Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yafana sana Mjini Dodoma Aprili 26, 2017

Bibititi1

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
464
218
Siku ya leo Tanzania inaadhimisha miaka 53 ya Muungano mjini Dodoma mgeni Rasmi akiwa Rais wa awamu ya Tano Mh Rais John Pombe Magufuli.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa Nchi huru mbili yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Nchi hizi mbili ziliingia kwenye Mkataba wa Muungano mnamo tarehe 22 Aprili, 1964 na kuwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 26 Aprili, 1964.

Muungano huu ni wa serikali mbili, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoshughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Zanzibar.

Katika sherehe hizi za Muungano waziri mwenye dhamana na Muungano amewataka watanzania kuendelea kudumisha na kuimarisha ushirikiano ktk kilimo pamoja na biashara na uwekezaji

Ukiangalia kwa sasa nchi yetu ipo katika ujenzi wa uchumi wa viwanda lazima watanzania wajikite kwenye uwekezaji ili kuimarisha maisha yao.

Watanzania mnatakiwa kufahamu tupo karne ya 22 inayohusisha maendeleo ya sayansi na Teknolojia tujitahidi kuwekeza katika sekta ya sayansi na Teknolojia ili kuujenga uchumi wa viwanda.

Sekta ya MAWASILIANO nchini Tanzania imechangia asilimia 2.1 ya pato la Taifa kwa mwaka 2015 ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 1 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganisha na mwaka 2009.

Kwa njia pekee ya Tanzania sasa ni kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano hasa kampuni za simu katika kununua hisa ili kuweza kukuza kiwango cha ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchi.

Tayari kampuni ya Vodacom imeweka hisa zake sokoni kwa wateja wake kuweza kujipatia nafasi ya umiliki na kuchangia kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

Nadhani muda si mrefu na makampuni Kama Tigo na Airtel nayo yatakamilisha mchakato wa ofa ya kuuza hisa zake kuziweka sokoni kuweka sawa mazingira ya ushindani na kumpa mwananchi uwezo wa kuchagua.

Soko la Data limekadiriwa kuwa na thamani ya takribani dola 966 milioni kwa mwaka 2016 -2017 na ukuaji wake ni takribani asilimia 6. Hii inachangia zaidi na ongezeko la wateja wa Intaneti

Watanzania mnatakiwa kujitokeza mstari wa mbele katika kuwekeza katika soko la hisa kwani kutaongeza upanuzi wa vipato vya kilasiku, pamoja na pato la Taifa katika ulipaji kodi kama tutaamua kuwekeza ktk kampuni hizi za Mawasiliano alimaliza Waziri huyo mwenye dhamana ya Muungano.

Joseph Kwizera

Dodoma Leo.
26|04|2017

======

Imetumwa : April 26th, 2017

DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli , leo tarehe 26 Aprili 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalama lililoandaliwa kwa heshima yake, Rais Magufuli amewahakikisia Watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.

“Muungano ndio silaha yetu, Ni nguvu yetu, Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano kwa nguvu zote, Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye” amesema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.

Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuunda Taifa moja lenye nguvu.

Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na Kukabiliana na matatizo ya umaskini na ukosefu wa ajira, kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini, reli na nchi kavu.

Aidha, Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha Makao Makuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.

“Niwahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa” amesema Rais Magufuli.

Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuria na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa Viongozi Waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Viongozi wa Chama na Serikali.

Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni “Miaka 53 ya Muungano, Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii”.

Pia soma:

Rais Magufuli afuta shamrashamra za miaka 52 ya Muungano, fedha zikajenge barabara Mwanza

Rais Magufuli aadhimisha sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Jiji la Dodoma
 
Siku ya leo Tanzania inaadhimisha miaka 53 ya Muungano mjini Dodoma mgeni Rasmi akiwa Rais wa awamu ya Tano Mh Rais John Pombe Magufuli.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa Nchi huru mbili yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Nchi hizi mbili ziliingia kwenye Mkataba wa Muungano mnamo tarehe 22 Aprili, 1964 na kuwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 26 Aprili, 1964.

Muungano huu ni wa serikali mbili, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoshughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Zanzibar.

Katika sherehe hizi za Muungano waziri mwenye dhamana na Muungano amewataka watanzania kuendelea kudumisha na kuimarisha ushirikiano ktk kilimo pamoja na biashara na uwekezaji

Ukiangalia kwa sasa nchi yetu ipo katika ujenzi wa uchumi wa viwanda lazima watanzania wajikite kwenye uwekezaji ili kuimarisha maisha yao.

Watanzania mnatakiwa kufahamu tupo karne ya 22 inayohusisha maendeleo ya sayansi na Teknolojia tujitahidi kuwekeza katika sekta ya sayansi na Teknolojia ili kuujenga uchumi wa viwanda.

Sekta ya MAWASILIANO nchini Tanzania imechangia asilimia 2.1 ya pato la Taifa kwa mwaka 2015 ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 1 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganisha na mwaka 2009.

Kwa njia pekee ya Tanzania sasa ni kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano hasa kampuni za simu katika kununua hisa ili kuweza kukuza kiwango cha ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchi.

