Maadhimisho ya Miaka 57 ya Mapinduzi Zanzibar: Rais Mwinyi asema Mapinduzi katika uchumi yatajibu changamoto za Wazanzibari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,672
2,000
Zanzibar inaadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi leo na baadhi ya masuala aliyozungumzia Rais Hussein Mwinyi katika hotuba yake ni kama ifuatavyo:

Dkt. Hussein Mwinyi amesema Zanzibar inapaswa kuleta Mapinduzi katika sekta ya Uvuvi ili wavuvi waweze kuvua kwa zana za kisasa, na rasilimali za Bahari kuu ziweze kuwanufaisha Wazanzibari.

Kuhusu sekta ya Kilimo, Rais Mwinyi amesema ni lazima kuwe na Mapinduzi ili Wakulima wapate kuongeza tija, kuinua mazao ya Karafuu na Mwani, na vilevile kuondoa utegemezi wa Chakula kutoka nje.

Akizungumzia Sheria na Taasisi, Dkt. Mwinyi amesema Mapinduzi ni muhimu ili kumuwezesha Mzanzibari mwenye #Biashara kufanya shughuli zake bila vikwazo.

Aidha, amesema Mapinduzi yanahitajika kwenye Utumishi wa Umma kujenga Uwajibikaji, kuboresha huduma pamoja na maslahi ya Watumishi wa Umma.

Amesisitiza kuwa, Mapinduzi hayo yanawezekana ikiwa Uchumi utafunguliwa kwa kuweka mazingira mazuri ya ukuaji na Makusanyo ya Kodi yakiongezeka.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,513
2,000
...
Kuhusu sekta ya Kilimo, Rais Mwinyi amesema ni lazima kuwe na Mapinduzi ili Wakulima wapate kuongeza tija, kuinua mazao ya Karafuu na Mwani, na vilevile kuondoa utegemezi wa Chakula kutoka nje
...
... sijamwelewa vizuri hapo kwenye red unless "nje" anayomaanisha ni nje ya Tanzania na sio nje ya Zanzibar kwani hilo haliepukiki. Kwa jiografia yake, mazao mengi hayastawi Zanzibar; mfano rahisi ni maharage yanayopendwa sana huko huko Zanzibar! Ngano pia hawataagiza kutoka "nje"? Maana chapati, maandazi, na mikate ni vyakula pendwa Zanzibar.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom