Maadhimisho ya Siku Kuu ya wafanyakazi duniani, nchini Tanzania Kauli Mbiu ya Mei Mosi 2021: “Masilahi Bora, Mishahara Juu, Kazi iendelee”

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Heri ya siku kuu ya wafanyakazi! Hii ni siku iliyobeba matumaini makubwa kwa wafanyakazi wote Tanzania.

Baada ya kupandisha mishahara kwa mara ya mwisho July 2015 (by Kikwete) ni takribani miaka 6 sasa wafanyakazi wameambulia patupu.

Matarajio kutoka kwa Rais:
1. Kuhimiza kufanya kazi kwa weledi, juhudi na maarifa
2. Kupandisha kima cha chini cha mishahara
3. Kupandisha madaraja 'mseleleko' kwa ajira mpya za 2012 na 2013 ambao hawajawahi kupanda.
4. Kupandisha madaraja wafanyakazi wenye miaka zaidi ya minne kazini.
5. Kupandisha mishahara 'annual increments'
6. Kutoa ajira kwa wahitimu
7. Malipo ya wastaafu
8. Kurekebisha kikokotoo
9. Kupunguza makato ya HESLB
10. Kurekebisha sheria ya Fao la kujitoa

Tuna Imani na Samia
 
Hakika leo tutazijua rangi zake zote!
Muda utaongea ingawa namuamini Sana 70%.
 
tunawatakia maadhimisho mema.
msitusahau na sisi wakulima japo sio siku ya wakulima.
 
Tunako kwenda kuna hatari MTU aliyeajiliwa mwaka 2012 na 2014 watakuwa na mshahara unaofanana.
 
11. Kuondoa limit ya wategemezi kwenye bima ya afya.

Jana aunt kanipigia ananiomba nimkatie bima nikasikitika sana. Amenilea na kunisomesha tangu darasa la pili.
 
Angeongeza mshahara Mwendazake angepata legacy kubwa sana.Lakini sasa karma ni mbaya sana tenda wema mapema.
 
Matumaini kwa Raisi Samia Suluhu yamekuwa makubwa sana, ila muwe makini maana asipofanya mnavyotarajia wengine mtaishia kupata pressure, usimtegemee mwanadamu, mtegemee MUNGU maana yeye ndiye Tumaini la uhakika, binafsi Mimi mwanzoni nilimwamini sana Magufuri, lakini mambo yalipobadilika niliumia sana maana nilikuwa nimemwani 100%. Usimtegemee mwanadamu, quote my words
 
Back
Top Bottom