Tayari kampuni ya Vodacom imeweka hisa zake sokoni kwa wateja wake kuweza kujipatia nafasi ya umiliki na kuchangia kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

Nadhani muda si mrefu na makampuni Kama Tigo na Airtel nayo yatakamilisha mchakato wa ofa ya kuuza hisa zake kuziweka sokoni kuweka sawa mazingira ya ushindani na kumpa mwananchi uwezo wa kuchagua.

Soko la Data limekadiriwa kuwa na thamani ya takribani dola 966 milioni kwa mwaka 2016 -2017 na ukuaji wake ni takribani asilimia 6. Hii inachangia zaidi na ongezeko la wateja wa Intaneti

Watanzania mnatakiwa kujitokeza mstari wa mbele katika kuwekeza katika soko la hisa kwani kutaongeza upanuzi wa vipato vya kilasiku, pamoja na pato la Taifa katika ulipaji kodi kama tutaamua kuwekeza ktk kampuni hizi za Mawasiliano alimaliza Waziri huyo mwenye dhamana ya Muungano.

Joseph Kwizera

Dodoma Leo.
26|04|2017
Safi sana,dunia imebadilika sana tupo katika karne ya teknolojia na nyanja ya mawasiliano ndio kitu pekee kinachoongoza dunia ya utandawazi.tuwekezeni kwenye nyanja hii ya mawasiliano kwa kuwekeza na kumiliki kampuni kwa kununua hisa za kampuni hizo ili uwe sehemu ya umiliki wa kampuni, Vodacom naona wameweka wazi hisa zao ili kuwawezesha watanzania kumiliki kampuni hiyo.
 
Yeah mambo yameongezeka mpka muda unaonekana hautoshi ndio maana nimekuwa nawashauri wengi wanaojiona wapo busy wawekeze hata kwenye hisa ninaamini fursa hii vijana wengi haita wapita hakika.
[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG] kwa maisha ya baadae
 
Siku ya leo Tanzania inaadhimisha miaka 53 ya Muungano mjini Dodoma mgeni Rasmi akiwa Rais wa awamu ya Tano Mh Rais John Pombe Magufuli.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa Nchi huru mbili yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Nchi hizi mbili ziliingia kwenye Mkataba wa Muungano mnamo tarehe 22 Aprili, 1964 na kuwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 26 Aprili, 1964.

Muungano huu ni wa serikali mbili, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoshughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Zanzibar.

Katika sherehe hizi za Muungano waziri mwenye dhamana na Muungano amewataka watanzania kuendelea kudumisha na kuimarisha ushirikiano ktk kilimo pamoja na biashara na uwekezaji

Ukiangalia kwa sasa nchi yetu ipo katika ujenzi wa uchumi wa viwanda lazima watanzania wajikite kwenye uwekezaji ili kuimarisha maisha yao.

Watanzania mnatakiwa kufahamu tupo karne ya 22 inayohusisha maendeleo ya sayansi na Teknolojia tujitahidi kuwekeza katika sekta ya sayansi na Teknolojia ili kuujenga uchumi wa viwanda.

Sekta ya MAWASILIANO nchini Tanzania imechangia asilimia 2.1 ya pato la Taifa kwa mwaka 2015 ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 1 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganisha na mwaka 2009.

Kwa njia pekee ya Tanzania sasa ni kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano hasa kampuni za simu katika kununua hisa ili kuweza kukuza kiwango cha ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchi.

Tayari kampuni ya Vodacom imeweka hisa zake sokoni kwa wateja wake kuweza kujipatia nafasi ya umiliki na kuchangia kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

Nadhani muda si mrefu na makampuni Kama Tigo na Airtel nayo yatakamilisha mchakato wa ofa ya kuuza hisa zake kuziweka sokoni kuweka sawa mazingira ya ushindani na kumpa mwananchi uwezo wa kuchagua.

Soko la Data limekadiriwa kuwa na thamani ya takribani dola 966 milioni kwa mwaka 2016 -2017 na ukuaji wake ni takribani asilimia 6. Hii inachangia zaidi na ongezeko la wateja wa Intaneti

Watanzania mnatakiwa kujitokeza mstari wa mbele katika kuwekeza katika soko la hisa kwani kutaongeza upanuzi wa vipato vya kilasiku, pamoja na pato la Taifa katika ulipaji kodi kama tutaamua kuwekeza ktk kampuni hizi za Mawasiliano alimaliza Waziri huyo mwenye dhamana ya Muungano.

Joseph Kwizera

Dodoma Leo.
26|04|2017
Asante kwa Ushauri kwa Watanzania maana hawakawi kulalamika kwamba hisa zinauzwa kwa matajiri pekee......
Tanzania ya viwanda itakuja kwa kuanza kuwekeza.
Ndugu yangu Mtanzania wekeza na Vodacom kwa kununua hisa zao.
Mimi nalifahamu vizuri soko la hisa hakika halitakuacha mtupu lazima ubarikiwe katika kampuni hii.
 
Back
Top Bottom