Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Afrika, leo Julai 12, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,515
8,999


======
Maxence Melo: PESA ZA UVIKO SIO BWERERE, TAKUKURU IPO MACHO
Tanzania imeelezwa kuwa ni miongoni mwa Nchi zinazofanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa licha ya changamoto kadhaa, ambapo ushauri umetolewa pesa za UVIKO-19 zinazotolewa na Serikali zikitakiwa kutumiwa vizuri kwa manufaa ya Taifa na si kuwa maslahi ya watu binafsi

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo amesema wadau kwa kushirikiana na TAKUKURU wanashughulikia masuala ya rushwa ndogo na kubwa kwa kuwapa wananchi uhuru wa kutoa taarifa za rushwa na ubadhirifu ili zifanyiwe kazi

“Rushwa si suala la kuchekea hasa wakati huu ambao kuna pesa za UVIKO-19. Kuna watu wanaona ni pesa za bwerere lakini sisi kama Asasi za Kiraia jukumu letu ni kushirikiana na mamlaka kama TAKUKURU kupambana na rushwa kwa vitendo

“…tusisubiri hadi rushwa itokee, tutengenezea mazingira ya kukabiliana na rushwa na kutoa elimu kwa umma”

“Sisi JamiiForums tunashiriki mapambano dhidi ya rushwa kwa vitendo, mwananchi popote alipo JamiiForums imetengeneza uwanja unaokuruhusu kutoa taarifa na faragha zao zitalindwa (anonymous); ukitupa taarifa za rushwa na ubadhirifu, tutahakikisha zinafanyiwa kazi,” - Maxence Melo

Kassim Majaliwa: Rushwa ni adui wa Haki na Maendeleo, pia hudumaza maadili katika Taifa

Rushwa ni adui wa Haki na Maendeleo, pia hudumaza maadili katika Taifa

Taasisi zetu za kupambana na Rushwa (Bara na Zanzibar) zimejitahidi kuboresha utendaji. Hatua zinachukuliwa haraka tofauti na awali. Siku hii leo kwa Afrika inaadhimishwa Tanzania, Zanzibar.

Hotuba ya Rais wa Zanzibar, DK. Hussein Mwinyi

Awali ya yote namshukuru Mungu Kwa kutuweka salama na pia naishukuru Jamhuri ya Muungano kwa kuipa fursa Zanzibar kuandaa maadhimisho haya.

Jamhuri ya Tanzania ni mwanachama wa umoja wa Afrika na imesaini mikataba ya umoja huo katika kuendeleza mapamabano dhidi ya rushwa kwa Afrika hivyo ni lazima tuungane na nchi nyingine katika kuadhimisha maadhimisho haya.

Kwa kutambua ubaya na athari za rushwa nchi wanachama wameamua kuitangaza 12 Julai kuwa ni sku ya kuadhimisha kupinga vitendo vya rushwa, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Mikakati na Mifumo ya Wazi ya Usimamizi ya Fedha za UVIKO-19"

Katika ahadi zangu wakati nachukua madaraka niliahidi kupambana na rushwa bila kuona aibu wala kumuonea haya mtu na naendelea kutekeleza na pia serikali ya Jamhuri inaendelea kupambana na kuchukua hatua dhidi ya rushwa kwani rushwa na uhujumu uchumi ni adui wa taifa na maendeleo.

Napenda kuwahimiza watu na watanzania wenzangu pia na taasisi binafsi wachukue vitendo vya rushwa na watoe taarifa za watu wanaojihusisha na rushwa ya aina yoyote, mapambano dhidi ya rushwa si ya taasisi za dini pekee bali ni ya kila mmoja wetu.

Waalimu, wazazi, taasisi za dini na watu wote muwafundishe vijana wetu madhara ya rushwa na pia wajue wana jukumu la kuto ataarifa kwenye vyombo vinavyohusika na Kupambana na rushwa kwani vyombo hivyo haviwezi kufanya kazi peke yake bali vinawahitaji ninyi wote.

Tunaanza Ziara rasmi ndani ya mwezi huu katika maeneo yote ambayo fedha za #UVIKO19 zimefika. Ningependa niwaambie wanaohusika wote wahakikishe wana maelezo mazuri. Na kazi hizo ziwe zina ubora unaoendana na fedha zilizotolewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom