Maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Muungano, Dkt. Philip Mpango aziongoza Dodoma

Leo ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe zimeshaanza kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma na anaeongoza ni makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi hawajahudhuria sherehe za leo.

Kuwa nami kwa yatakayojiri
=========

=> Viongozi wa dini zote wameshatoa sala na dua kwa ajili ya mjumuiko huu

=> Anayeongea sasa ni waziri Simbachawene na anatambulisha viongozi waliohudhuria, pia amesema sherehe zimefana.

=> Sasa ni salamu kutoka kwa waziri Suleiman Jaffo ambae anahusika na Muungano na anaaza kwa kumshukuru makamu wa Rais anaemuwakilisha Rais wa Jamhuri. Anawashukuru wote kwa kazi wakiadhimisha miaka 58 watanzania wakiwa na amani na furaha.

=> Sasa ni burudani kuhusu muungano

=> Anaeongea sasa ni waziri mkuu, Kassim Majaliwa na anaanza kwa kusema 'wasiotaka muungano wajitoe' kisha anatambua wageni waliohudhuria. Waziri mkuu amesema maandalizi ya sensa yamefikia 81%.

Philip Mpango: Tunapoazimisha miaka 58 ya muungano hatuna budi kuwakumbuka waasisi wetu wa muungano kwa maono yao makubwa, uamuzi wa busara, hekima na utashi wa kurasimisha na kuunganisha nchi mbili huru kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jambo kubwa ambalo watanzania wote tunapaswa kulifanya kwa wazee wetu hawa ni kuendelea kuenzi, kuimarisha na kuudumisha muungano.
Kweli marekani tamu.
 
Hivi kweli watu wamepanga ratiba ya Rais bila kujali tuna Sherehe za Muungano ambazo Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuwepo?
Sherehe za kitaifa kama hizi ni za CiC na vyombo vyake. Ndio maana gwaride huwa inakuwepo na kukaguliwa na Amiri Jeshi Mkuu.

Hivi pale ukumbini kutakuwepo na gwaride mbele ya Makamu wa Rais?
Mama yuko katika ibada akija apa wajinga watamuona mpyaaa tour ni mbwembwe tu
 
Back
Top Bottom