Lakini pia kuna Kliniki ya Kisheria kwa waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vyombo vya habari pamoja na kazi za taasisi zingine zinazosaidia utekelezaji wa majukumu ya vyombo vya habari.

Naomba niwapongeze kwa jitihada na ubunifu huu kwani wanahabari watapata kujifunza mengi kupitia maonesho haya.

Pamoja na mambo mengine wanahabari watapata uelewa juu ya Sheria mbalimbali zinazogusa Sekta ya Habari nchini. Mjadala na uelewa wa sheria mbalimbali zinazogusa tasnia ya habari hasa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2017 na ile Sheria ya Haki ya kupata taarifa ya 2016 pamoja na Kanuni zake, ni muhimu sana wakati huu ambapo tupo katika mchakato wa kufanya mapitio ya sheria na Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
Ni matumaini yangu kuwa uelewa na uzoefu tutakaoupata kwenye ushiriki wetu hapa utasaidia sana kwenye mchakato wa mapitio hayo ya sheria husika.

Ndugu Washiriki,
Nimeelezwa pia kuwa mtakuwa na mijadala na mawasilisho mbalimbali yenye lengo la kuangalia changamoto na fursa katika sekta ya habari Barani Afrika.

Lakini pia ni matumaini yangu kuwa mtatumia fursa hii kujadili na kutafuta njia bora za kushughulikia na kukabiliana na changamoto mtakazozianisha. Naamini mtaainisha pia fursa zilizopo katika kuendeleza sekta ya habari Barani Afrika.
Nimeeelezwa kuwa miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti, Matumizi ya Teknolojia katika kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari, Ubunifu na Tafiti, Majukwaa ya Kidijiti kama Chachu kwa Maendeleo ya Vyombo vya Habari na Kujenga Mshikamano wa Waandishi wa Habari Barani Afrika.

Ndugu Washiriki,
Mada zote nilizozitaja na zingine ambazo sijazitaja ni muhimu katika kuleta afya na maendeleo katika sekta ya habari Barani Afrika.
Ninaamini zitasaidia katika kuongeza wigo wa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza na kupata taarifa. Niwaombe mjadili kwa kina na kuja na majibu ambayo yataleta suluhisho ya changamoto zinazovikabili vyombo vya habari barani Afrika.

Aidha, wakati mkiendelea na mjadala, ni muhimu kuona jinsi vyombo vya habari vitakavyoweza kulinda na kuendeleza uhuru, rasilimali na utamaduni wa mataifa ya Afrika na maslahi mapana ya nchi na Bara la Afrika kwa ujumla wake.

Ndugu washiriki,
Mwisho napenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana UNESCO kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa habari na usalama wa waandishi wa habari.
Natambua nafasi yake kipekee na msaada wake kwa Serikali ya Tanzania. Pia niwashukuru washiriki wote kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Kwa maneno hayo machache napenda sasa kutamka kuwa Maonyesho haya yamefunguliwa rasmi.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari ambaye ni mwandishi wa habari huru na wa kujitegemea kwa kujitolea na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo huru cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari kwa media zetu za Tanzania yetu.

Nawatakia maadhimisho mema ya siku yetu hii ya leo na uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Back
Top Bottom