Maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Muungano, Dkt. Philip Mpango aziongoza Dodoma

Leo ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe zimeshaanza kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma na anaeongoza ni makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango
Kwa nini sherehe zinafanyika ukumbini badala ya viwanja vya wazi? Ni nini lengo la utaratibu huu?
 
Mama kiguru na njia ughaibuni wiki na ushehe!!
Mama ana mafaili 'mazito' mezani. Amejipa off kwanza akayatafakari kabla hajadondoka sahihi.
Moja ya mafaili yanahusu tenguzi na teuzi za baadhi ya wazito. Usimbeze, pengine na wewe ukaula zamu hii. 😀😀😀
 
Kwani aliyeomba kuungana na mwenzake ni Nyerere au Karume?
Suala la nani kaomba siyo la muhimu Mwagito. We elewa tu kuwa huu Muungano Samia asingevuka Chumbe bila passport.

We jiulize kwa nini makao makuu ya Muungani ni Dodoma na siyo Mji Mkongwe?

Jiulize Zanzibar walikuwa consulted yalipohamishiwa Dodoma toka Dar?
 
Wapi iliandikwa lazima ifanywe uwanjani?
Nafkiri kiitifaki ya kijeshi anayekagua gwaride la vyombo vya ulinzi ni Rais tu ambaye ni Amiri jeshi na si vinginevyo, so wameona wafanye ukumbininkwa mtindo wa kikongamano kwakuwa Rais hayupo maana ndio mamlaka yake. (ni uelewa wangu huo)
 
Leo ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe zimeshaanza kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma na anaeongoza ni makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango

Kuwa nami kwa yatakayojiri
=========

=> Viongozi wa dini zote wameshatoa sala na dua kwa ajili ya mjumuiko huu

=> Anayeongea sasa ni waziri Simbachawene na anatambulisha viongozi waliohudhuria, pia amesema sherehe zimefana.

=> Sasa ni salamu kutoka kwa waziri Suleiman Jaffo ambae anahusika na Muungano na anaaza kwa kumshukuru makamu wa Rais anaemuwakilisha Rais wa Jamhuri. Anawashukuru wote kwa kazi wakiadhimisha miaka 58 watanzania wakiwa na amani na furaha.

=> Sasa ni burudani kuhusu muungano

=> Anaeongea sasa ni waziri mkuu, Kassim Majaliwa na anaanza kwa kusema 'wasiotaka muungano wajitoe' kisha anatambua wageni waliohudhuria.
Wafanyakazi wajiandae kisaikorojia,inawezekana hata mei mosi hakasepa, sasahivi kapata kichaka cha kujificha USA 🤣🤣🤣
 
Nafkiri kiitifaki ya kijeshi anayekagua gwaride la vyombo vya ulinzi ni Rais tu ambaye ni Amiri jeshi na si vinginevyo, so wameona wafanye ukumbininkwa mtindo wa kikongamano kwakuwa Rais hayupo maana ndio mamlaka yake. (ni uelewa wangu huo)
Bora umesema kwa uelewa wako
 
Mama ana mafaili 'mazito' mezani. Amejipa off kwanza akayatafakari kabla hajadondoka sahihi.
Moja ya mafaili yanahusu tenguzi na teuzi za baadhi ya wazito. Usimbeze, pengine na wewe ukaula zamu hii. 😀😀😀

Kaka kwa speech hizi za "kuleni kwa urefu wa kamba zenu" "bei zitaendelea kupanda na kupanda"

Tumeula wa chuya na mawe juu!!
 
Hivi kweli watu wamepanga ratiba ya Rais bila kujali tuna Sherehe za Muungano ambazo Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuwepo?
Sherehe za kitaifa kama hizi ni za CiC na vyombo vyake. Ndio maana gwaride huwa inakuwepo na kukaguliwa na Amiri Jeshi Mkuu.

Hivi pale ukumbini kutakuwepo na gwaride mbele ya Makamu wa Rais?
Hilo linafikirisha
 
Leo ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe zimeshaanza kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma na anaeongoza ni makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi hawajahudhuria sherehe za leo.

Kuwa nami kwa yatakayojiri
=========

=> Viongozi wa dini zote wameshatoa sala na dua kwa ajili ya mjumuiko huu

=> Anayeongea sasa ni waziri Simbachawene na anatambulisha viongozi waliohudhuria, pia amesema sherehe zimefana.

=> Sasa ni salamu kutoka kwa waziri Suleiman Jaffo ambae anahusika na Muungano na anaaza kwa kumshukuru makamu wa Rais anaemuwakilisha Rais wa Jamhuri. Anawashukuru wote kwa kazi wakiadhimisha miaka 58 watanzania wakiwa na amani na furaha.

=> Sasa ni burudani kuhusu muungano

=> Anaeongea sasa ni waziri mkuu, Kassim Majaliwa na anaanza kwa kusema 'wasiotaka muungano wajitoe' kisha anatambua wageni waliohudhuria. Waziri mkuu amesema maandalizi ya sensa yamefikia 81%.

Philip Mpango: Tunapoazimisha miaka 58 ya muungano hatuna budi kuwakumbuka waasisi wetu wa muungano kwa maono yao makubwa, uamuzi wa busara, hekima na utashi wa kurasimisha na kuunganisha nchi mbili huru kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jambo kubwa ambalo watanzania wote tunapaswa kulifanya kwa wazee wetu hawa ni kuendelea kuenzi, kuimarisha na kuudumisha muungano.

Muungano hauna tija. Sasa kama upande wa pili wote wanaususia itakuaje kwa mfano
 
Hata mei mosi anaweza asiwepo maana watumishi wanamsubiri sana anaweza ishia huko huko pole watumishi
 
Back
Top Bottom